True love ni ngumu kama barter trade

True love ni ngumu kama barter trade

Migomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
945
Reaction score
1,339
History inatuonyesha kuwa miaka ya nyuma kabla ya kugunduliwa pesa watu waliuziana kwa mtindo wa kitu kwa kitu (barter trade) ambapo kama wewe ni mvuvi ambaye una samaki na unahitaji mbuzi basi itabidi utafute mtu ambaye ana mbuzi na wakati huo huo anahitaji samaki. Hivyo kupata tu mwenye mbuzi sio ishu, ishu ni kwamba naye awe anataka samaki tena aina ile ambayo wewe unayo na kwa kiasi cha kutosha kutoa mbuzi wake. Jambo hilo linaweza kuwa mfano mzuri kwenye mapenzi.

Bwana Nyangema labda interest yako ni mwanamke mweusi, mrefu, aliyejazia, mwenye elimu ya chuo, anayejua kupika na kutunza familia.

Bibie Mrembolisious anataka handsome boy, mwenye kazi nzuri, mwenye huruma, awe mrefu, mwenye umbo la kimazoezi na anayejua kuvaa.

Sasa hapo tabu ni Nyangema aliye single kukutana na Mrembolisious aliye single. Utaona ni rahisi kumpata mwenye sifa zako lakini asipende za kwako au mkawa na sifa lakini tayari mna uhusiano. Au ikakulazimu kuvumilia hizo chache alizonazo na ukiwa kwenye uhusiano ukajikuta unakutana na yule haswaa mwenye sifa zako na ukashindwa kuvumilia (mchepuko)

Kwa kuliona hilo wazungu wamejaribu kutengeneza hadi mitandao ya ku-date ili kuweka medium ya kukutanisha hizo sifa (kama pesa inavyotumika kutatua changamoto za barter trade) lakini bado humo namo kumejaa uongo na biashara.

Hivyo kiujumla kupata anayekupenda na ukampenda ni ngumu sana, ishu ni kukubaliana/kuridhika na kile ulichopata.
 
Mchagua nazi.... Wengi wanataka waoe wenye sifa za malaika sijui watawatoa wapi karne hii hahahaa emu waende mbinguni wakachumbie malaika mkiruhusiwa njooeni nao muoane.... Na Mungu haezi ruhusu maana mtamuharibia malaika wake kwa tabia zenu ... Bora tuvumiliane tu wanadamu[emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji13] [emoji12]
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Pagumu hapo!

Nilitegemea kupata mke bora huko kwenye Makanisa, na penyewe pamechafuka tu.
 
ukijifanya una true love siku hizi utaumia sana , mheshimu mwenza wako mtendee haki ila akikuzingua achana nae.
kwa uzoefu wangu watu wanaojiumiza kwa ajili ya wengine ndio wanaoongoza kwa majuto duniani
 
Mmh kwa hiyo unakuwa na false love? maisha ya ivo magum sana,
 
siwezi kuuita ni false, ila ukinijali mimi nitakujali, ukinizingua naachana na wewe,
wewe upo radhi kumg'ang'ania mtu asiyekujali kisa unampenda?
Ilo nalo neno! mi ndo maana nimeamua kuupiga chini huo upuuz! ngja nifanye yangu kwanza
 
watu wanataka awe na mtu mwenye kila sifa mpya inayotoka magazetini, movie, bungeni , vitabu vya hadithi,awe mzuri, asiwe na kasoro kimwili&kiroho, awe mchumi,project manager, mchapa kazi, mwenye hela, asiwe mbahili, mwenye kuweka akiba, awe na umbo la kati , awe mchapa kazi, fundi kitandani na kila nikimuhitaji home nimkute sasa cjui anatafuta saangapi[emoji15] [emoji15] [emoji15] utafikiri mchaguaji huyo yeye kakamilikq.

vijana hawajitambui na wote wamegeuka drama qeens&Kings

tuwaombee
 
Back
Top Bottom