Trilioni 424? Tuacheni utani jamani

Nimekuwa nikisikia wafanyabiashara wengi wazalendo wakilalamikia ukubwa wa makisio ya kodi toka TRA. Wengi wetu tumekuwa tukiwabeza na kubaki yatima wakilazimika kulipa kodi hizo kwa shingo upande wakikosa mtu wa kuwatetea. Tumewaona wengi wakifungiwa biashara zao tena kwa masimango makubwa. Nafikiri Mungu ameamua kudhihirisha wazi kile kilio chao. Nasubiri ACACIA wakifungiwa biashara zao kwa kushindwa kulipa hayo malimbikizo kama tunavyofanyiwa sisi wanyonge. Kwa mbaaali naanza kumuelewa TL
 


hizo hela zote nani alikuwa anaongoza na aliyesababisha tuibiwe kiasi hicho?
 
Mkuu swala hapa ni hao watu wa mahesabu tu yaani wanatumia kanuni gani kupata izo figure? Walisoma wapi?
Wapuuzi wanamfurahisha sizonje.....ukweli wanao!!! Vita Vya uchumi sio sawa na vita na Lisu!!! Ajiaangalie!! Aulize Venezuela!!!
 
TRA wako sahihi! Acha Acacia wajibu kwa hoja za kueleweka! Kilichopandisha juu ni riba na adhabu! Riba ya miaka 17 siyo ya kitoto!
 
Mimi siamini kama ile ndoto yangu ya kumiliki Noah ndio imeshatimia, wife nimempeleka driving school kabisa mana siku kila mtu anachukua Noah yake pale bandarini tusisumbuane. Kila mtanzania kuwa na Noah inawezekana.

Dogo dezo inaua pambana hio ndoto yako itakua usingizi wa baada ya kugonga kande kwa bamia chakula cha mchana
We pambana thamini baskeli yako kuliko VX clCruiser ta jirani yako
 
Kama mtu hana utaalam na masuala ya fiscal policy (kodi) na uchumi usijiingize kujadili kadhia ya Acacia kudaiwa kodi, penality na riba. Madai ya TRA ni sahihi kabisa. Kama Acacia wataona wameonewa watakata rufaa kwa mujibu wa sheria. Ninawashuri Watanzania watumie mfano huu kubaini namna ambavyo nchi yetu imekuwa ikiibiwa na hawa manyang'au wa Canada, Amerika, Australia na Ulaya.
 
Watoza ushuru wa TRA, elimu yao ni ya kuungaunga. Wengiwao, ni wale ambao pass marks zao ziligoma kuwawezesha kuendelea na masomo kwenye mfumo rasmi. Huwa hawana hata reasoning. Matokeo yake wameifanya Tanzania nzima ionekane ni nchi ya mazezeta, kutoka viongozi, wasomi, mpaka washangiliaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukilipwa hizi tirioni 424,basi na Mimi,kuna uwezekano ndoto zangu za kumiliki hammer na vogue,zikatimia,na wake zangu watatu kila mmoja akaendesha Lexus ya kisasa,na ile ndoto yangu ya kuanzisha kiwanda cha nafaka itatimia,mweeee,
Ni utani tu waungwana,
 
Hii Nchi ni tajiri hamuamini, kama naiona hiyo budgets ya matrilion..
Haki tena ata watu wa South Africa wangezamia kwetu badala ya kukimbilia kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hidden agenda hapa. Huenda kuna watu wameishagundua anataka kitu gani cha kumfutahisha. Watu hao wapo kila mahali na wanatoa takwimu ambazo ni invalid ili jamaa akenue. Suala hili linadhihirishwa na kuchelewa kwa tra tangu 2002 hadi leo kuassess kampuni hiyo huku brela wakisema hawaijui! Hapa anahujumiwa mr misifa waziwazi.
 
Hiyo invoice umepewa wewe !?
 
watanzania ifike Hatua tuelewane, tunashangaa y'all Acacia Lakini hatushangai y'all FATUMA KARUME KUDAI BILLIONI MOJA Kwa kuzuiwa kuongea

Tunadai malimbikizo ya kodi pamoja na FAINI Hebu tuelewane hapa
 
Hili jukwaa siku izi limekuwa ka kijiwe cha kahawa. Anaeongea sana ndo mjuaji. Mnaopinga hili jambo mbona hamji na hesabu kuonesha haiwezekani zaidi ya kutumia hisia tu?Tufanye hamna takwim za mapato,hivi ni kweli wamepeleka tu hayo madai bila maelezo yyt ni jinsi gani hicho kias kimefika?


Yani wanaopinga wanatumia data na reference za watuhumiwa na WANAHITIMISHA KABISA KUWA HAIWEZEKANI mara mtaji wao ni mdogo mara cjui nn....

NDIO MAANA WANASEMA MMEWEKEWA BETRI.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
Tuliposema tutajenga "Tanzania ya viwanda" hamkutuelewa. Sasa mtaanza kutuelewa vizuri pale Trilioni 424 zitakapoingia kwenye account ya TRA. Maana tayari ACCACIA wako benki wanashughulikia ku-transfer huo mzigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…