Tribute To Ephraim Kibonde: Ni Mtangazaji Multi Talented, Entertainer, Comedian na Politician wa Kiaina. He Was Great!, Pengo Lake Halitazibika!.

Wanabodi,

Juzi tumemzika mmoja wa Watangazaji nguli kabisa wa Radio na TV Tanzania, Ephraim Samson Kibonde. Usingizi umenikatika ghafla, usiku huu wa manane, naomba usishutuke kusema labda... sio Ephraim Kibonde amenitokea, bali usingizi umekata, hivyo nikaanza kumkumbuka Kibonde na kumtafakari, na ndio sasa na realize kuwa kumbe huyu jamaa ni kweli amekufa na hatuko nae. Hivyo hili ni bandiko la Tribute ya kuangazia Mazuri yake, pamoja na mazuri yote ya Kibonde tutakayoyaeleza humu, hatumaanishi kuwa Kibonde alikuwa malaika, no, Kibonde alikuwa binaadamu tuu kama sisi binaadamu wengine wote, hivyo nawaomba sana, tusiuzungumzie wa mashaifu ya ubinaadamu wake, au mapungufu yake, Tribute ni kuzungumzia Ukuu wake, concentrations on the positives not the negatives, please tumkumbuke kwa mema tuu and lets celebrate his achievements.
Karibuni.

Kiumri mimi ni mkubwa kwa Kibonde, nimemtangulia kwenye fani kwa miaka 5, mimi nimeanza mwaka 1990 RTD ndipo 1995 nikahamia DTV, Ephraim ameanza kazi mwaka 1995 CTN, mwaka 1996 CTN ikajiunga na DTV kuunda AMG, hivyo tukakutana na Kibonde Channel Ten, na hata wakati wa Kipindi cha Kiti Moto, siku nikipata udhuru, ni Kibonde aliniendeshea kipindi changu, na hata baada ya Channel Ten mimi nikaanzisha PPR, baada ya ile ajali yangu ya piki piki, ni Kibonde tena aliyeniendeshea vipindi vyangu vya Saba Saba pamoja na Jerry Muro, na mpaka umauti unamkuta, ni Kibonde na Aboubakar Liongo, ndio huwa natumia sauti zao zenye punch kubwa, kufanya jingle zozote za PPR, hivyo you can imagine the loss!.

Kibonde ni Multi Talented Radio/ TV Broadcaster, Anchorman na TalkShow Host.
Japo kila mtu mwenye sauti anaweza kuwa mtangazaji wa radio na TV, lakini kuwa mtangazaji mzuri, ni lazima uwe na kipaji cha utangazaji, Ephrain Kibonde, alikuwa ni mtangazaji mwenye vipaji lukuki.
  1. Sio kila mtangazaji anaweza kusoma habari, kuna watangazaji maalum wa habari, yaani newsreader, Ephraim Kibonde alisoma habari
  2. Sio kila mtangazaji anaweza kuwa Anchor Man, sio wengi wanafahamu kuwa zile taarifa za habari zinazosomwa kwenye redio na TV, watangazaji hawatio kichwani, bali wanaandikia script, wao kazi yao ni kusoma tuu, wanaitwa News Reader. Watangazaji wenye uwezo mkubwa wa kutangaza Live News Interactive kutokea Studio wanaitwa Anchorman (kutangaza live kutokea studio bila script) Ephraim Kibonde, alikuwa ni Anchorman.
  3. Sio kila mtangazaji anaweza kutangaza Piece to Camera, ni ule uwezo wa kutangaza live au kurekodiwa live kutoka eneo la tukio bila kuwa na scrip yoyote, Ephraim Kibonde ndie Mtangazaji Mtanzania wa kwanza kufanya live piece to camera kwenye CNN ile 1998 ubalozi wa Marekani jiji Dar es Salaam uliposhambuliwa shambulio la Kigaidi.
  4. Kwa vile lugha ya Taifa ni Kiswahili, hivyo watangazaji wengi wako fluent kwa lugha moja tuu ya Kiswahili, Ephraim Kibonde ni mmoja wa Watangazaji wa Tanzania ambao ni bi-lingua, ana flow vizuri kwa lugha mbili ya Kiswahili na Kiingereza.
  5. Sio kila Mtangazaji anaweza kutengeneza matangazo, ili mtangazaji aweze kutengeneza matangazo ya biashara, sauri take kazima uwe ya kushibam yaani punch, Kibonde alikuwa na wa kui controll sauti yake na kutengeneza punch ya aina yoyote kwa tangazo la aina yoyote, hivyo alilamba deals nyingi za matangazo, yakiwemo matangazo kutoka kwangu.
  6. Ili utengeneza tangazo zuri, ni lazima uandae script nzuri, ili kuandaa script nzuri, ni lazima uwe creative kwa kuwa na kipaji cha creativity, Ephraim Kibonde, alikuwa very creative, kuna matangazo wewe unampa tuu concept, kila kitu anamaliza mwenyewe. Hivyo tasnia ya matangazo ya biashara, imepata pigo kubwa ambalo halitazibika leo au kesho.
  7. Kwenye fani ya Utangazaji, kuna kitu kinaitwa "presence", sijui Kiswahili chake, ila ni ile hali ya mtangaji wa habari akisoma ile habari, anaonyesha yeye ndio anaijue ile habari halafu anatujulisha sisi kutokea kichwani mwake. Wengi wa watangazaji wa sasa wa habari, anatangaza habari huku hata mtoto mdogo anajua kuwa huyu anasoma, presence haipo. Kufuatia presence hii, Kibonde alimiliki vizuri vipindi vyake, mfano kipindi kama Maisha ni Nyumba, kwa sasa kime flop baada ya kumkosa Kibonde, hivyo hata Jahazi, Gardner G. Habash, ana mtihani mgumu sana kuziba pengo la Kibonde ili kipindi kisi flop, but Jahazi bila Kibonde, will neber be the same again.
  8. Utangazaji una maeneo tofauti tofauti, sio kila mtangazaji anaweza kutangaza mpira, boxing, michezo, mimi nikiwa mmoja wapo, siwezi kutangaza mpira, Ephraim Kibonde, anatangaza kila kitu, kuanzia habari, michezo, mpira, ngumi, Ephraim Kibonde ni miongoni mwa Watangazaji walioweza kutangaza kila kitu, popote utakapompeleka Kibonde, ata fit.
  9. Zaidi ya Utangazaji, Kibonde pia alikuwa ni entertainer, mfurahishaji na mshereheshaji na mchekeshaji, a comedian, hivyo japo Watangazaji wengi huweza kuwa ma MC wazuri, hata mimi nilikuwaga MC, ila kuwa MC ambaye watu hawataboreka, watafurahi, watachangamka na watavunjika sana mbavu, Ephraim ni mmoja wa watu hawa, hivyo sio tuu tasnia ya habari ndio imepata pigo, bali tasnia ya ma MC na entertainment industry pia imepata pigo,
  10. Ephraim Kibonde, alikuwa ni mtu wa watu, anajichanganya na watu wa aina yoyote, mcheshi wakati wote, mchangamfu wakati wote, mtani wa hapa na pale, anasalimia wote, siku akimzungumzia Zitto, utafikiri Kibonde ni ACT, siku akizungumzia Chadema, utafikiri Kibonde ni Chadema, kwa vile CCM ndio chama kubwa na chama tawala, Ephraim Kibonde alionekana kama mshabiki wa CCM, in short, Ephraim Kibonde alipenda watu wote, ni mtu wa wote na uthibitisho ni kwenye msiba wake, watu wamejitokeza kumsindikiza.
Nenda kwa Amani Ephraim Kibonde, sijui ni uliumia sana kifo cha Ruge, ukaumia sana Ruge akakuona akakuita, nisije nikasema sana nawe akaita mtu, nenda tuu salama, wasalimie kina Mzee David Wakati, Julius Ntaisanga, Misanya Bingi na watangazaji wengine wote.

RIP RAFIKI NA MTANGAZAJI MWENZANGU EPHRAIM SAMSON KIBONDE.

KALALE PEMA PEPONI.

PASKALI.

Kaka Paskali niliwahi toa defence hii kwa Ndugu Efraim Samson Kibonde ...
"Wahanga wa matokeo gentleman division tuko wengi, kinachotofuatisha ni mazingira yetu ya kuingia ktk janga hili, ukipata story ya kila mtu kwa uhalisia na siyo utetezi unapata somo....

Kingine tukubaliane kuwa o'level au a'level sekondari education siyo njia pekee ya kutufikisha ktk stashahada, shahada na uzamili...., na siyo lazima kuung'ang'ania mtaala wa tanzania ktk kujipatia weredi hususani ktk duni hii ya sasa.

Kibonde kama wahanga wengine asihesabiwe kuwa ni form iv leaver kama tayari ameshaichukua line nyingine ya taaluma ambayo inamtofautisha kabisa na mhitimu tu wa kidato cha nne au sita.

Bado nakubaliana sana na wengi wanomtizama kibonde kama mwanaharakati aliyejipambanua kupitia karama na fursa za weledi wa dunia ya sasa hatimaye kuwa gumzo la nchi yetu. Tupende tusipende, daima tunayo fursa ya kupata jema ndani ya ubaya....tukajifunza huko leo na kesho......."

Signature

"SAFARI YA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI BADO NI NDEFU NA YENYE VIKWAZO LUKUKI"

"..leo naomba kusimamia ninachoamini juu yake....awali nakubaliana sana na Kaka Paskali....umegusaa poteeee.

Pili niliwahi husika ktk kuhakikisha kuwa MC wa shughuli ya Taasisi yetu Elimu ni Ephraim, nilijitahidi kujenga hoja bila hata kuwa na direct contact za Kibonde, hatukuwa na urafiki wala ukaribu bali kuna dada mmoja wa pale Clouds ambaye nature ya kazi yake na yangu zilikuwa na umapacha....Mimi nikimpatia ushirikiano wa matangazo toka kwetu na yeye kuhakikisha jingles zinakwenda hewani kwa sauti ama ya Kibonde ama kijana yule aliyeko E-fm sasa....

Yule patner wangu in business kati ya hapa na Clouds akani link na Kibonde tukakutana naye...it was fruitfully meeting and the next committee meeting aaah sikuwa msemaji mimi...Kibonde mwenyewe akaimeza kamati .....

siku ikafika tukio la Graduation ....tunafika eneo la tukio mitambo na kila kitu iko intact ikirindima na kuburudisha watu....ghafla sauti inayorindima kuratibu si ya Ephraim Kibonde looooooh nilihisi dunia imeniangukia na sina kifua cha kuhimili uzito wake....

Ghafla simuni napewa Asalaaam aleikhum....unajua nilishindwa kuiitikia , akaendelea kwa kunitaka radhi kwa maneno machache , Ndg yangu ......nafahamu nimekufanya uonekane kuwa ni mtu wa hovyo kwa sababu tu umenipendekeza na kunipigania mimi Mkosefu Ephraim Kibonde, nimelazimika kusafiri asubuhi hii kushughulikia jambo la Mzee mmoja wa hapa Arusha na ndio nimeshuka toka kwenye ndege....Nikamkatiza kwa swali....Gadna asingeliweza kuifanya kazi hii on behalf? Ndugu yangu ,nisamehe kwanza , pili huyo aliye na Mic ni kama mimi ama Gadna hebu muombe Profesa aruhusu kazi iendelee. Narudi kesho tuongee....

Jamaa zangu pale wanaoniamini waliona nilivodondoshwa na kubomoka....lakini watu fitna wakaanza oooh unajua oooh vile aaaah lazima Prof ajulishwe....

Nikiwa ktk msongo huo na shughuli ikiwa kama dak 5 bado kuanza rasmi nikasikia jina langu kwenye speakers ....uonane na Prof ...ktk chumba Maalum Wageni maalum.....looooh nikajua moto umewaka...

Nafika nakuta prof yuko full smile na kunitaka niimpe full support MC na kwmba nduguyo Kibonde ana dharura inayomuhusu Mzee Lowassa...tukacheka pamoja kazi ikaanzaaa ikaisha vyemaaaa

Aliporudi yule dada aliungana nami ktk huzuni ya kilichotokea basi aka initiate meeting....siku najipanga kwenda Clouds kikazi na kufahamu siku ya kukutana namuona Kibonde huyooooo anapaki gari yake moja kwa kwa moja mapokezi akaniulizia ...nikajitokeza tukakumbatiana na kama kawaida ukitizamana na Kibonde uso kwa uso lazima wote mtachekaaa tu....maana mie mie alinipiga " Ebana vipi?" tukacheka , sasa hebu niache nikakusafishe kwa Professa huko juu ghorofani maana nakuona umechafuka sana...tukacheka tena, nikamwambia hewala kaka kama ni hilo panda ngazi ukirudi utanikuta hapa afisini kwangu....baada ya 15minutes akashuka , Mzee amenisamahe na amenielewa , sikuwa na neno bora sana kwake ....Kaka umefanya vyema sanaaaaa. Nikamsindikikza mpaka pale pale Parking Udsm opp na NBC akaingia kwenye Premio yake akaondoka.... To me it was cleansing ....

Tunaye kijana wake hapa ameanza Mafunzo ya Kitaaluma ya Tehama....
Alikuwa muungwana sanaaaaa Efraim Kibonde.

Mungu akurehemu rafiki, mchapakazi Efraim Kibonde
 
We unataka akasome nini kwa mfano, aende QT ili uendelee kumdhihaki kwa kumwita MEMKWA au?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndo tunapokwama wabongo. Tunaogopa kunangwa. Audience yetu inaishia hapa hapa TZ na kuishia kulima MPUNGA huko mbarali=80% ya income inatoka kwenye kilimo badala ya Sanaa yet tunajiita wasanii nguli badala ya mkulima nguli.
NB: KANSIIME ni degree holder akienda London kufanya show tiket zinaisha kabla hajakwea pipa Entebbe. Masanja anaruka-ruka mara mchungaji, mara mkulima mara muuza ubwabwa yaan vurugu tu/haeleweki.Mameneja nao NGUMBARU wanachojua ni kuvaa miwani myeusi misibani lakini kichwani hamna kitu
 
Ukisikia pengo lale halizibiki Ephraim ameacha tundu sio pengo maana hadi leo hii JAHAZI bado linapigwa mawimbi halijasimama teeenaaaa kama alivyokuwa Kibonde nimeamini kuna nafasi ambazo akiondoka mtu kweli hazizibiki... tunakumis sana bro. RIP
 
maisha yake nje ya kazi sijui ila kwenye utangazaji jamaa bado tulikuwa tunamhitaji, ndio hivyo Mungu kampenda zaidi
 
Back
Top Bottom