Treni za Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni za Mwakyembe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kijakazi, Aug 11, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Pamoja na kwamba ni jambo zuri kuanzisha au kufufua treni kwa usafiri wa abiria katika jiji la Dar, na watu wengi wamekuwa wakitegemea kuwa ni moja ya utatuzi wa foleni hapa Dar mimi natofautiana kidogo na nitaelezea hapa!

  Hizi treni hazitapunguza foleni hata asilimia moja kwa maana watakao kuwa wanazitumia ni watu wa kipato cha chini na wengi wao watakuwa wanakwenda BURE, kwa maana hapa tatizo kubwa katika nchi yetu hatujaweza bado kumanage chaos na sioni ni jinsi gani wanavyoweza kufanya hiyo huduma ikawa nzuri kiasi kwamba inishawishi mimi na niache gari langu na kuja kupanda treni Ubungo, sioni ni jinsi gani wanavyoweza kuzuia watu wasidandie juu kama India!
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  wewe utaendelea na gari yako
  waacha wengine wapate ahueni ya daladala

  msongamano wa wtu angalau utapungua
   
 3. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  We ndugu yangu mbona mgumu sana kubadilika? Au ni kwa sababu umeshakuwa conditioned na ahadi hewa za haohao CCM ndiyo maana humuamini yeyote kutoka chama hicho akikuahidi ukombozi? wako wachache miongoni mwao tunawaamini wataweza! please change your mind set! Kwani weye ukikaa juu ya kichwa cha treni si utafika kariakoo huku ukila upepo kuliko joto la ndani ya Daladala yahe?
   
 4. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Kwanza nakuomba ndugu yangu ubadilishe kichwa cha habari kutoka "Treni za Mwakyembe" kusomeka TRENI ZA WAKOLONI.

  Hivi kama issue ni kupunguza foleni wangejenga treni kutoka bagamoyo hadi posta, wawapitie watu wa mikocheni, kawe, msasani, tegeta, mbezi beach, sinza, k'nyama, kidondoni maana maeneo hayo ndio yana kila mtu na gari lake.

  Ila sisi watanzania hatujaielewa serikali ya ccm, kwa kuwa imeshindwa kutimiza ahadi zake zitakazoweza kuonekana kama vile kujenga flyover ubungo, wameamua kufanya kitu kwa watanzania masikini walio wengi ambao watakiona, kufufua treni ya mkoloni (kuweka kiraka), maana walau wengi wa huko buguruni wataona serikali imefanya kitu wakati wengine wao wenye magari watakuwa wanakaa foleni mara mbili zaidi ili kupisha muda wa treni kukatisha.

  Me niliposikia kutakuwa na usafiri wa treni dar es salaam, nilichojua kuwa serikali itajenga treni za chini za kisasai, ambazo zitatumia umeme. Kumbe, imefanya bora tufanye.

  2015 hambaki hata mkila ma*i yenu hatuwaonei huruma
   
 5. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  bora watu hawatakaa ndani ya mabasi kubanana kwa masaa na kusikia kelele za makondakta na madereva wakiwa wanaendesha ovyo kuwahi upande wa pili.


  ni idea nzuri sana,na hata nchi zingine rush hour traffic huwa bado ipo kama kawa.
   
 6. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Nafikiri hujanielewa mimi nimetoa maoni yangu hasa kutokana na watu wengi kufikiri kwamba treni zitapunguza foleni na wala sijatilia shaka kuhusu kuanza kwake kazi, nilichosema ni kwamba watu wengi wa kawaida bado watarudi kwenye dala dala kwa maana bado hatujaweza kumanage chaos, mfano mdogo sana angalia ferry ya Kigamboni kwa nini magari yanatumbikia baharini? Uongozi wa feri unashindwa kumanage chaos kitu ambacho ni rahisi sana kwa mfano kwa nini kusiwe na mpangilio wa kuruhusu aidha magari kwanza au watu wakati wote wa kushuka na kupanda ili kuondoa chaos matokeao yake watu na magari wanachanganyika, ni kutokana na uzoefu kama huo ndio umenifanya nifikiri kwamba hata hizo treni zitakuwa ni hivyo hivyo sioni jinsi ambavyo wanaweza kumanage hiyo chaos!
   
 7. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  sana kabisa
   
 8. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Sio kweli, Kenya wanayo hiyo ya tangu mkoloni na kama sisi hiyo ya Ubungo inatembea na inapita sehemu kubwa ya watu kama vile ubungo na hakuna anayetaka kupanda zaidi ya watu wasioweza kulipa nauli za daladala wanadandia na kupanda juu ya treni ni chaos kuliko hata dala dala, kwa hiyo shida hapa ni jinsi ya kuifanya iwe bora kuliko dala dala na hiyo sio kazi rahisi kama unavyofikiri!

   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Lets wait and see mapungufu yatafanyiwa kazi!
  Kama ulaya wanaweza why not us?
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  tatizo la wengi wabongo kila kitu wanabisha hata kabla hakijaanza
  wlaibisha kujengwa barabara ya kawawa, upanuzi wa sam nujoma nk
  wacha tren ianze watamanage tu suala la kusafiri bure halitakuwepo mtu anatakiwa akate ticketi ya wiki au mwezi
  kutakuwa na machine card reader vituoni hakuna kuingia bure.
  litapunguza sana tatizo la usafiri dar. kuhusu tegeta kuna reli kama hawajangoa itajengwa ingine
  tuanze kwanza na reli iliopo nyingine itajegwa tu.
  we kama una kigari chako wengine hatuna na itasave sana muda na fedha za wengi kuishia ktk mafuta
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu acha treni ianze kazi hayo mingine ni mataokeo tu.
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hajui kwamba kuna wengine wanaendesha magari yao binafsi kwenda posta kukwepa vurugu za dala dala? At least usafiri watren ukiwepo watu tutapunguza kugombania usafiri kama kweli watatimiza ahadi. Aafu kwani mwakyembe kasema itakuwa bure?
   
 13. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280

  basi mfuate umwambie as una haraka sana, subiri ianze ionekane, be +.

  sio unafikiria umasikini tu, kwani utajua kama mwenye pesa kapanda anataka kufika mjini haraka?
   
 14. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Treni + mabasi yaendayo kwa kasi= Nafuu zaidi ya msongamano
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa ulitaka zisiwepo?
   
 16. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  ticket ya WEEK au MWEZI nadhani wewe uko nje ya tanzania i mean ULAYA au MAREKANI. hivi mwananchi wa tandika au kigogo anayefanyakazi pugu road kwenye viwanda vya wahindi au makampuni ya ulinzi. NAULI YAKE YA SIKU TU NI YA KUBAHATISHA SEMBUSE HIYO TICKET YA WEEK AU MWEZI au hujawaona hata hii nauli ya daladala ya sh 300 mtu anaomba kwa konda kuwa ana 200. nakushauri acha kubeba maboksi rudi nyumbani uone halisi ya mwananchi wa tz
   
 17. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Nafikiri una uwezo mkubwa sana wa uelewa tofauti na watu wengi sana hapa, wanaongea vitu kama vile wako sayari nyingine na wanashabikia vitu bila kufanya tathimini ya kutosha hivyo vitu vyote Dar vipo mfano kituo cha mabasi Ubungo kuna milango wa kuzunguka (Revolving door) iliwekwa (kwa pesa nyingi!) ili mtu mmoja mmoja aingie nakuzuia chaos, kaangalie sasa hivi wameufunga na kamba na hauzunguki, ukienda feri ambayo wamajenga kwamba unanunua ticketi kuna sehemu unapanchi geti linafungunguka unapita (mtu mmoja mmoja) lakini hawatumii matokeo yake wameweka mtu, na kuna chaos ya ajabu mpaka magari yanatumbukia baharini, sasa vitu kama hivi kwa nini niamini kwamba hii treni itakuwa tofauti? kama wizara ya uchukuzi wameshindwa kufanya kivuko kiwe efficient wataweza treni?

   
 18. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  wewe ndio unapotosha hoja, mimi sijapinga ila nimetoa changa moto nipinge jambo zuri kama hilo kwa lengo gani?
  hayo yote uliyoandika yapo sijui ticket machine reader kivukoni ferry ipo iliwekwa sasa kaangalie kama inatumika na magari na watu bado wanajichanganya, nenda Ubungo bus terminal kuna milango iliwekwa ya kuzunguka lengo likiwa ni kuruhusu mtu mmoja kwa kwa wakati lakini wameifunga na kamba na haizunguki na watu wote wanagombania kupita na wengine bila tiketi na vyote hivyo chini ya wizara hiyo hiyo kama sikosei sasa kwa nini nisihoji ufanisi wa hiyo treni?

   
 19. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,716
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  yeah...tuanze na kisha hayo matatizo tutayajua huko mbele na kuyapatia ufumbuzi!!!
   
 20. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Waweke na mabehewa ya kubeba magari ili asubuhi nilipakie gari mpaka mjini,ni hepukane na foleni
   
Loading...