Ponjoro wa Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 5, 2024
- 2,882
- 7,916
Treni ya Mwendokasi (SGR) imeripotiwa kuacha njia yake na kupata ajali katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo ikiwa inatokea Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma ambapo Abiria wawili walioongea na AyoTV wamesema hawajamuona yeyote aliyejeruhiwa isipokuwa ni hofu tu iliyowapata wachache.
“Haijafahamika chanzo ila treni imehama kwenye reli kama inavyoonekana kwenye video na picha, hatujaambiwa chochote ila kuna Viongozi na Maaskari wameanza kufika hapa sio mbali na hapa Stesheni Ruvu” - amesema mmoja wa Abiria hao. Msemaji wa Shirika la Reli (TRC) Fredy Mwanjala akizungumza na AyoTV kwa njia ya simu, amekiri kupokea taarifa za ajali hiyo ambapo tumemnukuu akisema “tumepokea hizo taarifa za Treni kupata ajali na kwa kuwa ndio kwanza tumezipata kwa sasa Mkurugenzi Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara wote tunaelekea eneo la tukio na tunatoa taarifa baadae baada ya kufanya tathmini ya kina na Wataalamu”
Soma Pia: TRC: Ajali imesababiswa na hitilafu za kiuendeshaji