Tray la mayai 4000 tsh.



Tunahitaji watu kama wewe,asante kwa kutujuza.Umenipatia jambo ambalo sikutarajia kama linaweza kutendeka katika Dunia hii.
 
Senior Manager, kuna mdau mmoja anaitwa Tafakuru, anakampuni yake inaitwa Maverick Supplies, anapatikana kwa namba hii 0713079661. Na anapost yake humu jamvini, anasema hiyo ndiyo biashara yake. Unaweza ukawasiliana nae


~Jamani hii ni forum ya kibiashara na mambo yanayoendana na hayo. Ni mshtuko na mshangao mkubwa kama watu wengine mnaona kama ni jamvi la majungu, umbea, uzushi na kupoteza muda. Entrepreneur, sijui unaushaidi gani halisi au hata wa kimazingira kuambatanisha na wimbi la upotoshaji unaojaribu kuuandika kila leo kuhusiana na kampuni yangu. Sikujui hunijui wala hatujawai kukwaruzana popote. Taarifa chafu za mimi kujitangaza nnafanya biashara hii sijajua wewe unazitoa wapi? kama ni ushindani wa kibiashara, unachofanya ni mchezo tope ambao haukufikishi popote. How stupid would i be to air my contacts with such a business in Tz!!!!!
~Nnakuona kama mtu mwenye mawazo finyu, mchanga kibiashara, mmbea na usie na kazi za kufanya. Nmekusaidia tu ila kashfa huwa haijibiwi.
 

Mkuu hapo kwenye red ni maneno mazito sana, hebu pitia hizi post zako kwanza, halafu nitarudi labda utaniambia ni uposhoshaji gani ninaoufanya kila leo kwa ushahidi wa maandishi kama ninavyofanya mimi hapa chini.
 
picha yenyewe inatisha hata ya hayo mayai yanavyoonekana hata huwezi kuyanunua, cheki humohttp://www.mwananchi.co.tz/mwananchi-jumapili/41-biashara-mwananchi-jumapili/20576-mayai-feki-yatua-dar
 

Mkuu mimi siwezi malumbano hivyo sitajikita kwenye hizo kashfa zako ulizonirushia kwani sijaona kama zinabadili ukweli kuhusu mimi ila kabla sijakuomba msamaa, hebu pia post hizi
1. 1. Nnasupply mayai na matikiti maji idadi yeyote unayotaka
2. Kwa anayehitaji mayai ya kisasa tuwasiliane

Sina haja ya kukwambia namna ninavyoiheshimu privacy yako , but kuweka contact zako humu inamaana zimeingia kwenye public domain. Vilevile ninaheshimu nisiemjua na ninayemjua pia awe mkubwa kunizidi au mdogo wa kumzaa.

Mkuu hakuna sehemu yoyote katika post yoyote niliwahi kumkashfu yeyote muchless wewe (iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi). Nipo makini sana kuchagua aina ya maneno ninayoyatumia. Ukipata muda angalia michango yangu kwenye post zako zote, kama kuna sehemu nimesema (hata by implication) kuwa unasambaza mayai feki. Senior Manager wa JF alihitaji information za mtu anayesambaza mayai na wewe ulikuwa na bango lako lenye mawasiliano yako na kampuni yako hivyo nikaona ni vyema kumpatia bila kucomment chochote.

Napenda uelewe kuwa sipo kwenye biashara ya ufugaji wa kuku, uuzaji wa mayai au uuzaji wa matikiti maji. Na wala sitegemei kuwa kwenye biashara ya namna hii, ingawa nilishawahi kujishughulisha na ufugaji mkubwa wa kuku wakati nikiwa mdogo. Hata hivyo hukuhitaji kutumia hasira sana na kurusha hayo makombora yako na kashfa mfululizo kwani hata habari iliyotolewa na Tanzania daima (ambayo mimi niliipost humu) inazungumzia kampuni ya Morning Fresh na si Maverick Supplies.

Sasa mpaka hapa kama kweli wewe ni muungwana na uungwana ni vitendo, basi utakuwa umeshajua ni nani anastahili kuomba mwenzie msamaha na kufuta kauli. Kama ni mimi basi nisamehe na kama ni wewe basi nimeshakusameee. Tuendeleze mapambano katika kujenga uchumi wa familia zetu na nchi kwa ujumla, kwani malumbano ya namna hii hayana afya. Aksante
 
kiumri au kimtaji?
 

yani hapa cancer nnje nnje....kwa hali hii tutapona kweli ??? dah Ukicheck kuku wanapewa ARV, mayai feki nayo kibao, chips nazo wanakaanga na mafuta ya transfomer, samaki wanaokaangwa feri ndio uchafu mtupu. TFDA ina kazi au manufaa gani kwa jamii sasa ?? Huo utumbo (intestine) utastahimili haya masumu kweli ??? dah...Tanzania cjui tunaelekea wapi kwa kweli.....Mi na suggest watu wa namna hii wakikamatwa wapigwe life improsonment cz huu ni uuaji kabisa.
 
kuna taarifa kuwa huko kenya kuna wazalishaji wakubwa wa mayai ambao walitarajia ku export mayai nchi za kiarabu lakini kutokana kuwa chini ya kiwango(ubora) wakashindwa, sasa waya peleke wapi? kuliko kuyateteza wanayauza kwa bei ya hasara kwa wachuuzi wanaojua udhaifu wa TZ katika kudhibiti bidhaa mbovu, hizi habari nimezipata kwa rafiki mtanzania anaish kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…