Tray la mayai 4000 tsh. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tray la mayai 4000 tsh.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Senior Boss, Feb 28, 2012.

 1. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Hello,

  Nimepata habari ya kwamba tray la mayai kutoka nnje ya nchi linauzwa kwa shs. 4000. Ningependa kujua haya mayai yanatoka nchi gani ?? Yamethibitishwa na tbs kuwa yanafaa kwa matumizi ya binadanu ?? Pia nauliza ni wapi naweza kuyapata mayai haya ili nitambue ubora wake?

  Ahsanteni !!
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  biashara huria, mayai yanaingia toka Mombasa - Holoholo - Tanga then Dar. ni kwa semi teller's -- nafikiri tray itafika 1500 muda si mwingi. ila msiniulize gharama za uzalishaji wao wanafanyaje fanyaje.

  si mnataka biashara na East Africa sasa shida ipo wapi? jiandaeni bado na sekta zingine.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hii ni changamoto

  watanzania tunahitaji kujua mbinu halisi ya sector hii ya uzalishaji wa mayai na sio kupinga tuu haya mayai yanayoingia

  mbona hatupingi na kukataa used Toyota vehicles zinazoingizwa kama utitiri kutoka japan, si kuna magari yalivumbuliwa na wanajeshi yanaitwa 'nyumbu' , mbona hatuyanunui?

  tutafakari nje ya box
   
 4. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  sawa mi nataka kujua hapa dar haya mayai ntayapata wapi??? I need tha exact location ​wanapoyauza. nataka nikayacheck !!!
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Senior Manager, kuna mdau mmoja anaitwa Tafakuru, anakampuni yake inaitwa Maverick Supplies, anapatikana kwa namba hii 0713079661. Na anapost yake humu jamvini, anasema hiyo ndiyo biashara yake. Unaweza ukawasiliana nae
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli kwa teknolojia ya sasa hiyo inawezekana kabisa, hapo kinaweza kufanyika kwa wale kuku kuwa genetical modified wakazalisha mayai hata 5 kwa siku na kwa chakula kile kile then automatically gharama ya kuzalisha mayai inapungua na bei itashuka tu. Cha kujiuliza ni kuwa hivyo viwanda au makampuni wanaofanya hivyo wako wapi? na je wanatumia teknolojia gani? Pia ni muhimu mayai hayo yakawa na utambulisho kuwa ni yanayotokana na GMO..ili kuwapa watumiaji fursa ya kuchagua kati ya mayai ya GMO na yale ya kawaida..
   
 7. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  TAHADHARI
  mayayi haya hayana ubora kwa afya ya BINADAMU.
   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tahadhari hii ingetolewa na TFDA kwenye vyombo vya habari tungewaokoa wengi, but kwa kuwa nao wamelala basi kila mtu atasema lake? Hebu wasaidie basi
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kweli, tunahitaji kutoka nje ya box, na kupokea hizi changamoto katika sekta hii, lakini kama mayai haya yanatengenezwa viwandani kwa kemikali kama wanavyosema wadau, basi hakuna tena suala la ushindani au masoko. Tunahitaji ushindani na Soko linaloheshimu Afya ya Binadamu
   
 10. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ubora gani mkuu, tufafanulie... je, hayana proteini au yana additivies.. tuambie mkuu sio kutupa hearsay!
   
 11. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ..kulen vya dezo,muote mikia, ..mayai hayo,yamepgwa marufuku tz,yana chemical nyngi sana ambayo ni hatar kwa binadam.
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot] Shehena ya mayai feki yakamatwa Dar

  Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, imekamata shehena ya mayai yakiwa ndani ya lori katika eneo la Kitunda Dar es Salaam ambayo yalikuwa yakisafirishwa bila kibali.[/FONT][FONT=&quot] Shehena hiyo iliyokuwa na zaidi ya trei 500, ilikamatwa siku chache baada ya vyombo vya habari kuripoti kuingizwa kwa mayai feki kutoka nchini Kenya ambayo yanauzwa kwa bei rahisi hali inayozua shaka kwa walaji.[/FONT]


  [FONT=&quot]Tanzania Daima ilishuhudia shehena hiyo ikiwa kwenye lori lenye namba za usajili T 423 BCQ likiwa limeegeshwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Mayai hayo huuzwa kati ya sh 4,000 hadi 5,000 kwa trei moja wakati bei halali sokoni kwa sasa ni kati y ash 6,000 hadi 7,000 kwa trei.[/FONT][FONT=&quot] Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa wizara hiyo, Dk. Winston Mleche, alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa, walisema mayai hayo ni mali ya kampuni ya Morning Fresh kutoka Mkuranga mkoani Pwani na kwamba wanayazalisha huko.[/FONT]


  [FONT=&quot]Kutokana na hali hiyo waziri mwenye dhamana, Dk. David Mathayo, ameagiza maofisa wake kwenda Mkuranga kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali ikiwemo kujua kama mayai hayo yanazalishwa huko au la. Dk. Mleche alikiri kuwa hata ofisa mifugo wa wilaya ya Mkuranga hana taarifa za kampuni hiyo iliyotajwa kuwa mmiliki wa mayai yaliyokamatwa kwani haina uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa kama hicho.[/FONT][FONT=&quot]Alisema kuwa hata wanapokwenda kwenye eneo la kampuni, maofisa hukataliwa kuingia ndani vinginevyo watimize masharti likiwemo la kufanyiwa uhakiki wa kuoga kabla hawajaingia kiwandani jambo ambalo hupingwa na maofisa hao.[/FONT]


  [FONT=&quot]Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri Mathayo alisema hivi sasa kuna taarifa za kuingizwa kwa mayai mengi kutoka nchi jirani hali ambayo husababisha soko la ndani kudorora.[/FONT][FONT=&quot]Kwa mujibu wa Dk. Mathayo, serikali ilishapiga marufuku uingizwaji wa mayai ya kula kutoka nje ili kudhibiti pia magonjwa na kwamba hata leseni ya aina hiyo hawatoi badala yake imeruhusu kuingizwa nchini mayai ya mbegu pekee.[/FONT][FONT=&quot]Pamoja na mambo mengine alisema hakuna upungufu wa mayai nchini hivyo hakuna sababu ya kuendelea kulididimiza soko la ndani na kuwanufaisha wengine.[/FONT]


  [FONT=&quot]Hivi karibuni kumeripotiwa kuingiliwa kwa soko la mayai hapa nchini kutokana na kuingizwa kwa mayai kutoka Kenya hali inayosababisha wafanyabiashara wa nchini kupata wakati mgumu.Mayai hayo yanaelezwa kuwa siyo makubwa kama yanayopatikana nchini na yanapovunjwa hayana kiini na baadhi maji yake yamechanganyika na vitu mithili ya nyuzi zenye rangi nyekundu.[/FONT][FONT=&quot] Mayai hayo yanapatikana kwa wingi maeneo ya Kariakoo na Gongo la Mboto na yanauzwa kwa wingi kwa wafanyabiashara wa vyakula jijini [/FONT]Dar es Salaam

  Source. Tanzania Daima
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ahsante sana.
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mkila hayo mayai ya GMO wanaume mtaota matiti!! Msije mkasema hamkuonywa!!
   
 15. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  TBS? Hii hii ya kwetu TZ? Unachekesha!
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  kila sehemu kuna biashara huria lakini lazima nchi husika kuwakinga wazalishaji wadogo wadogo wa ndani; bila hivyo wananchi wa hali ya chini wataishi maisha ya ajabu mno;

  sasa nakumbuka utabiri wa Idd Simba umetimia - hali inazidi kuwa mbaya mno na hii inachangia kwa kiasi kikubwa na soko huria mi naliita soko holela - uingizwaji nchini ya vitu kwa njia ya magendo; vitu feki;

  kwa hawa wenzangu mie kwa sasa wanakula mlo mmoja - na hii ni hatari kwa usalama wa taifa letu maana siku wakichoka kuvumilia itakuwa zahma.

  Lazima tuanze kuwalinda hawa watu wa chini kabisa ambao wengi wanategemea ujasiliamali mdogo mdogo kupata kipato chao.
   
 17. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Unajua mfanya biashara huyu ni mjinga sana na sidhan kama zimetimia sawa sawa kichwani mwake....Yeye bahati nzuri amegundua njia ya kuzalisha mayai kwa gharama ndogo na yanayafaa kuliwa....sasa nini kitu gani kilichomfanya ashushe bei kiasi hicho mpaka media na watu kibao wamebaki wakijiuliza inakua vipi ??

  Mimi nilitegemea yeye angeendelea kuuza bei ile ile 6000-7000 kimya kimya kwa usiri mkubwa huku akipiga profit margins kubwa sana. Naamini angefanya hivyo ndani ya mwaka angekua mbali sana. Ona sasa media na wananchi washakinukisha mitaani. Mda si mrefu atafungiwa na atadorora mbayaa. I cant believe HE/SHE amechezea shillingi chooni kiasi hicho (a waste of opportunity). Huko aliko ajue kwamba "Senior Manager wa jamii forum a.k.a The Untouchable" NIMEMDHARAU KIMBWAAA !!! Hio opportunity angepewa mtu kama shirima, massawe au mushi wa kiboroloni pale ndani ya mwaka angekua anapush Range Rover Sports kitaani.

  "Wote tumepewa akili lakini sio wote wanajua kuzitumia effectively"
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nilishajiamuliaga nkiwa na field visit nanunua kuanzia nyama mpaka mayai uko uko!
  Maana TFDA na TBS wakiwekwa sawa watakuja na majibu kuwa yako sawa.
  Ivi majibu ya wale samaki toka Japan yalikuwaje vile?
   
 19. matron

  matron Member

  #19
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 13
  STUNNING
  Manufacturing fake eggs
  In China there are fake schools and classes that teach a variety of blatant fraud technology, even eggs can be modulated by chemical materials, but also be able to fry cook, is currently the most popular False course.

  Step 1 modulation of raw materials

  Using 7 kinds of chemical materials, see pic below
  [​IMG]


  Fake egg was made from calcium carbonate, starch, resin, gelatin, alum and other chemical products.
  Step 2 egg production
  Raw egg into the mold to 2 / 3 full, put calcium chloride, colouring die, theegg appears on the film been announced.
  [​IMG]
  The 'yolk' is shaped in the round mould. 'Magic water'containing calcium chloride is used.
  [​IMG]

  By adding a yellow pigment and become raw egg yolk..
  Step 3 fake egg shape
  In the mold into 1 / 3 raw egg white, like the first package, like dumplingsinto the egg yolk, egg white into another, into the magic water, ashell eggs willcome slowly.Naked eggshape to 1 hour to dry after washing with water, at shellsready.


  Step 4


  Sewing lines through the use of eggs, immersed in paraffin wax,calcium carbonate, such as modulation of the eggshell into a solution, repeatedseveral times until the shell a little dry, immersion in cold water pumpingline shape, this point, the egg has been put on a false cloak , You're done.

  [​IMG]

  Hard shells are formed by soaking in paraffin wax onto the egg, which are thenleft to dry.
  [​IMG]

  [​IMG]


  Oh yeah The Egg isready. The artificial egg shell is very fragile and break easily but whocares!!
  Look so real


  [​IMG]

  Many small bubbles is formed during frying the egg but not manypeople can tell the difference.
  The egg look exactly the same, and the eggs taste better than real but you areadding to the
  statistic of food poisoning person.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  Why make fake eggs?
  Because of money.

  The cost of fakeegg is only 0.55 Yuan/kg, while the true [WINDOWS-1252?]eggs' market price is5.6 Yuan/kg.
  Cases of problem foods and food poisoning are widely reported inMainland China over the last few years. In 2001, there were 185 cases of foodpoisoning, affecting about 15,715 people and causing 146 deaths. The casesdoubled in 2002. In 2003, the number of reported cases was ten times more thanthat in 2001, and the number of people suffered wasashighas29,660,including262 deathsNowInSept2008Neary53,000 Chinese children sick from contaminated milk; 4 have died
   
 20. matron

  matron Member

  #20
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 13
  Hii nimeianzishia thread ila nimeona pia niilete hapa kwa faida ya wengi,jamani tuwe macho
   
Loading...