Transfer Window 2014/2015, Special thread

Transfer Window 2014/2015, Special thread

Kiungo mkongwe wa Barcelona Xavi Hernandez (34) amekamilisha uhamisho wa kwenda Al Arabi ya Qatar.
 
Kiungo wa Southampton Adam Lallana (26) amehamia Liverpool kwa mkataba wa miaka 5 kwa dau la £25m na mshahara wa £100,000 kwa wiki.
 
Golikipa anayetisha kwenye Kombe la Dunia mMexico Guillermo Ochoa (28) sasa yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Barcelona. Timu za EPL zimeambiwa zisipoteze muda kumfuatilia.
View attachment 165750

Barcelona tayari wameshasajili makipa wawili mmoja katoka Ujerumani mwingine ni kipa wa timu ya taifa ya Chile Claudio Bravo .Sidhani kama watasajili kipa 3 ndani ya msimu mmoja
 
Mzee Wenger amesema HANA MPANGO na mshambuliaji mtata wa AC Milan Mario Balotelli (23) kwani anaye kinda anayetisha Joel Campbell ambaye anarudi klabuni msimu ujao.
View attachment 167264

AC Milan imesema inataka kupunguza mzigo wa gharama za mishahara kufuatia msimu mbaya. Lakini inataka kitita cha £29.5m kumwachia Balotelli.
arsenali itaishia kuchukuwa kombe la FA na jinsi kikosi kilivyo hakina uwezo wa kupambana na timu kubwa . hata hiyo UEFA tunaingia tu ila sio kwa kuchukua kombe.
ARSENAL aina kikosi imara
 
Arsenal inajipanga kumwaga £44m kuipiku ManUtd kumchukua kiungo anayetisha duniani kwa sasa - Arturo Vidal (27) wa Chile na Juventus. ManUtd iliweka day la £30m.
 
Jose Mourinho anajiandaa kumwaga £60m kumchukua kiungo kinda 'hot cake' anayetisha duniani kwa sasa Paul Pogba (21) kutoka Juventus.
 
Arsenal inajipanga kumwaga £44m kuipiku ManUtd kumchukua kiungo anayetisha duniani kwa sasa - Arturo Vidal (27) wa Chile na Juventus. ManUtd iliweka day la £30m.

Mkuu,

Man Utd wanaweza kumsajili huyo Arturo Vidal lakini Wenger yupo Brazil na yupo "busy".

Kama ikiwa Arsenal kweli wanashughulikia usajili makini kwa msimu ujao basi kuna wachezaji watatu ambao ni lazima wawasajili kufikia mwisho wa wiki ijayo.

Wachezaji hao ni Alexis Sanchez wa Barcelona ambae Liverpool pia wanamtaka na wanataka Barcelona wabadilishane kwa Luis Suarez.

Ikishindikana basi watamsajili Mario Balotelli kutoka AC Milan ambae nae amekasirishwa kwa kushutumiwa kutoisaidia Italy kuwenda raundi ya pili kwenye WC.

Mchezaji mwingine ni kiungo Morgan Schneiderlin wa France na Southampton ya Uingereza. Kiungo huyu bado ni mdogo kumlinganisha na Vidal(ingawa Arsenal wanaweza kuipiku Man Utd kwa kuongeza dau) lakini wanaangalia long term stability pale kwenye midfield kwa kuzingatia Mikael Arteta anaondoka baada ya msimu huu.

Pia Morgan Schneiderlin amewasaidia sana Southampton na pia anahesabika kama homegrown player ambae amekulia kwenye Southampton Academy.

Mchezaji wa tatu ni beki wa kulia Mathieu Debuchy ambae ni kutoka Newcastle ya Uingereza.

Huyu Debuchy huenda akasajiliwa kuziba nafasi ya Bacary Sagna ambae ameenda Man City.
 
Kiungo wa Athelic Bilbao Ander Herrera (25) amehamia ManUtd kwa dau la £29m baada ya kuvunja mkataba wake kwa kutumia 'buy-out clause' baada ya timu hiyo kukataa ofa ya £28.4m kutoka ManUrd. Herrera anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 5.
 
Athletic Bilbao imekataa kumuuza Ander Herrera. Hata hivyo Herrera atatumia kipengele kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuunua mkataba wake (buyout) kwa £29m halafu aende kurejeshewa fedha zake na ManUtd.

Bilbao walichemsha...kwani toka mwanzo Man United walipomeet release clause (ya £29m) ya kwenye mkataba wa Herrera, Bilbao walikuwa hawana ubavu wa kumzuia zaidi ya kumsikiliza Herrera. Hivyo ndivyo sheria za mikataba ya wachezaji wa soka zilivyo. Kwa mfano, release clause ya Messi ni £215m. Hivyo timu yoyote ikiweza kumeet hiyo clause, Barcelona wanakuwa hawana ubavu wa kukataa; si ndivyo walimvyo mvalue mchezaji wao.

Kiuhalisia Herrera haja buyout mkataba wake, kwani United ndiyo watalipa hiyo pesa.

Timu iki trigger tu release clause na kuimeet hakuna siasa tena hapo, kama watu walivyofikiri eti Bilbao wanataka pesa zaidi! Pesa zaidi za nini wakati walikwisha mvalue Herrera kwa £29m?

Release na buyout clauses ni utaratibu mzuri sana wa kuwafanya wachezaji wasiwe watumwa wa klabu.
 
Beki wa Newcastle na Ufaransa Mathieu Debuchy (28) anakaribia kutua Arsenal kuziba pengo la Bacary Sagna.
 
Beki wa Arsenal Thomas Vermaelen (28) anakaribia kutua ManUtd kwa dau la 11m.
 
Na sawa na kuwa na kisu, panga na shoka kwenye mapambano, vyote haviwezi kutumika pamoja
na mtu mmoja kwa wakati mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom