Transcend Vs Seagate

Mkuu Chief unaposema
"jifunze kitu kinaitwa RAID, unaweka HDD mbili kwa pamoja inakuwa HDD moja na kila kilicho kwenye hdd moja kinakuwa cloned na kuekwa hdd nyengine, hapa ikiharibika moja basi ya pili inakuwa na data zote, japo ni expensive sababu ni HDD mbili ila ni njia ya uhakika" hapa una maananisha kuwa unanunua HDD mbili au zaidi then huwa kuna namna ya kutengeneza hiyo RAID au una maanisha kuna tayari HDD ambazo ni RAID ambazo zinauzwa? if kuna namna ambayo IT Technician anaweza kutengeneza hiyo RAID je vitu gani vitahitajika vinunuliwe then mtu ampe IT Technician atengeneze? sorry nimeuliza nikiwa sina clue na hivi vitu so usinicheke au kushangaa, nina video zangu nyingi sana sasa sitaki zipotee japo nitazihifadhi kwenye gdrive but still nataka nizihifadhi na kwenye external HDD pia ili niweze kuzitumia kwa urahisi pindi ninapozihitaji
 
Unanunua hdd 2 za kawaida kuipata.

Kuna kitu kinaitwa Nas (network attached storage), inakuwa kama desktop ndogo na milango mingi ya HDD, hii inakupa Raid kirahisi



Ukinunua Nas huna Haja ya It kukutengenezea inakuwa tu na milango unapachika HDD zako, inakuja Na Apps zake za kuweka kwenye vifaa mbalimbali kama simu ili uweze ku access mafile yako popote.

Alternative unatumia Desktop ama laptop yenye uwezo wa kuingia HDD mbili hapa ndio utahitaji mtaalamu akusetie ama akuwekee software Ya Raid/Nas kuifanya hio computer yako kama Server ya mafile yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…