Trafiki ni halali kusimamisha gari kwenye kona?

KAKA NASOKI

Senior Member
May 25, 2016
191
212
Leo saa 5.42 asubuhi traffic wenye Pikipiki No. MC.......BXR wamesababisha msongamano na mvutano na abiria baada ya kusimamisha Daladala kwenye kona iliyoko kati ya barabara ya bandari na Devis Corner wakilazimisha gari hilo lirudi kituoni.

Kwanza kulikuwa na joto kali mno kina mama abiria wakaomba kwa kuwa wana watoto na mizigo tokea Kariakoo, basi dereva aruhusiwe washushwe Tandika kituoni gari lirudi wamelizane nao.

Jamaa waligoma kabisa ikabidi washuke sasa heka heka ilikuwa kwa kina mama wenye mizigo na watoto. Mabishano yao yalisababisha foleni na mvutano kiasi cha kuwavutia Askari wa tigo ambao walikuja lakini hakuna walilofanya.

Sasa swali dereva ukipaki kwenye kona kosa je wao kusimamisha daladala kwenye kona ni halali, wakati kulikuwa na eneo zuri la kuegesha hapo karibu?
 
Kuna nyakati madereva hufanya mambo ya kipuuzi kwa imani kuwa Abiria watamtetea.

Kingine ni kwamba Maaskari wetu wamefundishwa matumizi ya Nguvu bila akili.. Ndiyo maana yanapenda kutumia msemo Wa TII SHERIA BILA SHURUTI..

Kwa hiyo hapo ni pipa na mfuniko vilikutana, kero ikahamia kwa abiria..
 
Back
Top Bottom