Sijui mnakiona nikionacho?
Trafiki kusababisha ajali ni kosa ambalo kwa tabia za watz zilivyokuwa zamani hata yeye wangempa pole ya kusababisha ajali,lakini leo wamempiga,je,katika akili yako unadhani ni hii ajali tu iliyowafanya kufika mbali hivyo kimaamuzi?
Mie naona kufikia hatua ya wananchi kumpiga askari huyu na uniform yake haijatokana na ajali tu,bali tayari kuna kitu cha ziada akilini mwao kinachojijenga gradually kama reaction kutokana na mazingira wanayoishi hivi sasa kilichowaendesha kufanya hivyo na hicho kitu nakiogopa sana,hakina macho,kuna siku kitawapeleka kwenye kambi za jeshi na magogoni.
Kinajaa taratibu mioyoni mwao,angalia hata comments za wachangiaji wengi wa mjadala huu,utaona jambo jipya mioyoni mwa watz, na kama mnafikiri watz wanamalizia hasira zao mitandaoni tu,basi haya matukio ni ujumbe maridhawa,kwamba wanaweza kutekeleza wanachotamani,hizi ni dalili tu,binadamu ni yule yule Misri,Ulaya,Somalia,Syria and so Tanzania!na ipo siku atadhihirisha hilo duniani kote,endeleeni kuwaonea,stay tuned!