Naskia huyu mkuu wa jeshi wa sasa hawapendi traffic kabisa. Labda ndio maana raia wanawadharau.
Sio Mkuu wa Jeshi hilo peke yake anayewachukia trafiki bali ni watu wengi wenye kutumia barabara, naye akiwa mmoja wapo.
Kuna kero sana barabarani.Yani mtu akiwaona trafiki mbele yake anaona janga la kuchomoa hela zake.Yani ukisimamishw lazima hela itoke bila hata kosa.Ukiuliza kosa lako nini nini mbona unacheleweshwa basi inakuwa tabu kabisa.
Wakubwa wao wamefanya makusudi kuweka viwango vikubwa vya makusanyo kwa siku kwa kila trafiki ili wananchi wapige kelele na kitengo hiki cha kula rushwa rushwa kiondolewe kuepusha lawama zinazolichafua jeshi.
Nasikia kuna askari mmoja aliwahi kununua utrafiki kwa sh. 2,500,000/= kwa kukopa benki kabisa.Sasa sijui atazirudishaje.Wanawake wanaingia kwa rushwa ya ngono.
Hapo usitegemee mtu mwadilifu kama Mangu kukipenda kitengo cha namna hii.
Cha msingi ni kurudisha suala la barabara na matumizi yake kwenye wizara ya miundo mbinu yenye chuo cha usafirishaji.Polisi wabaki na misafara na road block kuzuia magendo.
Mwakyembe aunde chombo maalum kikichojaa wasomi wa vyuo mbalimbali hata kama atawachukua huko polisi lakini kisiwe na hulka za kijeshi na vitisho.
Mbona huko baharini na angani hawahusiki polisi kwenye kutoaadhabu zaidi ya kuimarisha ulinzi tu?