Trafiki afa baada ya kukamata daladala

Trafiki afa baada ya kukamata daladala

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani
mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo
kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa hospitali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini
alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana,
baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.
------------------------------------------------------------------
Moshi. Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.

Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa hospitali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana, baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.

Mmoja wa mashuhuda alisema "Baada ya kuikamata hiyo Hiace (Toyota) pale Kiborloni aliingia kwenye hiyo gari na kukaa kiti cha mbele pembeni ya dereva na kumwamuru kulipeleka kituoni.

"Wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni ghafla yule trafiki akawa haongei na akawa anamwegemea dereva… hiyo hali iliendelea hadi walipofika kituoni ndipo dereva akawaeleza trafiki wenzake." Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi.

Chanzo:MWananchi

makubwa hayoooo, wakome kupanda gazi zetu. wanatakiwa wawe na gari zao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.
 
Hata kama basi lina makosa yanayoonekana dhahiri?!
 
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.

Acha kuwajambisha askari kwa ushirikina. Wengine wanalindwa kwa damu ya Yesu
 
Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani
mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo
kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa hospitali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini
alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana,
baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.
------------------------------------------------------------------
Tusihukumu
 
Aise hayo mambo yapo kuna huyu jamaa wa makambako mwandulami naye noma..gari yake huwa haikamatwi na trafiki
 
tungepata na picha yake tungeweza pata jibu, kama ni wale matrafiki wanene wenye BP na presha ingeweza saidia, ila kikubwa alala kwa amani.
 
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.
Huo ni ukatili na ushetani kwa binadamu mwenzako anayetafuta maisha, mshauri kama yeye ni mlozi sana afanye hivi: Magari yake yote yawe hayawezi kuonekana kwene macho ya trafiki, as simple as that.
 
Watu tunatembea na magonjwa mengi..juzikati hapa nimepanda daladala dada mmja alikuwa kasimama yaani akaanguka gafla na kuzimia.aisee it shocked me
 
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.

Kuna trafiki alikamata gari la mzee kilenga, watu wakamshauri aliachie akawa mbishi, kuanzia siju hiyo akivaa nguo za trafiki anawashwa karibu ya kufa, akivaa za kawaida mzima.
Dada mmoja trafiki nae alikamata akatokwa na bleed mfululizo bila kukoma wakamshauri akamtafute mzee mwenyewe, akampelekea zawadi ya sukari mzee akamshika kichwa dada akapona, siku yapili akaacha kazi
 
Hilo gari lisachiwe, hwawezi kosa madudu humo..

Enzi zangu walikuwa hawaniwezi hao, tena sumbawanga..
 
Aikambeeee....... Shikamoni wachagga, kumbe na nyie kwa ndumba hamjambo??!!
 
sio kila kitu ni uchawi aisee... acha mawazo vimini
Ndio zetu hizo mkuu, watu wanaamini uchawi kuliko vyote ila mbele za watu utasikia "mie mambo ya ushirikina sipendi"lakini akiwa chocho au na hizi ID zetu anautukuza huyo
 
Back
Top Bottom