TRA yavuka lengo mapato ya Machi, imekusanya shilingi trilioni 1.31

Akili yako ya ajabu kwenye u aweka makadrio ambayo wenzako hawajaweka?
Inaweza onekana ya ajabu lakini ninakuambia ukweli bado TRA hawajabana mianya ya upotevu wa kodi kwa kiasi cha kutosha. Mfano mzuri ni huku nilipo, Watu wananunua vitu bila kudai risiti, si kwenye vituo vya mafuta, si kwenye maduka ya jumla na rejareja, si kwenye mahoteli na nyumba za kulala wageni, n.k. Ni lazima TRA waje na mikakati itakayowawezesha kubana kila eneo kikamilifu. Ninaamini wakifanikiwa katika hilo wanaweza fikisha hata zaidi ya Trilioni 2. Changamoto yangu kwao ipo palepale, wakaze buti maana bado hawajafanya ipasavyo.
 
Hongereni TRA kwa kazi inayoenda vizuri. Naomba kuwashauri. Hakikisheni kuwa wafanyabiashara wakubwa wanalipa kodi stahiki kwani bado ukwepaji upo mwingi. Kwa wafanyabiashara ndogo ndogo achaneni na kuhimiza mashine za efd zaidi hakikisheni wote wanalipa kodi kwa udogo wao mfano wote wapatiwe TIN na walipe kodi kulingana na biashara zao mfano magenge, saluni za kiume na kike, mama ntilie, viduka vidogo vya mitaani etc wote hawa wanaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye mapato ya serikali kama wakilipa japo 20,000 kwa mwaka. Watz wanapenda kulipa kodi tatizo ni utaratibu mbaya wa ukusanyaji uliwekwa na TRA wenye lengo la kuweka mazingira ya rushwa.
 
Hadi sasa makusanyo yanaashiria kuwa kuna billion 400 hadi 500 zilikuwa hazikusanyi awamu ya nne.
Wengine tulisema mabadiliko ndani ya ccm Yanawezana hasa baada ya jamaa tuliowaamini kubadili gia angani.
Yote kwa yote, madhumuni ni kuendeleza nchi bila kujali chama
Kweli mkuu Mi naona hapo kuna kama Trillion kabisa ilikuwa haikusanywi ndo mana tra wanaisogelea mdogo mdogo so kuna siku tutaambiwa wamekusanya Tri.. 2+
Daaah ila serikali ya Mkwere ilikuwa kiboko aseeeee

Viva Mh Magufuli
 
Afadhali sasa hivi hata nikikatwa kodi at least naimani hela yangu itafanya kazi inavyotakiwa tofauti na awamu iliyopita au angechukua huyu nywele nyeupe

Hii si kweli mkuu,tra wanazuga wananchi tu...ile ya mwezi wa kwanza ingechukuliwa kama benchmark,ambapo tunazidi kushuka sana....haya malengo binafsi ya kila mwezi ni uhuni mtupu...wangechukulia the highest ile ya january ndio utajua ukweli kua tunashuka kadri miezi inavyoenda
 
Hivi huwezi kufanya argument mpaka utukane hijo de puta wewe.
Kwanza hili jukwa sio level yako mbwa wewe. Wewe size yako ni post za akina Ali Kiba and the likes.
What do you know about politics? Huna upeo wa ku judge political affiliation ya mtu.
Mkuu huyo PUTA matola amekurupuka:Anamshambulia kila mtu Na mada husika hazijui.
 
Kampuni zinafungwa sana

Potelea mbali. Wanaofunga ni wale waliozoea njia mkato. Hao hata wakijaa nchi nzima hawana maana yeyote. Afadhali kuwa na biashara chache zinazofuata sharia. Sasa naanza kuamini watu wengi walikuwa wakifaidika na njia za mkato. Imekula kwenu sasa!
 
Ila serikali ya MAGU ianze kufikiria haraka namna ya kushusha kodi hasa, VAT. Ni bora kuwa na kodi ndogo na kupata watu wengi watoao kuliko kuwa na kodi kubwa na wakwepaji au biashara zinazokufa.
 
Wafuasi Ponda mna tabu sana, aliyekuzidi amekuzidi tu akili maarifa mpaka mali.
Sasa weye ma to la una akili gani?Au maarifa gani? Na mali?
Kwanza angalia maoni yako ktk Uzi Huu tu. Halafu jitathmini
1) akili
2) maarifa
3) Mali
4) sifuri
 
back to square 1.... upikaji wa takwimu.

this is always destined to catch up with someone. don't go away!
 
TAARIFA KWA UMMA

MAKUSANYO MWEZI MACHI 2016

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya na kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato mwezi Machi 2016 kwa asilimia 101. Lengo hilo limevukwa baada ya TRA kukusanya shilingi trilioni 1.31 kati ya lengo la shilingi trilioni 1.30.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata amesema ongezeko la makusanyo linatokana na jitihada zinazofanyawa na TRA katika kuongeza kasi ya usimamizi wa ufuatiliaji na ukadiriaji wa kodi kwa usahihi.
“Tumejitahidi kudhibiti biashara za magendo katika maeneo ya Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, mipakani na maziwa yote, Alisema Kamishna Mkuu.

Amesema hadi kufikia Machi 2016, tayari TRA imekusanya shilingi Trilioni 9.89 sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya shilingi trilioni 9.99 mwaka wa fedha 2015/2016. Bw. Alphayo amewasisitiza wafanyabiashara ambao hawajasajili biashara zao kufanya hivyo mara moja kupitia ofisi za TRA zilizoko katika maeneo ya biashara zao na kwa wale wanaoshiriki vitendo vya uingizaji bidhaa za magendo nchini amemewata kuacha mara moja kwani vinaipotezea serikali mapato. “Wakikamatwa katika msako unaoendelea watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutaifisha bidhaa hizo, kutozwa faini pamoja na kifungo”, amesisitiza.

Kwa Wafanyabiashara ambao wanastahili kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) Kamishna Mkuu amewataka kujisajili katika ofisi yoyote ya TRA na wahakikishe wanataarifa muhimu ikiwemo anuani inayotambulika na namba simu zinazofanya kazi. “Natoa wito kwa wafanyabiashara wote waliosajiliwa na VAT lakini hawatumii mashine za kielektroniki za kodi (EFDs) watumie mashine hizo kwa mujibu wa sheria. Wakibainika hawazitumii watachukuliwa hatua za kisheria kwani zoezi la ukaguzi wa biashara linaendelea mtaa kwa mtaa katika mikoa yote. Aidha wananchi wanakumbushwa kudai risiti za kodi kwa thamani halisi ya manunuzi kila wanapofanya manunuzi au kupata huduma”, alisema Kamishna Mkuu na kuongeza kuwa wananchi wema na wazalendo wenye taarifa za ukwepaji wa kodi wazifikishe TRA kwa usiri. TRA inawaahidi donge nono ikiwa ni pamoja na kutunza siri za taarifa hizo. Vilevile wanapoadaiwa rushwa au kutendewa isivyo wasisite kutoa taarifa mara moja.

Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao makuu

watupatie namba za simu za kuripoti wakwepa kodi kwa kila mkoa
 
Bandarini upitishaji wa mizigo umeshuka kwa 46%,haya tufungeni kamba hizo sarakasi zilizosababisha sky rocketing ya mapato ni zipi!?Vijana wa magufuli kwa kamba bana...
 
Mkuu naona bado unakomaa Na arrears!
Naona bado TRA wana ku-prove wrong!! Ukubali tu ukweli mkuu kwamba makusanyo halisi ya kodi yameongezeka, najua ulikuwa unategemea makusanyo yawe chini ya trillion 1 ili uweke uzi hapa wa arrears!!! Pole mkuu!!
Jamaa huyu na wenzake wa UKAWA wanatma kunywa sumu
 
Swala la uchumi wa Taifa wewe unaleta ushabiki wa siasa, wewe ni mpuuzi kama hulijuwi jina lako.

Nenda monchwari Muhimbili halafu unioneshe monchwari ya mashabiki maandazi wa ccm

Tanzania sasa ni ya Magufuli na siyo ccm, mtaisoma namba vizuri tu.

Wee bwana huwa unanivunja mbavu unavyowapashaga jamaa wanaolete mzaha katika maswala mazito hahahaaa!
 
Back
Top Bottom