Kati ya Wizara ya Fedha na TRA mmoja kadanganya mahesabu kwenye ripoti ya mapato 2022/23

Mawimba

Senior Member
Apr 29, 2013
155
156
Habarini waungwana!

Kama kichwa Cha mada kinavyojieleza.

Kipindi waziri wa fedha anaiwasilisha hotuba ya bajeti mwaka 2023/2024 katika kipengele 'IV. Tathimini ya utekelezaji wa bajeti ya serikari kwa mwaka 2022/23 alieleza serikali ilitaraji kukusanya trilion 41.48 kutoka vyanzo vya ndani na nje Hadi Aprili 2023 jumla ya shilingi Trilion 32.43 zilipatikana kutoka vyanzo hivyo.
Mchanganuo wa mapato yaliopatikana ni kama ifuatavyo

Mapato yaliopatikana kupitia mamlaka ya mapato Tanzania yalikuwa ni shilingi Trilion 18.81 ambapo lengo la mwaka ni shilingi Trilion 23.65.' Naiweka nukta hapa Tuje kwenye Ripoti iliotolewa na TRA TRA walitoa taarifa kwa umma.

Ripoti ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Julai 3, 2023 Ambapo mamlaka ya mapato iliutaarifu umma katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2022/23 mwezi Julai 2022 Hadi Juni 2023 mamlaka imefanikiwa kukusanya kiasi Cha shilingi Trilioni 24.11 sawa na ufanisi wa 97.1% katika lengo la kukusanya shilingi Trilioni 24.76.

Naiweka nukta Swali la kwanza TRA katika bajeti ya mwaka 2022 alipewa jukumu la kukusanya shilingi Trilioni 23.65 Nani alitoa jukumu kwa TRA la kukusanya Trilioni 24.76 kama mamlaka ilivyo tutaarifu kwenye taarifa yake kwa umma?

Swali la pili Wizara ya fedha kwenye Hotuba ya Bajeti 2023/2024 kwenye kipengele Cha tathimini ya Bajeti 2022/23 Wizara inasema TRA ilikusanya shilingi Trilioni 18.81 kuanzia Julai 2022 Hadi Aprili 2023. Wakati Ripoti ya TRA kwenye jedwali namba 1: makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Ukijumrisha makusanyo yote kutokea Julai 2022 Hadi Aprili 2023 unapata trilioni 20.00 Kuna nini hapa?

Nawasilisha

Screenshot_20230704-144200.jpg
Screenshot_20230704-154534.jpg
 
Mwanzo nilidhani labda wamechukua lengo LA mwaka LA 24.76 trillion wakagawanya kwa miezi 10 kupata lengo LA miezi 10,but bado hazi tally.
Ninavyoona ni makosa yamefanyika.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom