TRA yamkana Ngeleja, yasema kazi yake ni kukusanya kodi

Ngeleja lazima atapata kichaa kusikia haya
1: PCCB inasema kurudisha hela za escrow hakukuondolei mashtaka na kushtakiwa kuko pale pale

2: TRA inasema haihusiki na kuzipokea hela za escrow sbb kazi yao ni kukusanya kodi, hivyo Ngeleja kabaki mkiwa na case yake inakuja moto balaa yaani kheri angekaa kimya asubiri kusulubiwa tu, hizi hela za escrow zitawatokea sehemu yoyote iliyo wazi alafu Mkuu alisema hela ya serikali haipotei, ila mtu anaweza potea, sio hela za serikali..

Poleeeeeeniiiiiiiii mliokula hela za escrow zilikuwa tamuuuuuuuuuuu sasa zinageuka sumuuuuuuuuuuuuuu
 
Malipo hayo kayafanya chini ya Ushauri wa BASHITE mkuu.

sent from my BBC using JamiiForums mobile app
 
Payee: COMMISSIONER FOR DOMESTIC REVENUE
Account Number: 9921134701

Kayombo: hilo li-account ni la TRA?
 
Ujinga mtupu, hawazitambui wakati Ngeleja ana risiti ya kuzirudisha?! Ujinga sana unapo pokea hela ambayo hata supporting document yake haihusiani na shughuli za TRA, yaani ni ujinga ujinga ujina..
Ngeleja hajaonyesha acknowledgement receipt kutoka TRA hii inngempa mamlaka yakusema TRA wamepokea hela.
 
Naombeni msaada hapa sijaelewa maana inaonekana mgao ulikuwa Billion4.77 lakini ripoti ripoti ya uchunguzi wa kashfa Tegeta Escrow ilisema Sh. bilioni 306 zilichotwa kutoka Benki Kuu kinyume cha sheria, sasa hizo nyingine baada ya kutoa billion 4.77 zilienda wapi????
Walibaki nazo kina Ruge na Seth
 
Hivi Ngeleja amefikia mahali pa kutojua maana ya neno 'rejesha'?!!!! fedha apewe na Rugemalira, akae nazo ama azifanyie biashara kwa miaka kadhaa halafu awalipe TRA halafu aseme amezirejesha! hivi TRA ni Rugemalira?!
 
TRA imesema haizitambui shilingi milioni 40 zilizorejeshwa na Ngeleja na kwamba hawatahangaika nazo sababu kazi yao ni kukusanya kodi.

8d152328127effedcaabe6aa5c9f43be.jpg


Sent from my Diamond Crypto using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo hawakupokea hela
Sasa ngeleja alizipeleka wapi

Karatasi ya kulipia benki inaonyesha zililipwa kwenye Akaunti ya Commisioner for Domestic Revenue, ambayo ni ya TRA.

Huyo ofisa wa TRA angekubali tu kuwa zililipwa kwenye akaunti yao hata kama ni kwa makosa; kwamba wao hawahusiki na kupokea pesa za Escrow. Iliyopo ni wao wafanye utaratibu wa kuzihamishia huko kunakotakiwa.
 
Karatasi ya kulipia benki inaonyesha zililipwa kwenye Akaunti ya Commisioner for Domestic Revenue, ambayo ni ya TRA.

Huyo ofisa wa TRA angekubali tu kuwa zililipwa kwenye akaunti yao hata kama ni kwa makosa; kwamba wao hawahusiki na kupokea pesa za Escrow. Iliyopo ni wao wafanye utaratibu wa kuzihamishia huko kunakotakiwa.
No,
wao wazirudishe CRDB zilikotoka, huko unakosema wewe kua KUNAKOTAKIWA hakuko kihalali
 
Back
Top Bottom