JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,865
- 6,806
Kabla ya kusoma maoni yangu tazama hizi takwimu na maelezo ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari:
BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2023/24
Katika Mwaka wa Fedha 2023/24 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliidhinishiwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 212.4. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 30.5 ziliidhinishwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi bilioni 18.5 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi bilioni 11.9 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo. Aidha, Shilingi bilioni 181.9 iliidhinishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, ambapo Shilingi bilioni 146.8 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 35.2 ni fedha za nje.
katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara imepokea jumla ya Shilingi bilioni 213.9 sawa na asilimia 100.7 ya Shilingi bilioni 212.4 ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge katika Mwaka 2023/24. Kati ya zilizopokelewa Shilingi bilioni bilioni 16.3 ni kwa ajili ya Mishahara, Shilingi bilioni 7.0 ni Matumizi Mengineyo na Shilingi bilioni 190.6 ni fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Fedha za miradi ya maendeleo inajumuisha Shilingi bilioni 102.1 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 88.5 ni fedha za nje
BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2024/25
katika Mwaka wa Fedha 2024/25, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 180,926,557,000.00 kwa mchanganuo ufuatao:-
Nimekuwa muumini mzuri wa kufuatilia mijadala ya Bunge inayoendelea wakati huu hasa kuhusu masuala ya Bajeti.
Moja kati ya Wizara ambayo imenifanya nibaki na mshangao ni Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutokana na kiwango cha fedha ilichoomba kwa ajli ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Najua kuwa Wizara zote zinaingiliana na nyingine kimajukumu lakini Wizara hii inayoongozwa na Nape Nnauye inaingia katika Wizara na Idara zote Nchini kutokana na kuhusisha masuala ya Digitali au Teknolojia.
Dunia ya sasa kuanzia mawasiliano na njia za kutuma, kupokea au kuhifadhi fedha zote zinafanyika mtandaoni, kwa ufupi kila mwenye maendeleo anaelekea katika Uchumi wa Kidigitali (Digital Economy).
Uwekezaji mkubwa katika masuala ya Digitali ndio msingi mkubwa wa Tanzania kupiga maendeleo, kupunguza mianya ya rushwa, kuongeza uwajibikaji, kuboresha huduma na kurahisisha njia za mawasiliano.
Pamoja na hayo yote Wizara hii mwaka wa fedha unaomalizika sasa iliomba Shilingi bilioni 212.4 ikapewa Shilingi bilioni 213.9 sawa na asilimia 100.7 ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge katika Mwaka 2023/24.
Ajabu kuelekea mwaka ujao wa fedha Wizara hiyo imeomba pungufu ya fedha ambazo ilipata mwaka huu unaomalizika, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 180,926,557,000.00, kwa hali hii Serikali na Wizara kwa jumla inawekeza vipi kwenye Dunia ya Kidigitali kwa kupunguza bajeti kama hivi?
Hii sio sawa, Duniani wenzetu wengine wanaendelea kuwekeza kwenye teknolojia sisi ndio kwanza tunapunguza bajeti kisha tunataka maendeleo ya teknolojia.
Bajeti ya 2023/24
Bajeti ya 2024/25