issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,781
- 5,205
TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA
* Ni ya ukwepaji kodi kwa miaka 19
* Wajitetea kupoteza kumbukumbu
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha CHADEMA, ambacho kinadaiwa kukwepa kulipa kodi halali za serikali, kimeshindwa kutoa taarifa za mapato kwa kile kilichodaiwa kumbukumbu zimepotea.Badala yake, CHADEMA imetoa taarifa ya hesabu za mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, za kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, huku ikidaiwa kutolipa kodi tangu kuanzishwa kwake.Kutokana na hilo, CHADEMA iko katika hatari ya kudaiwa mamilioni ya shilingi na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), ambayo imeanza kufanya uchunguzi wa madai hayo.
Habari za kuaminika ndani ya TRA zimesema taarifa ya hesabu za chama hicho kwa mikoa hiyo zina utata na zinaonyesha ukwepaji kodi.
Katika utetezi wake kwa maofisa wa TRA, CHADEMA imedai haiwezi kukatwa kodi kwa kuwa inawalipa watendaji wake posho na si mishahara.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, maofisa wa TRA katika uchunguzi wamebaini fedha wanazolipwa watendaji wa chama hicho ni nyingi kuliko kima cha chini cha mshahara.
Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi, kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TRA.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini CHADEMA iliwasilisha taarifa ya fedha ambayo ina dosari. Watendaji ambao hawalipiwi kodi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, anayelipwa mshahara wa zaidi ya sh. milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.
Dk. Slaa alishawahi kuhadaa Watanzania kwa kupaza sauti akidai mshahara wa mbunge ni mkubwa hivyo upunguzwe.
Kuibuliwa ufisadi huo ndani ya CHADEMA kulimfanya Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa chama hicho, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando kukanusha kupitia vyombo vya habari wakidai ni uongo.
Komu alidai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi, wakati waraka ambao Uhuru inao unaonyesha mamilioni ya fedha yanayochotwa na mtendaji huyo.
Viwango hivyo ni mwendelezo wa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam na kuonyesha kuna tofauti kubwa na maelezo waliyotoa Komu na Marando.
Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.
Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa wastani wa lita 750 kwa
mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja.
Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.
Dk. Slaa anadaiwa kupata posho ya nyumba mara mbili, kwani ilipendekezwa alipwe sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, ambako anaishi kwa sasa.
Hata hivyo, licha ya kulipwa fedha hizo Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. milioni moja kila mwezi.
Sourc: Uhuru