TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,782
5,204
TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

* Ni ya ukwepaji kodi kwa miaka 19

* Wajitetea kupoteza kumbukumbu

Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha CHADEMA, ambacho kinadaiwa kukwepa kulipa kodi halali za serikali, kimeshindwa kutoa taarifa za mapato kwa kile kilichodaiwa kumbukumbu zimepotea.Badala yake, CHADEMA imetoa taarifa ya hesabu za mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, za kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, huku ikidaiwa kutolipa kodi tangu kuanzishwa kwake.Kutokana na hilo, CHADEMA iko katika hatari ya kudaiwa mamilioni ya shilingi na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), ambayo imeanza kufanya uchunguzi wa madai hayo.

Habari za kuaminika ndani ya TRA zimesema taarifa ya hesabu za chama hicho kwa mikoa hiyo zina utata na zinaonyesha ukwepaji kodi.

Katika utetezi wake kwa maofisa wa TRA, CHADEMA imedai haiwezi kukatwa kodi kwa kuwa inawalipa watendaji wake posho na si mishahara.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, maofisa wa TRA katika uchunguzi wamebaini fedha wanazolipwa watendaji wa chama hicho ni nyingi kuliko kima cha chini cha mshahara.

Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. “Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi,’’ kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TRA.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini CHADEMA iliwasilisha taarifa ya fedha ambayo ina dosari. Watendaji ambao hawalipiwi kodi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, anayelipwa mshahara wa zaidi ya sh. milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.

Dk. Slaa alishawahi kuhadaa Watanzania kwa kupaza sauti akidai mshahara wa mbunge ni mkubwa hivyo upunguzwe.

Kuibuliwa ufisadi huo ndani ya CHADEMA kulimfanya Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa chama hicho, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando kukanusha kupitia vyombo vya habari wakidai ni uongo.

Komu alidai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi, wakati waraka ambao Uhuru inao unaonyesha mamilioni ya fedha yanayochotwa na mtendaji huyo.

Viwango hivyo ni mwendelezo wa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam na kuonyesha kuna tofauti kubwa na maelezo waliyotoa Komu na Marando.

Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa wastani wa lita 750 kwa
mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja.

Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa anadaiwa kupata posho ya nyumba mara mbili, kwani ilipendekezwa alipwe sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, ambako anaishi kwa sasa.

Hata hivyo, licha ya kulipwa fedha hizo Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. milioni moja kila mwezi.


Sourc: Uhuru
 
Hii topic ilianzishwa asubuhi na ikajadiliwa vya kutosha. mod ifute inajaza sever
 
Maneno yote wanayo hubiri kumbe wanakwepa kulipa kodi!? Uzalendo uko wapi sasa wa Chama cha Denda na Magwanda!
 
Hii topic ilianzishwa asubuhi na ikajadiliwa vya kutosha. mod ifute inajaza sever
Suala si kuanzishwa asubuhi au usiku,, NO! Ni kukwepa kodi,
Hapa ndipo napata shida na viongozi wetu,, kelele nyiiiiiingi kwelikweli majukwaaani, kumbe wanatula kekundu tu,, hakuna CDM wala takataka gani sijui, wote walaji tu. Tunaibiana
 
TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

* Ni ya ukwepaji kodi kwa miaka 19
* Wajitetea kupoteza kumbukumbu
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha CHADEMA, ambacho kinadaiwa kukwepa kulipa kodi halali za serikali, kimeshindwa kutoa taarifa za mapato kwa kile kilichodaiwa kumbukumbu zimepotea.Badala yake, CHADEMA imetoa taarifa ya hesabu za mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, za kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, huku ikidaiwa kutolipa kodi tangu kuanzishwa kwake.Kutokana na hilo, CHADEMA iko katika hatari ya kudaiwa mamilioni ya shilingi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambayo imeanza kufanya uchunguzi wa madai hayo. Habari za kuaminika ndani ya TRA zimesema taarifa ya hesabu za chama hicho kwa mikoa hiyo zina utata na zinaonyesha ukwepaji kodi. Katika utetezi wake kwa maofisa wa TRA, CHADEMA imedai haiwezi kukatwa kodi kwa kuwa inawalipa watendaji wake posho na si mishahara. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, maofisa wa TRA katika uchunguzi wamebaini fedha wanazolipwa watendaji wa chama hicho ni nyingi kuliko kima cha chini cha mshahara. Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. "Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi,'' kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TRA. Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini CHADEMA iliwasilisha taarifa ya fedha ambayo ina dosari. Watendaji ambao hawalipiwi kodi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, anayelipwa mshahara wa zaidi ya sh. milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.
Dk. Slaa alishawahi kuhadaa Watanzania kwa kupaza sauti akidai mshahara wa mbunge ni mkubwa hivyo upunguzwe. Kuibuliwa ufisadi huo ndani ya CHADEMA kulimfanya Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa chama hicho, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando kukanusha kupitia vyombo vya habari wakidai ni uongo. Komu alidai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi, wakati waraka ambao Uhuru inao unaonyesha mamilioni ya fedha yanayochotwa na mtendaji huyo. Viwango hivyo ni mwendelezo wa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam na kuonyesha kuna tofauti kubwa na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa wastani wa lita 750 kwa
mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo. Dk. Slaa anadaiwa kupata posho ya nyumba mara mbili, kwani ilipendekezwa alipwe sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, ambako anaishi kwa sasa. Hata hivyo, licha ya kulipwa fedha hizo Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. milioni moja kila mwezi.


Sourc: Uhuru

Huyo source tu mwenyewe nimechoka! Badala ya kujivua gamba kwanza wanarukia yasiyowahusu
 
Lord have mercy!! This is scary,,,, Njaa mbaya jamani doh!
wanahubiri nini na wanachofanya ni nini? Huku ni kumwibia mtanzania kimachomacho kabisa. Ukwepaji wa kodi nchi za wenzetu ni kosa kubwa sana, ni uhuni na unahitaji kulaaniwa na kukemewa kwa nguvu zote. Hawa ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Hongera sana TRA, msirudi nyuma mpaka pesa za watanzania zilipwe.
Kinachokera zaidi ni kule kujifanya wana uchungu wa nchi kumbe ni yaleyale. Upuuzi mtupu.
 
Hii topic ilianzishwa asubuhi na ikajadiliwa vya kutosha. mod ifute inajaza sever
Hahahahahahaaaa,
Jamaa anaomba kocha amtupie taulo aokoke na makonde! usiweke mpira kwapani, wacha upigwe, unataka ubondia usiogope ngumi za usoni dada. Topic ifutwe kwanini, kujadiliwa vya kutosha maana yake nini? Kwanza zikifika posts ngapi ndiyo imetosha? Umehesabu zingine za JK na maaskofu, hazijatosha? Chundu wewe
 
Hii topic ilianzishwa asubuhi na ikajadiliwa vya kutosha. mod ifute inajaza sever
Unatia aibu mshkaji, yaani unaomba kabisa ifutwe? kisa? ni sawa na demu kumkimbia mwanaume kitandani! bwahahahahahahahahahahaaaa :smiling:
 
Maneno yote wanayo hubiri kumbe wanakwepa kulipa kodi!? Uzalendo uko wapi sasa wa Chama cha Denda na Magwanda!
chadema haiwezi kulipa kodi ili wakina lowassa na rostam wakachukue kwa ajila ya matumizi yao binafsi ingekua fedha za kodi zinarudi kwa watanzania ni sawa lakini kulipa kodi kwa mafisadi ni uhaini na TRA kama mnatumiwa na mafisadi kuidhoofisha cdm patachimbika
 
chadema haiwezi kulipa kodi ili wakina lowassa na rostam wakachukue kwa ajila ya matumizi yao binafsi ingekua fedha za kodi zinarudi kwa watanzania ni sawa lakini kulipa kodi kwa mafisadi ni uhaini na TRA kama mnatumiwa na mafisadi kuidhoofisha cdm patachimbika
wewe ndiyo umeishiwa sera kabisa, Huna dira wala mwelekeo. Imetajwa chadema wewe unakimbilia eti Lowassa. Mkwepe kodi nyie, msiulizwe, eti Lowasa, give me a break here! You need to take responsibilities for your own actions. TRA please do something, uhuni huu usivumiliwe hata kidogo. Patachimbika, patachimbika, what will you do? unamtisha nani? You need to pay.
 
Nyie mlio tumwa na Nepi itabidi mumpe na visogo vyenu avikune kune ili azidi kuwadanganya.
 
wewe ndiyo umeishiwa sera kabisa, Huna dira wala mwelekeo. Imetajwa chadema wewe unakimbilia eti Lowassa. Mkwepe kodi nyie, msiulizwe, eti Lowasa, give me a break here! You need to take responsibilities for your own actions. TRA please do something, uhuni huu usivumiliwe hata kidogo. Patachimbika, patachimbika, what will you do? unamtisha nani? You need to pay.

TRA inastahili kuomba radhi, siku zote walikuwa wapi kudai kodi. Kama Luoga anataka kupambana na CDM avue tai aingie rasmi katika siasa APATE MAPIGO. Hawa wameona suala la Mbowe limepotea kiana wameamua kutumia TRA
 
wewe una uchungu na nchi kweli? These are serious allegations wewe eti unaleta ushabiki! Ajabu sana vichwa maji wako wengi humu.
Serious allegations kwenye gazeti la magamba? Wake up and smell the roses.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom