TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

TRA wanatumiwa kisiasa na watu wa magamba kujaribu kuiokoa CCM inayotota matopeni! Nauliza: CCM inalipa kodi? maviwanja yote waliyopora kutoka kwa wananchi wanavilipia? Nasema hivi kwa sababu nimedokezewa kwa uhakika kabisa wahajawahi kuvilipia kodi ya viwanja na nyinginezo.

Usahahidi wa kwamba TRA (pamoja na vyombo vingine vya sewrikali kama polisi etc) vinaendeshwa kwa pua na wanasiasa wa magamba na siyo kutokana na uwezi na weledi wa wavyoviongoza. Suala hili lilianzia kutoka gazeti la magamba kwa kuwauliza TRA iwapo CDM wanalipa kodi. Halafu Nape Nauye akadakia jukwaani na hapo TRA ndio wakaingilia!
 
Serious allegations kwenye gazeti la magamba? Wake up and smell the roses.

Ngoja nikusaidie -- haya magamba ni very hard nuts toi crack. Serious allegations ni pale Mkuu wa kaya na genge lake RA na EL walipokula njama kuiba benki. Jumla zilizoibiwa ni over 130bn sh. The most single serious allegation involving theft in the country's history and one against the Head of State!
 
Una ushahidi wa hiyo sentensi nzito uliyokurupuka kuiandika hapo? If so, tupe huo ushahidi
 
TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

* Ni ya ukwepaji kodi kwa miaka 19

* Wajitetea kupoteza kumbukumbu

Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha CHADEMA, ambacho kinadaiwa kukwepa kulipa kodi halali za serikali, kimeshindwa kutoa taarifa za mapato kwa kile kilichodaiwa kumbukumbu zimepotea.Badala yake, CHADEMA imetoa taarifa ya hesabu za mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, za kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, huku ikidaiwa kutolipa kodi tangu kuanzishwa kwake.Kutokana na hilo, CHADEMA iko katika hatari ya kudaiwa mamilioni ya shilingi na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), ambayo imeanza kufanya uchunguzi wa madai hayo.

Habari za kuaminika ndani ya TRA zimesema taarifa ya hesabu za chama hicho kwa mikoa hiyo zina utata na zinaonyesha ukwepaji kodi.

Katika utetezi wake kwa maofisa wa TRA, CHADEMA imedai haiwezi kukatwa kodi kwa kuwa inawalipa watendaji wake posho na si mishahara.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, maofisa wa TRA katika uchunguzi wamebaini fedha wanazolipwa watendaji wa chama hicho ni nyingi kuliko kima cha chini cha mshahara.

Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi, kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TRA.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini CHADEMA iliwasilisha taarifa ya fedha ambayo ina dosari. Watendaji ambao hawalipiwi kodi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, anayelipwa mshahara wa zaidi ya sh. milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.

Dk. Slaa alishawahi kuhadaa Watanzania kwa kupaza sauti akidai mshahara wa mbunge ni mkubwa hivyo upunguzwe.

Kuibuliwa ufisadi huo ndani ya CHADEMA kulimfanya Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa chama hicho, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando kukanusha kupitia vyombo vya habari wakidai ni uongo.

Komu alidai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi, wakati waraka ambao Uhuru inao unaonyesha mamilioni ya fedha yanayochotwa na mtendaji huyo.

Viwango hivyo ni mwendelezo wa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam na kuonyesha kuna tofauti kubwa na maelezo waliyotoa Komu na Marando.

Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa wastani wa lita 750 kwa
mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja.

Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa anadaiwa kupata posho ya nyumba mara mbili, kwani ilipendekezwa alipwe sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, ambako anaishi kwa sasa.

Hata hivyo, licha ya kulipwa fedha hizo Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. milioni moja kila mwezi.

Sourc: Uhuru
Kwa uhuru hapa ndo limesomeka. Vinginevyo ni kwa ajili ya vichwa habari kusomwa kwenye redio na tv basi.Hapa JF nani amewahi kulinunua siku za karibuni?
 
WAkuu, hii ni duplicate, ipo mahali pengine-na slaa mwenyewe ameshaitolea majibu!
MAGAMBA WANARUKA NA KUKANYAGANA!:majani7:
 
mahali gani pengine? wacha kukurupuka wewe, wacha watu wachangie hoja

Ushauri kwa members ambao wamejiunga hivi karibuni, huu ukumbi ni wa Great thinkers kwahiyo kabla hujapost kitu chochote ni bora kupitia thread zilizopita toka zamani, hii kitu ilishajadiliwa hapa muda sana,na hata huo ushaidi unaohitaji wa JK, EL na RA kukwapua 130 billions ulishaletwa hapa kitambo sana, ushauri kwa nyie newa member ni kwamba mjifunze kupenda kusoma na kufikiri kabla ya kuongea.
 
Kwa hiyo na sisi tusiamini habari kama source yake ni Tanzania Daima au Mwanahalisi??
 
Nikitembelea huku huwa siku yangu inaharibika kwa hasira!!!!
 
Lord have mercy!! This is scary,,,, Njaa mbaya jamani doh!
wanahubiri nini na wanachofanya ni nini? Huku ni kumwibia mtanzania kimachomacho kabisa. Ukwepaji wa kodi nchi za wenzetu ni kosa kubwa sana, ni uhuni na unahitaji kulaaniwa na kukemewa kwa nguvu zote. Hawa ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Hongera sana TRA, msirudi nyuma mpaka pesa za watanzania zilipwe.
Kinachokera zaidi ni kule kujifanya wana uchungu wa nchi kumbe ni yaleyale. Upuuzi mtupu.

Kijana wa Nape karibu jamvini. Hebu twambie kwanza CCM pamoja na kupora vitega uchumi vyote vilivyokuwa vinamilikiwa enzi za chama kimoja wanalipa kodi kiasi gani serikalini? Je Makamba alikuwa analipa kodi kiasi gani kutoka kwenye mshahara wake?

Acha kudandia treni kwa mbele itakumaliza!!! Hii njaa inawasumbua ndio maana mnakuja hapa kwa wingi kutetea upupu.

Suala la kulipa kodi ni halina tatizo lakini hao TRA watwambie na kutuonyesha kwanza hesabu za CCM na kodi inayolipwa kabla ya kuidandia Chadema.

Anyway we need to ignore this as long as source yenyewe ni gazeti mfu la Uhuru.

Tiba
 
TRA wanatumiwa kisiasa na watu wa magamba kujaribu kuiokoa CCM inayotota matopeni! Nauliza: CCM inalipa kodi? maviwanja yote waliyopora kutoka kwa wananchi wanavilipia? Nasema hivi kwa sababu nimedokezewa kwa uhakika kabisa wahajawahi kuvilipia kodi ya viwanja na nyinginezo.

Usahahidi wa kwamba TRA (pamoja na vyombo vingine vya sewrikali kama polisi etc) vinaendeshwa kwa pua na wanasiasa wa magamba na siyo kutokana na uwezi na weledi wa wavyoviongoza. Suala hili lilianzia kutoka gazeti la magamba kwa kuwauliza TRA iwapo CDM wanalipa kodi. Halafu Nape Nauye akadakia jukwaani na hapo TRA ndio wakaingilia!

Mbona kila kitu mmeshakifanya siasa nyie wenyewe. Hebu tupe mstari uliogawa siasa na ukusanyaji wa kodi???
 
Kijana wa Nape karibu jamvini. Hebu twambie kwanza CCM pamoja na kupora vitega uchumi vyote vilivyokuwa vinamilikiwa enzi za chama kimoja wanalipa kodi kiasi gani serikalini? Je Makamba alikuwa analipa kodi kiasi gani kutoka kwenye mshahara wake?

Acha kudandia treni kwa mbele itakumaliza!!! Hii njaa inawasumbua ndio maana mnakuja hapa kwa wingi kutetea upupu.

Suala la kulipa kodi ni halina tatizo lakini hao TRA watwambie na kutuonyesha kwanza hesabu za CCM na kodi inayolipwa kabla ya kuidandia Chadema.

Anyway we need to ignore this as long as source yenyewe ni gazeti mfu la Uhuru.

Tiba

Kila jambo hufanywa kwa utaratibu na hao magamba kama walikuwa wakifanya hivyo watashughulikiwa. Kwa sasa na tuzungumze hili la CHADEMA. Baadae tutakuja kwa magamba baadae wake zake wawili CUF na NCCR na kufuatiwa wachovu wengine.
 
Ushauri kwa members ambao wamejiunga hivi karibuni, huu ukumbi ni wa Great thinkers kwahiyo kabla hujapost kitu chochote ni bora kupitia thread zilizopita toka zamani, hii kitu ilishajadiliwa hapa muda sana,na hata huo ushaidi unaohitaji wa JK, EL na RA kukwapua 130 billions ulishaletwa hapa kitambo sana, ushauri kwa nyie newa member ni kwamba mjifunze kupenda kusoma na kufikiri kabla ya kuongea.

Mwenzangu habari daima haifi na ndio maana kuna kitu kumbukumbu. Kuna sababu nyingi za kufanya topic kujirejea. Hivyo unafikiri kila mtu akijiunga atakuwa na wakati wa kuangalia ya nyuma kujua hiki kimeshapita au la? Hata hivyo kuna suwala la kubadilika mazingira ya jambo hilohilo, pengine kuna ushahidi mwengine. Namna watu watakavyochambua mada ndio itakayoamuwa muendelezo wa topic,hivyo usiwe na wasiwasi ukiona kitu kinakukera basi nyamaza kwani kwa kuchangia ndio unakiendeleza. Wache watu wawe huru usiwaamulie!!
 
wewe ndiyo umeishiwa sera kabisa, Huna dira wala mwelekeo. Imetajwa chadema wewe unakimbilia eti Lowassa. Mkwepe kodi nyie, msiulizwe, eti Lowasa, give me a break here! You need to take responsibilities for your own actions. TRA please do something, uhuni huu usivumiliwe hata kidogo. Patachimbika, patachimbika, what will you do? unamtisha nani? You need to pay.

We can do something,:majani7: hutishwi ila habari ndo hiyoooooo.:majani7:
 
Back
Top Bottom