Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,178
- 29,886
- Thread starter
-
- #221
Mkuu asante kwa ushauri.TAX BURDEN PRINCIPLE (KANUNI YA MIZANIA/MZIGO WA KODI)
Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wachangiaji wa huu uzi ni kuwa ufahamu wa kodi ni tatizo kubwa kuliko kodi yenyewe. The problem is not "tax" but "understanding of tax".
Jambo muhimu kwa kila mfanyabiashara si tu kujua aina za kodi bali kujua MIZANIA YA KODI (TAX BURDEN) ktk aina hizo za kodi.
Laiti wafanyabiashara weng wangejua kanuni (principle) hii ya TAX BURDEN watafahamu kuwa kodi nyingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji (Witholding tax agent) na watoa taarifa ktk mamlaka husika (file returns).
TAX BURDEN ni kanuni inayoonyesha ni nani haswa (Halisi) anawajibika kuilipia kodi fulani. Kwa dhana hii kuna tofauti kati ya mkusanyaji kodi na mlipaji wa kodi. Unaweza kuwa mkusanyaji kodi fulani lakini si wewe mlipaji wa kodi husika. Na hapa ndio wafanyabiashara wengi wameshindwa kuelewa kanuni hii na kuhisi wanaonewa au kulipa kodi kupita kiasi. Si sahihi
Kwanza, Mfano ni kodi ktk mishahara ya wafanyakazi inayoitwa PAYE anayelipa(kukatwa) ni mfanyakazi husika ila mwajiri anaiwakilisha tu ofisi za mapato
Pili, Kodi ya zuio (Withholding tax) ktk kodi ya pango (rent) na huduma (outsourced services) anayelipa/kukatwa ni Land Lord au anayepokea pango na sio mfanyabiashara anayelipa pango. Jukumu la mfanyabiashara ni kuikata na kuipeleka ofisi ya mamlaka.
Vivyo hivo ktk kodi ya ongezeko la thamani (Value added tax - VAT) pamoja na Capital gain tax ni kodi ambazo wafanyabiashara hawalipi wao direct ila wanakusanya kwa watu wengine na kuikabidhi kwa mamlaka husika.
Changamoto inakuja pale ambapo aliyepewa jukumu la kukusanya kodi kisheria hafanyi jukumu lake (failure to collect and remit tax to authority), hapo ndipo TAX BURDEN huhama kutoka kwa MLIPAJI halisi wa kodi husika kwenda kwa MKUSANYAJI., na wafanyabiashara wengi huishia kuumia kwa kubeba msalaba usio wao.
Kutokana na principle hii ya TAX BURDEN tayari tunaona kodi nyingi kimsingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji tu (Collect and file returns). Ukielewa principle hii kama mfanyabiashara utafanikiwa sana katika biashara yako na utapunguza Tax liabilities zisizo na ulazima.
ITAENDELEA..
😂TRA watausoma watatafuta namna ya kupenyeza kodi
Wewe ndiyo umejificha kwenye kicha cha ajabu ajabu hujui kuwa baadhi ya maofisa wa TRA huwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kwa makusudi kutengeneza mazingira ya Rushwa, umejitoa fahamu zote na kuwaona maofisa wa TRA ni mungu na malaika hawakosei wapo sahihi kwa kila jamboNdio elimu hii , na mnakubali kabisa kufundishwa huu ujinga
1. Kama mfanyabiashara sii mlipa kodi, kwann watu wa kodi wanamfuata, kwann wasimfute mhusika moja kwa moja?
2. Kama yeye si mlipa kodi, kwann kodi hizo zinaondoka hadi na mtaji wake na kuua biashara na kumwacha na madeni?
3. Kama yeye sii mlipa kodi hiyo, kwann hiyo pesa ikiondoka anai feel kwenye mzunguko wake wa pesa kwamba kuna kitu kimepungua??
Acheni kujificha kwenye vichaka vya ajabu ajabu, wekeni mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi, kateni kodi za halali sehem halali
TRA yafaa ifumuliwe isukwe upya na wale maofisa vinara wa kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kuwafungia account kuwafungia biashara watu wachunguzwe na Takukuru juu ya uhalali wa mali zao binafsiMkuu asante kwa ushauri.
Lakini nafikiri unajua fika kuwa kodi kama With Holding Tax na Provisional Tax huwa ni sehemu tu ya Annual Corprate Tax.
Na unajua madudu ambayo yanafanyika katika hili.
Kodi hizi zinakatwa (hasa WHT) kupita na kuzidi makadirio ya Corporate Tax,
Na ikishakatwa hairudishwi.
Nataka neno lako katika hili.
Halafu kwenye Invoicing.
Wafanyabiashara wengi hawalipwi in time, lakini wanapaswa kuwasilisha VAT at source and in time.
Yaani ukimpelekea Invoice na risiti ya EFD mteja wako(mara nyingi Serikali) unatakiwa ulipe a kodi uliyotakiwa kukusanywa ndani ya mwezi mmoja.
Uzoefu unaonyesha kuwa kuna wafanyabiashara hawalipwi hata ndani ya mwaka hivyo kufilisi kampuni.
Haya mambo ya vitabuni wee yaache tu, uhalisia na TRA ni kitu kingine.
Wafanyabiashara wakubwa wamehamishia pesa zao Nchi Jiran kukwepa A/C zao kufungwa na TRA kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetaniNdani ya miaka 3 nchi itakua hoi sana
Nimesoma andiko lake nikabaki kushangaa naona analeta elimu ya darasani ambayo ni tofauti kabisa na uhalisia..Mwambie afungue biashara yake afu a apply hizo theory zake tuone atafika wapi...wasomi wetu ni shida sanaNdio elimu hii , na mnakubali kabisa kufundishwa huu ujinga
1. Kama mfanyabiashara sii mlipa kodi, kwann watu wa kodi wanamfuata, kwann wasimfute mhusika moja kwa moja?
2. Kama yeye si mlipa kodi, kwann kodi hizo zinaondoka hadi na mtaji wake na kuua biashara na kumwacha na madeni?
3. Kama yeye sii mlipa kodi hiyo, kwann hiyo pesa ikiondoka anai feel kwenye mzunguko wake wa pesa kwamba kuna kitu kimepungua??
Acheni kujificha kwenye vichaka vya ajabu ajabu, wekeni mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi, kateni kodi za halali sehem halali
Ha ha ha hao wasomi watetea uonevu uovu Rushwa za baadhi ya maofisa wa TRA ni bora wangesalia na Elimu ya darasa la pili kuliko wakajiita wasomi huku wakitetea mateso manyanyaso uonevu kwa wafanyabiashara, hakunaga msomi wa hivyoNimesoma andiko lake nikabaki kushangaa naona analeta elimu ya darasani ambayo ni tofauti kabisa na uhalisia..Mwambie afungue biashara yake afu a apply hizo theory zake tuone atafika wapi...wasomi wetu ni shida sana
Wafanyabiashara wengi sasa wanabuni mbinu za kuhifadhi pesa zao Nchi zingine ama hata kuficha ndani mwao, hawana imani na Bank tena, na hii ni hatari kubwa kwa usitawi wa mabenk na mifumo ya mikopo ni vigumu Tanzania kupiga hatua kimaendeleo kwa kuendelea kuwalinda baadhi ya maofisa wa TRA vinara wa kuwabambikia kodi kubwa, kuwafungia Account, kuwafungia biashara wafanyabiashara wengi.Ndio maana hata mabenki sasa hivi wanashindwa kutoaa mikopo sasbabu hamna. Mfanyabiashara mjiinga ataacha pesa yake benki huku akijua kwamba T.R.A wanamnyemelea.kwahio mwisho wa siku ni Tanzania inaingia kwenye great depression.
Hajakataa kulipa Kodi lakini iendane na uhalisia wa biashara mkuulipa kodi mzee
TRA ifumuliwe isukwe upya imejaa wala Rushwa mno akina masamaki wapo wengi sana, Takukuru iwachunguze maofisa wa TRA wale vinara wa kufunga biashara na Account za watu kwa njia haramu za kishetaniNi wakati Sasa na sisi Tanzania tuwe na Bodi ya Rufaa za Kodi yenye kujielewa
Wametajirika kwa RushwaHawa jamaa siku sio nyingi watatunyonya damu kabisa maana pesa watamaliza zote.
Umeandika nn hapa? Mada inahusiana na nn? Unapinga au unakubali? Unapinga nn unakubali nn?Wewe ndiyo umejificha kwenye kicha cha ajabu ajabu hujui kuwa baadhi ya maofisa wa TRA huwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kwa makusudi kutengeneza mazingira ya Rushwa, umejitoa fahamu zote na kuwaona maofisa wa TRA ni mungu na malaika hawakosei wapo sahihi kwa kila jambo
Ni vigumu kunielewa kwa sababu wewe ni mnufaika wa Rushwa na uonevu wote wa baadhi ya maofisa wa TRAUmeandika nn hapa? Mada inahusiana na nn? Unapinga au unakubali? Unapinga nn unakubali nn?
Comment yako ni kama polo haieleweka inasimama wapi, unapinga nn inaafiki nn
Ni vigumu kunielewa kwa sababu wewe ni mnufaika wa Rushwa na uonevu wote wa baadhi ya maofisa wa TRA
Nilimwona Lissu kwenye kampeni zake akipita kariakoo, mkamwambia mambo yako poa kabisa.Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.
TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.
TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.
Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.
Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.
UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.
Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.
Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.
Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba
Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.
Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.
Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.
Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.
Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.
USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.