TRA wahusike pia kugawa mapato.

TRA wahusike pia kugawa mapato.

Doria Mtandaoni

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
326
Reaction score
677
Naprndekeza itungwe sheria ya kuipa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kufanya distribution ya mapato kwenda wizara/taasis husika.

Hasa kipindi ambacho tunakaribia kujitegemea kwa asilimi 100.

Mara baada ya bajeti ya serikali kusomwa na kupitishwa, kuwe na kitengo maalum cha kuhakikisha makusanyo yanayopatikana yanagawanywa kadiri ya mipango ya bajeti.

HIli linamanufaa kuendelea kujenga imani ya walipa kodi kwa mamlaka ya mapato.

TRA kuwa na ufahamu mzuri na kuongezeka uwajibikaji katika kukusanya ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.

Walau wanasiasa na watendaji wengine kuanza kuwawajibisha na kuacha visingizio vya fedha kutokufika.
TRA Tanzania
 
kwanza kabisa labda nikusaidie TRA wamepewa jukumu la kukusanya tu. Na fedha hizi zinakwenda moja kwa moja kwenye mfuko au akaunti zilizopo Benki Kuu ya Tanzania.Hilo ndilo jukumu lao kuhakikisha kodi inakusanywa kwa mujibu wa sheria zilizopo na kufikisha benki kuu. Bunge kazi yake kubwa ni kuisimamia serikali na kuishauri ikiwepo na kupitisha sheria mbalimbali na bajeti ya matumizi. Wizara ya fedha wao wamepewa jukumu la kuisimamia TRA katika kuhakikisha inafanya kazi iliyopewa na serikali lakini pia kusimamia matumizi ya pesa yaliyopitishwa na bunge. Ndiyo maana katibu mkuu wa wizara ya fedha anaitwa mlipaji mkuu.Gavana wa Benki Kuu anawajibika kutunza fedha na kusubiri maelekezo ya serikali kwa mtiririko wa makubaliono yaliyopitishwa bungeni.Ndiyo maana kuna msimamizi wa Matumizi ya Serikali na mkaguzi mkuu.Sasa ukisema tena TRA wawe wanakusanya na kusimamia matumizi utakuwa ni sawa na kusema polisi wakamate wao na kuhukumu wao.Ni jambo gumu na usimamizi wake ni mgumu sana.
 
Mkuu asante kwa mchango. Kimsingi sio kusimamia matumizi tu.

Huyo mlipaji mkuu ni kama ameshindwa, fedha haziendi ama zisifike kabisa.
TRA wao wapewe zile kasma, na wawe wanapeleka fedha. Hao wengine waendelee na majukumu ya kusimamia matumiz ya hizo fedha.
 
Nimekuelewa Ndg kwamba kwa kiasi tra wameaminika zaidi na unashauri kwa kuaminika huku wapewe jukumu hili.
 
Back
Top Bottom