TRA: Ufafanuzi kwa umma kuhusu kodi ya pango

TRA: Ufafanuzi kwa umma kuhusu kodi ya pango

Huyu mama kabariki haya yanayoendele???
Mkuu mwanamke hakuumbwa aongoze aliumbwa kuongozwa.!

Unavyoona mambo yanaenda mrama ujue huo siyo utashi wa taasisi ya urais (KIONGOZI MKUU WA NCHI) bali ni utashi wa watu aliowapa dhamana yeye kiongozi mkuu (kwa sababu kwa udhaifu wake aliona hawezi) akiamini kwa akili zao watamsadia kumbe nao akili zao kisoda.

Angekuwa Raisi mwanaume huu ujinga usingeuona.
 
Haya makodi yanakuja kujaje??

Yaani watu wanajiulia tu au wananchi wanashirikishwa??

Nini maana ya kuwa na Bunge kama jambo linafanyika na mwananchi ambaye limgusa moja kwa moja hashirikishwi?

Hata wakidai wanashirikishwa maoni yao yanazingatiwa au wanafanya hivyo tu kwa kutimiza wajibu.
 
Hii nchi nikipata nikikamilisha process zangu za kwenda ughaibuni sirudi milele yani wametufanya kama maiti vile wanatupeleka wanavyotaka
 
TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU KODI YA PANGO

Dar Es Salaam, 25 Agosti, 2022:
Mamlaka ya mapato ya Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi kuwa Kodi ya pango hulipwa kama Kodi ya zuio inayotokana na mapato ya pango la nyumba Kwa asilimia 10

Tunaenda kuwahamisha watanzania kuwa Kodi hii si mpya bali wigo umeongezwa Ili wapangishaji wa nyumba binafsi wenye pato linaloanzia shilingi 500,000/= Kwa mwaka na kuendelea wamejumuishwa kwenye wigo wa Kodi kuanzia Julai mosi 2022.

Mwenye nyumba atapata cheti Cha Kodi ya zuio kama ushahidi wa malipo ya Kodi iliyolipwa kutokana na zuio la asilimia 10

Kwa maelekezo zaidi wasiliana nasi Kwa namba za bure;
0800-750075 au 0800-780078 au Whatsapp namba 0744-233333

"Pamoja tunajenga Taifa letu"

Imetolewa na;

IDARA YA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
View attachment 2335063
Na ile tunayolipia kupitia manunuzi ya LUKU kila mwezi ni nini?
 
Kodi ilikuwepo tokea kitambo na baadhi ya watu waliyofanya uwekezaji
Kwenye maeneo yao wamekuwa wakilipa
Sahivi inabidi TRA itoe elimu za kodi zote ambazo zinatakiwa kulipiwa
Ili raia wawe wanazijua na wakiambiwa wazilipe wasishtuke
Raia wengi bado elimu ya kodi hawaijui vizuri

Ova
Sio kwamba ilikua ina lipwa na mwenye nyumba.?. Kodi ya Pango na sasaiv wame Jumuisha ilipwe na Kila Mmoja alie pangisha.!?!..

Hii itaweza kusanya Nying kuliko ile ya Mwenye nyumba kulipia kule 10% koz angeweza kulipo 100K ata kama ilitakiwa kua 200K kwamaana anaweza sema nina watu 2 kumbe ana wapangaj 5[emoji23].. hapa serikali imelenga kupiga ndefu zaidi. Wapangaj ita walamba hii atari asa wa vyumba vya Self maana lazan wenye nyumba wapandishe kodi.

Kwa msaada labda watoe ukomo wa Kodi ya Vyumba.. yaan chumba Bei Gani kulingana na hili.
 
Nyumba nijenge kwa gharama zangu! Halafu mapato tugawane, huku ukiwa hujachangia chochote!

Yaani nitahakikisha hiyo kodi hainiathiri kwa namna yoyote ile. Na mpangaji akileta za kuleta, nampandishia tu kodi ya pango. Hataki aondoke, ampishe mwenye uwezo wa kulipa hiyo kodi.
Ndio kilichobak....
 
Kuanzia kiwanja kodi, nyumba uliyojenga mwenyewe kodi, umeme wa nyumba kodi, maji ya nyumba kodi etc..... lakini hata title ya nyumba lazima utoe rushwa na ukipata barabara ya tope shukuru mungu
 
TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU KODI YA PANGO

Dar Es Salaam, 25 Agosti, 2022:
Mamlaka ya mapato ya Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi kuwa Kodi ya pango hulipwa kama Kodi ya zuio inayotokana na mapato ya pango la nyumba Kwa asilimia 10

Tunaenda kuwahamisha watanzania kuwa Kodi hii si mpya bali wigo umeongezwa Ili wapangishaji wa nyumba binafsi wenye pato linaloanzia shilingi 500,000/= Kwa mwaka na kuendelea wamejumuishwa kwenye wigo wa Kodi kuanzia Julai mosi 2022.

Mwenye nyumba atapata cheti Cha Kodi ya zuio kama ushahidi wa malipo ya Kodi iliyolipwa kutokana na zuio la asilimia 10

Kwa maelekezo zaidi wasiliana nasi Kwa namba za bure;
0800-750075 au 0800-780078 au Whatsapp namba 0744-233333

"Pamoja tunajenga Taifa letu"

Imetolewa na;

IDARA YA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
View attachment 2335063
Tatizo la kodi hii ni kwanini alipe mpangaji kwa kigezo kuwa mwisho wa mwaka amdai mwenye nyumba? Endapo mwenye nyumba atakataa kuzirejesha kwa mpangaji itakuwaje? TRA ondoeni mzigo huu kwa wapangaji.
 
Bado zoezi la sensa ya majengo ambapo kutakuwa na kutatambua nyumba za biashara na thamani ya nyumba wamewahi sana kugusia hili jambo hivyo wanaweza kuathili zoezi la sensa hasa kwenye majengo
 
TRA wanaelemewa
TRA wanakurupuka
TRA hawana mikakati

Sipingi hiyo kodi kutozwa ila najua fika hawawezi kuratibu hilo zoezi.

Ushauri wangu ni huu.
Zoezi liachiwe shirika la nyumba.

Biashara ya kupangisha irasimishwe

Kuwe na leseni kwa ajili ya hii biashara mtu asipangishe kama hana leseni husika.

Kodi iwe 5% na sio 10%

Sidhani kama kuna mtu atakataa kulipia.

Ila kwa niwajuavyo tiharaei hili zoezi wataishia kulamba lamba sehemu chache.

Watu hawana vision, wapo kuunga juhudi na kungoja mishahara.

Wenye sifa, wenye uwezo, wenye maono ya kuongoza hizi taasisi hawapewi nafasi.
Mjomba fuko!
Kamata 5 zangu. Na unaona wametoa namba za simu Ina maana tunafanya majadiliano? Hakuna utaratibu mzuri wa kuwasaidia wananchi na Kwa Nini asilimia 10??

Hizo anwani za makazilizoanzisha mbona hatuoni zoezi likikamilika? Alianza nalo Paul Daud Bashite (Kolomije) hadi Leo Bado! Kweli tunashangaza. Ninyi endeleeni kumega kweli ya Taifa mkigawa SIFA Kwa aliye juu!! Yetu masikio!
 
hutapata mtu wewe au unafikir mwenye nyumba ni wewe tu litabak pagale mpaka utaman kumrudisha uliyempandishia kodi akahama.
Hii kodi itawaumiza wapangaji. Wewe bisha tu. Imagine jengo lipo barabani, litakosaje sasa wapangaji!!
 
Aà
Tatizo kubwa la hii kodi inawaumiza wapangaji,wenye nyumba wengi hawakubali kabisa kulipa,yeye anataka kodi yake iliyokamilika,na mpangaji hasa wa vyumba vya biashara anapoenda kufanyiwa makadirio ya biashara yake tra wanamkomalia na hii kodi na huku mwenye nyumba hataki kuilipa,ukimlazimisha sana anakupa notice uhame hivyo mpangaji anajikuta mzigo unakua mkubwa na ili kupunguza maumivu kama kodi ni laki tano kwa mwezi anasema laki mbili.

Tra tafuteni namna ya kuwabana wenye nyumba direct.
TRA ongezeni Tena ifike 20% watanzania wavivu sana
 
Back
Top Bottom