TRA si wanakusanya kodi kwa mujibu wa sheria na nyingine kwa matamko kama vitambulisho vya Magufuli, kosa lao nini?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hizi kodi anazozipiga vijembe sio ndio huyuhuyu alisema anakusanya kuliko waliomtangulia tena wananchi wakaitwa wanaolalamika kuwa wapiga dili si ni huyu huyu rais?

Sio huyu aliyesema lazima kodi zilipwe hadi tra wakawa wanatembea na bunduki na askari polisi na waziri mkuu akawatetea bungeni?

Sio huyu baba aliyeanzisha kodi za machinga kwa tamko?

Na sheria si wao ndio wanatunga na kupeleka miswada bungeni na huyu baba si ndio anasaini inakuwa sheria?

Kuna kodi inayokusanywa ambayo haipo kwenye sheria? Kwanini walaumie watendaji wanaofuata sheria badala ya watunga sheria?
 
Kinacho lalamikiwa ni baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kinyume na taratibu, ili kutengeneza mwanya wa wao kujipatia kipato kutoka kwa wafanyabiashara.
 
Kama ni watumishi basi sheria ina mapungufu inatoa mwanya kwa watendaji kwa hiyo tunarudi kule kule tatizo ni Watunga sheria
 
Kinacho lalamikiwa ni baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kinyume na taratibu, ili kutengeneza mwanya wa wao kujipatia kipato kutoka kwa wafanyabiashara.
Wewe ndio umebeba vyema. Thread closed.
 
Zile report za ukusanyaji Kodi uliotukuka uko wapi?
Wenye akili tulisema zile zilikuwa drama za magufuli ili awapumbaze akili malofa
 
Kinacho lalamikiwa ni baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kinyume na taratibu, ili kutengeneza mwanya wa wao kujipatia kipato kutoka kwa wafanyabiashara.
Aliyezuiliwa mizigo baada ya kushindwa kulipa kodi aliyokadiriwa kwa mujibu wa Sheria nayo utasemaje? Watu wanafata sheria. Mwanzo mliwaita wapiga dili leo maji yamezidi unga eti tunashangaa.
 
Sheria zipo sawa...

Ila kuna watendaji wamekua wakizitumia ndivyo sivyo... mabavu mbele busara kushoto...

Sheria zinatungwa kwa nia njema... ghafla tu hata bila kutoa elimu kwa wananchi utashangaa tuu, kuanzia sasa ni hivi.. hivi na hivi...

Cc: mahondaw
 
Hizi kodi anazozipiga vijembe sio ndio huyuhuyu alisema anakusanya kuliko waliomtangulia tena wananchi wakaitwa wanaolalamika kuwa wapiga dili si ni huyu huyu rais?

Sio huyu aliyesema lazima kodi zilipwe hadi tra wakawa wanatembea na bunduki na askari polisi na waziri mkuu akawatetea bungeni?

Sio huyu baba aliyeanzisha kodi za machinga kwa tamko?

Na sheria si wao ndio wanatunga na kupeleka miswada bungeni na huyu baba si ndio anasaini inakuwa sheria?

Kuna kodi inayokusanywa ambayo haipo kwenye sheria? Kwanini walaumie watendaji wanaofuata sheria badala ya watunga sheria?
Kiuhalisia wewe huna biashara. Anzisha biashara hata moja kwanza
 
Hizi kodi anazozipiga vijembe sio ndio huyuhuyu alisema anakusanya kuliko waliomtangulia tena wananchi wakaitwa wanaolalamika kuwa wapiga dili si ni huyu huyu rais?

Sio huyu aliyesema lazima kodi zilipwe hadi tra wakawa wanatembea na bunduki na askari polisi na waziri mkuu akawatetea bungeni?

Sio huyu baba aliyeanzisha kodi za machinga kwa tamko?

Na sheria si wao ndio wanatunga na kupeleka miswada bungeni na huyu baba si ndio anasaini inakuwa sheria?

Kuna kodi inayokusanywa ambayo haipo kwenye sheria? Kwanini walaumie watendaji wanaofuata sheria badala ya watunga sheria?

Huna hoja yoyote hapa Ndugu yangu
 
Kinacholalamikiwa siyo sheria, tatizo ni hao watendaji wa tra kutafsiri kivyao hizo sheria kwa njia ya kujipatia pesa wao binafsi isivyo halali
 
Kosa lao ni kusema maagizo kutoka juu, wamemchanganisha mkuu na wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom