TRA na USHURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA na USHURU

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JAMIETZN, Apr 21, 2010.

 1. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salamu.

  Najaribu kutaka kujua ajira za TRA zinapatikana je hasa kwa maeneo ya Longroom.

  Je nahitaji kuwa na Elimu ya aina gani kuweza kupata ajira maeneo kama yale ? Na je Kuna kufahamiana fahamiana katika kupata ajira za TRA hasa makao makuu ?

  Sitaki kuamini kwamba waliopo pale Longroom ni watoto wa wakubwa au wakufahamiana kama wasemavyo walio wengine.

  NB: Na kumbuka kuna member hapa Jamii aliuliza au alitaka kujua ni vigezo gani vinavyo chukuliwa na vijana wa hapa Longroom katika kupandisha bei (
  Ku uplift ) bei za bidhaa ambazo zilisha fanyiwa malipo, mfano bei mizigo kutoka China au bei za magari?

   
 2. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Wafanyakazi wa TRA wako wengi,kuna walioingia kwa migongo ya vigogo(although ni ngum kudhibitisha) na walioingia haki bin haki.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuwa Mchagga na tafuta Kigogo akupenyeze!
   
 4. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo walio wengi pale wachagga na pia weshapenyezwa. Hahaaa..Duh hata wanaume wanapenyezana ? Basi hata hiyo kazi sitaki..
   
 5. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huenda hii ya kuingizwa mingongoni na mwa vigogo ikawa ina ukweli ndani yake, Masanilo anasema( wanapenyezwa), kwani si dhani wale vijana wa Longroom wana tumia Elimu zao.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Si kihivyo! Kigogo akupe kimemo
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Najua si neno sahihi (wale jamaa ni wajinga) reasoning yao duuuuu
   
 8. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ina ogopesha.. TRA hakuna sheria za mapato ambazo zinafanya kazi. Jitu likiamkia kwenye supu ya utumbo likifika pale linaweka bei yoyote ya ushuru. Halafu hawa watu wana kiburi fulani.
   
 9. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #9
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mkuu kimemo tu bila chochote kitu utakipewa na nani ?
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Inategemea wewe ni nani katika nji hii! Ajira za TRA lazima upelekwe na mtu na ukweli ndio huo!
  Pia lazima hata ukipelekwa na mtu utaanzia Mtwara
  then utaamishiwa Kigoma utapelekwa Musoma
  halafu ndio utarudi Dar hapo chumba-kirefu!
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tafuta urafiki na akina Lowassa ama mzee wa standard and speed.....hapo lazima upate kazi!
   
 12. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #12
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi hao watu huwa nawaona tu kwa mbali wakipita kwenye motokaa, Hata uwezo wa kusalimiana nao sina. Ila vyeti vyenye kukidhi qualifications za longroom natumaini ninavyo.
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu hata mabinti zao huwezi wavizia makanisani?
   
 14. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #14
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kuna vijana pale hata mikoani hawakujui. Niamini..
   
 15. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #15
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haa hahahaaaaaa!!!! Masanilo huu mzaha sasa..!
   
 16. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,747
  Trophy Points: 280
  hili suala kwa kweli linatakiwa kuangaliwa kwa makini,ukitaka balaa import kitu ambacho hawajawahi kukiona wala kukisikia,kwanza hawajui hata wapi wakatafute detail sasa utaletewa bei yao ya ajabu ambayo inaweza kukupa nafuu ya ajabu au hasara ya ajabu.kwa kweli kama alivyosema MASANILO reasoning yao duuhh.
   
 17. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #17
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hivi tuna kwenda wapi na hali ya jinsi hii ? Huku ni kudumaza uchumi wa nchi, Kwasababu sasa kwanza watu wataogopa hata kuingiza bidhaa nchini na matokeo yake bei za vitu zitakuwa juu sana. Sitegemei kuona mtu kalipia ushuru wa milioni 7 au 9 kwenye Toyota Mark II aje kukuuzia gari hiyo kwa milioni 10.

  Kama TRA wataendeleza hali hii ya ajabu ajabu ya kubuni bei za vitu ambavyo tayari vimesha lipiwa na document original zikaonyesha malipo halali, Itatokea kuwaumiza wananchi walio maskini.
   
 18. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wa TRA wameanzisha tabia moja mbaya sana, Ambayo kama itaendelea hivyo itakuja kutuletea madhara makubwa japo kwa sasa tulio wengi hatujaweza kulitambua hilo.

  Ina shangaza sana kuona Mtanzania mwenzio anakuja kukupangia bei ya kitu ambacho ulishalipia nje ya nchi na kukithamanisha kwa bei anayo taka yeye . Huu ni utaratibu gani ? Let say mtu ananunua Plasma TV yake nje ya nchi kwa ml 2 na risiti au invoice aliyofanyia malipo anayo, wewe unakuja kupanga bei kwenye TV hiyo mfano Ml 3 au hata laki 3.

  Huu utaratibu wanaofanya hawa jamaa sio mzuri, Huku ni kuwakomoa watanzania walio wengi. Hata kama ni kukusanya kodi, watu hawakusanyi kodi kwa utaratibu wa namna hii. Ni heri basi ikawekwa bayana kwamba unapo nunua kitu nje ya nchi na kukiingiza Tanzania mnakipa bei ingine tofauti na ile mtu anayo nunulia.
   
 19. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,747
  Trophy Points: 280
  kinachosikitisha mkuu,ni mimi mlalaho nachajiwa tsh 7mil kwa mark2 wakati kuna mtu mwingine anachajiwa 6mil tsh kwa RANGE ROVER VOGUE!!!
   
 20. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,747
  Trophy Points: 280
  hii tabia yao ya ku-uplift ushuru kwa bei za ajabu ndio inafanya watu watumie kila mbinu kukwepa ushuru
   
Loading...