TRA na Fire-Extinguisher za Pikipiki...mmmh! jamani

NAFIKIRE

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
634
415
Wadau hili swala la kwenda TRA na kudaiwa elfu kumi kulipia fire extinguisher ya pikipiki naona kama halijakaa sawa...Naomba tulijadili hili kwani naona ni njia mojawapo ya kuwaumiza walala hoi..Mimi sioni mantinki ya kununua fire-extinguisher ya pikikiki kwani sioni utaitumia wapi na wakati gani.karibuni mtoe maoni yenu
 
Mtakoma, soon wataanza kudai fire extinguisher za baiskeli na watu,kila mtu atembee nayo kwenye pochi.

Hayo ni matokeo ya kupeana AJIRA bila kufuata weledi. Sasa huko TRA kumejaa wapuuzi wenye ubunifu SIFURI wa jinsi ya kupanua wigo wa kodi.

Pathetic
 
Duuuuuh kweli hii ndo tanzania yaani sijui uwaambie nn .... Yaani mtu anakulindia uhai wako ila hutaki
 
Duuuuuh kweli hii ndo tanzania yaani sijui uwaambie nn .... Yaani mtu anakulindia uhai wako ila hutaki

Unaweza ukafafanua?

Sasa hivi tunataka tulete fire extinguisher za mikokoteni na wilbaro then tuje kwenye fire extinguisher za kuku
 
Duuuuuh kweli hii ndo tanzania yaani sijui uwaambie nn .... Yaani mtu anakulindia uhai wako ila hutaki
Anakulindaje uhai wako kwa faya eksitinguisha?Takwimu za mioto iliyozimwa au mali zilizookolewa kwa kifaa hicho zaidi ya kutaka kukusanya pesa haramu kwa matumizi haramu?Hata siku mija ktk ukaguzi wa hivyo vifaa ulishawahi kusikia au kuona wakihusisha pikipiki?Au ilimuradi tu na ww tujue upo?
 
Ifike mahali viongoz wakuu wa serekali wawakemee hawa wanaobuni mirad inayowahumiza wananchi,mradi huu tena kwa pkpk aisee ni hatari .Kwa maoni yangu naona ni ukosefu wa ubunifu wa vyanzo vya mapato.
 
Waliuza viwanda na wakaja na mbinu ya ubunifu kwenye vyombo vya usafiri. Gari au pikipiki ukinunua kiwandani hupewi hiyo fire ext.. na hata wakitengeneza sioni mahali pa kuweka au vishikizo vya hiyo kitu. Pia moto wa mafuta ya petrol au diesel hauwezi kuzimwa na hicho kichupa cha robo kilo. Hii ni kodi haramu kati ya kodi zinazofanywa na TRA
 
Road licence, Road toll (kwenye mafuta), wiki ya nenda kwa usalama, fire ext.. Huu ni wizi mtupu.
 
Unaweza ukafafanua?

Sasa hivi tunataka tulete fire extinguisher za mikokoteni na wilbaro then tuje kwenye fire extinguisher za kuku

Ukitulia na ukatumia akili utajua kwanini wanakuambia uweke Fire Extinguisher kwenye Gari na Pikipiki..

Si mihemko ya kuku na mikokoteni
 
Anakulindaje uhai wako kwa faya eksitinguisha?Takwimu za mioto iliyozimwa au mali zilizookolewa kwa kifaa hicho zaidi ya kutaka kukusanya pesa haramu kwa matumizi haramu?Hata siku mija ktk ukaguzi wa hivyo vifaa ulishawahi kusikia au kuona wakihusisha pikipiki?Au ilimuradi tu na ww tujue upo?

Acha papara zisizo za Msingi... Ungekataa basi hata kufundishwa matumizi ya Fire Extinguisher huko primary na secondary kama unaona hazikusaidii

Pikipiki ni chombo cha Moto sehemu yeyote inayohusu moto lazima fire Extinguisher iwepo...... kutokuona ukaguzi katika pikipiki ni makosa lazima kila sehemu kwenye hatari ya Moto kuwe na Fire Extinguisher kwa Mtu aliyeelimika

Mbona Hujauliza kama majumbani kinatakiwa Fire Extinguisher ingawa Sheria ya zima moto inakulazimu uweke fire Extinguisher nyumbani kwako..

Kama hujui kitu Nyamaza
 
Wadau hili swala la kwenda TRA na kudaiwa elfu kumi kulipia fire extinguisher ya pikipiki naona kama halijakaa sawa...Naomba tulijadili hili kwani naona ni njia mojawapo ya kuwaumiza walala hoi..Mimi sioni mantinki ya kununua fire-extinguisher ya pikikiki kwani sioni utaitumia wapi na wakati gani.karibuni mtoe maoni yenu

Kumbe Jambo si kununua bali utaitumia wapi.......

Ok Fanya hivi washa pikipiki yako fungua Tank la mafuta halafu tia Kiberiti ..... utajua matumizi ya Fire Extinguisher
 
Back
Top Bottom