TRA na Fire-Extinguisher za Pikipiki...mmmh! jamani

hivi kuna fire extinguisher ina youzwa elfu kumi 10 000?maana hata ukilipa unapewa sticker tu na sio fire extinguisher,hivi unaweza kuzima moto kwa kutumia sticker?na hapo sijui maisha ya mtu yanalindwa je sasa! Fikiria vizuri hapo.

Nimesema Fire Extinguisher inauzwa Elfu kumi??... kwani ukipigwa Faini ya Tairi bovu basi hilo tairi linauzwa Hiyo hela....

Nunua Fire Extinguisher
 
Kazi ya hii 10000 ni mini? Huwa ni kuuziwa hii chupa, kuikagua au ni kusaidia jeshi la polisi idara ya zimamoto kujiendesha?
Manake tunalipa lakini hatupewi inabidi kwenda kununua wenyewe au kujaza wenyewe kwa gharama ingine.
Hazikaguliwi kwa muda husika na zikikaguliwa ni kwa utaratibu gani?
 
Naamini utaratibu wa kodi bila maelezo kwa yule anaetozwa ni wa kawaida sana hapa nchini Ingekua jambo la busara huyu ananelipa hiyo kodi akaelimishwa kwanza ili aelewe. Akishaelewa hii mitafaruku na ugumu wa kutaka kuilipa hiyo kodi itapungua au kuondoka kabisa
 
Ukitulia na ukatumia akili utajua kwanini wanakuambia uweke Fire Extinguisher kwenye Gari na Pikipiki..

Si mihemko ya kuku na mikokoteni

Hujafafanua lolote.

Wewe unajua au ulishafundishwa kutumia hiyo fire extinguisher au unawekaga kwenye Pikipiki kama urembo tu?
 
Acha papara zisizo za Msingi... Ungekataa basi hata kufundishwa matumizi ya Fire Extinguisher huko primary na secondary kama unaona hazikusaidii

Pikipiki ni chombo cha Moto sehemu yeyote inayohusu moto lazima fire Extinguisher iwepo...... kutokuona ukaguzi katika pikipiki ni makosa lazima kila sehemu kwenye hatari ya Moto kuwe na Fire Extinguisher kwa Mtu aliyeelimika

Mbona Hujauliza kama majumbani kinatakiwa Fire Extinguisher ingawa Sheria ya zima moto inakulazimu uweke fire Extinguisher nyumbani kwako..

Kama hujui kitu Nyamaza

Hiv boda boda Wa Kenya,Nigeria, Uganda, Malawi, USA, Zambia nk sijaona wana fire extinguisher au si ndo Wa kuanzisha hili
 
Hujafafanua lolote.

Wewe unajua au ulishafundishwa kutumia hiyo fire extinguisher au unawekaga kwenye Pikipiki kama urembo tu?

Mimi najua matumizi na Jinsi ya kuzitumia hizo Fire Extinguisher sikurupuki tu..

Nimefundishwa toka Primary na Secondary pia kulikuwa na Fire Extinguisher na Kazini zipo pia.....

Si mpaka moto utokee ndo ukumbuke Fire Extinguisher kununua au jinsi ya kuitumia.. Jitahadhalishe mapema na Jukumu la Kukagua Fire Extinguisher ni lako ili uwe salama Zaidi.. Maelezo huwa yanatolewa wakati wa kuzifunga sasa kama Unafungiwa tu hudai maelezo ya jinsi ya Matumizi utaonekana mjinga
 
Haya ndio mambo ya msingi ya wenye boddaboda kuandamana.

Nchi hii haramu inahalalishwa sijawahi kuona bodaboda kuungua au kusababisha moto sehemu yoyote kwenye maisha yangu ya miaka 55
 
Haya ndio mambo ya msingi ya wenye boddaboda kuandamana.

Nchi hii haramu inahalalishwa sijawahi kuona bodaboda kuungua au kusababisha moto sehemu yoyote kwenye maisha yangu ya miaka 55

Kwahiyo mpka uone Pikipiki ikiwaka Moto ndo unakumbuka Fire Extinguisher? ??

Na wewe ni Mungu Unaona Kila Sehemu ... usipoon Wewe jua kuna Watu imeshawatokea
 
kuna watu wana mahaba niue na mfumo wa kifala unaotumika kukusanya kodi hapa nchini.wanafaidika na upuuzi huu.Kitaeleweka tu mbele ya safari yetu macho.traffic &tra iko siku tu
 
Mimi najua matumizi na Jinsi ya kuzitumia hizo Fire Extinguisher sikurupuki tu..

Nimefundishwa toka Primary na Secondary pia kulikuwa na Fire Extinguisher na Kazini zipo pia.....

Si mpaka moto utokee ndo ukumbuke Fire Extinguisher kununua au jinsi ya kuitumia.. Jitahadhalishe mapema na Jukumu la Kukagua Fire Extinguisher ni lako ili uwe salama Zaidi.. Maelezo huwa yanatolewa wakati wa kuzifunga sasa kama Unafungiwa tu hudai maelezo ya jinsi ya Matumizi utaonekana mjinga

Shule ya primary na secondary umefundishwa? Shule nzuri hiyo.

Kwahiyo nikilipa tu naenda napewa fire extinguisher na maelezo jinsi ya kutumia?
 
Wadau hili swala la kwenda TRA na kudaiwa elfu kumi kulipia fire extinguisher ya pikipiki naona kama halijakaa sawa...Naomba tulijadili hili kwani naona ni njia mojawapo ya kuwaumiza walala hoi..Mimi sioni mantinki ya kununua fire-extinguisher ya pikikiki kwani sioni utaitumia wapi na wakati gani.karibuni mtoe maoni yenu

Mgombea uraisi wa ukawa lazima tukubaliane nae kwamba ataondoa kodi za kukera kama mwinyi alivyoondoa kozi za kichwa,huu wizi wa mchana haukubaliki,kero nyingine ni service charges za tanesco ni wizi wa mchana kabisa.Kama Mgombea yeyote atakayeondoa hizo kero hizi nitampigia kampeni ya kutosha.

KODI ZA KUKERA NI:-
1.TLB-Unalipia TLB wakati ukijaza mafuta unakatwa tena kodi ya kuchangia barabara
2.Service Charges na Kulipia EWURA/REA huu ni wizi(Ewura inabidi walipwe na serikali,Serikali ilipe gharama za REA wao wenyewe na si mwananchi.
3.Fire Extinguisher nainunua mwenyewe na nisikatwe hizo elfu 10 na kuendelea(kutegemea cc ya gari).

Serikali ina vyanzo vingi vya mapato tu kwenye Mali asili vinatosha kulipa mishaara,kulipa REA,kujenga barabara etc
1.Kodi ya mikaa/miti/mbao
2.Kodi ya uvuvi/samaki
3.Kodi ya bandarini kuingiza/kutoa bidhaa nje/ndani ya nchi.
4.VAT(Bidhaa zote tunazonunua tunalipia kodi.
5.Wakusanye kodi kwenye madini hiyo 3% ni ndogo,tufanye kama Zimbabwe(Not SUre) wanakusanya 50%.
6.Kodi ya PAYE kwa wafanyakazi na wafanyabiasha(including wasanii).
7.Naungana na January Makamba,serikali ikusanye kodi kwenye Kupanga nyumba,kuuza etc

Hivyo vyanzo vya mapato 7 vinaweza kuendesha serikali bila kukopa nje.

cc: Dr.W.Slaa , Freeman A. Mbowe , Julius Mtatiro , John Mnyika , Mikael P. Aweda , Yericko Nyerere , Ben Saanane , Josephine , Prof. Anna Tibaijuka , Jamal Malinzi , Adrian Stepp , Jackton Manyerere , Zitto , W. J. Malecela , Ritz , Kilaza EMT , Jason Bourne.
 
Shule ya primary na secondary umefundishwa? Shule nzuri hiyo.

Kwahiyo nikilipa tu naenda napewa fire extinguisher na maelezo jinsi ya kutumia?

Sehemu unaponunua Fire Extinguisher lazima Upewe maelekezo ya Kuitumia.... Na usipopewa una haki ya Kulalamika Ili ujue jinsi ya Kuitumia OVER
 
Sehemu unaponunua Fire Extinguisher lazima Upewe maelekezo ya Kuitumia.... Na usipopewa una haki ya Kulalamika Ili ujue jinsi ya Kuitumia OVER

OK, kwa hiyo dukani watanielekeza.

Ila nalipa TRA then naenda kununua dukani tena au hela nayolipa TRA ni ya nini?
 
Mtakoma, soon wataanza kudai fire extinguisher za baiskeli na watu,kila mtu atembee nayo kwenye pochi.

Hayo ni matokeo ya kupeana AJIRA bila kufuata weledi. Sasa huko TRA kumejaa wapuuzi wenye ubunifu SIFURI wa jinsi ya kupanua wigo wa kodi.

Pathetic

Du du du nimecheka sana sana. Uliyosema ni kweli kabisa. Siku si nyingi kila mtu atatakiwa kutembea nayo. Ikifika wakati wa ku-create namna ya kukusanya fedha Tanzania ni vituko vya hali ya juu. Ukisafiri kwenye barabara zetu siku hizi mabasi huwa yanalazimika kuingia kwenye vistendi vya ajabu sana... ili tu kukusanya ushuru. Mimi naona sisi wananchi ndio tatizo kwani tunapelekeshwa kama makondoo wala hatuhoji!
 
OK, kwa hiyo dukani watanielekeza.

Ila nalipa TRA then naenda kununua dukani tena au hela nayolipa TRA ni ya nini?

Hili ndio swali langu hasa.
Na je ni vyombo vya usafiri tu vinalipiwa 10000 kwa service charge ya kifaa au hata majumbani pia tukalipie?
 
Duuuuuh kweli hii ndo tanzania yaani sijui uwaambie nn .... Yaani mtu anakulindia uhai wako ila hutaki

Wewe hata baiskeli huna!!! Ukilipa hiyo pesa ya fire extinguisher iwe ni kwa pikipiki, gari ndogo au kubwa, unapewa hiyo extinguisher???
 
Back
Top Bottom