TRA Msimstafute Mchawi. Mchawi ni TRA

TRA Msimstafute Mchawi. Mchawi ni TRA

Mwingereza

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
1,115
Reaction score
2,771
Kwa makusudi Kabisa, TRA inahujumu (Sabotage) Jitihada za Rais Magufuli kuelekea Uchumi wa Viwanda.

Kwa kipindi kirefu, TRA wamekuwa ni wababe, wamelalamikiwa sana. Hawamskilizi mtu, wamekuwa wakifanya mambo kwa kukurupuka na kukomoa. Unafungua biashara wanakuja na kukupa makadiro ya kutisha kabla ya kuanza biashara. Wafanya biashara wakaanza kwenda nchi jirani

Unaleta bidhaa bandarini, wanakupa ushuru mkubwa kuliko thamani ya bidhaa, unapobisha, unaombwa rushwa kubwa ili amigo wako utoke. Mwisho wa siku wafanya biashara wakaanza kusita kuagiza.Na ndio maana mizigo nayo ikapungua. Hapa mchawi ni nani?

Wafanya biashaa wadogowadogo wanalaimishwa kununua EFD machine wakati mitanni yao ni midogo kuliko thamani ya EFD. Kwa nini wasifunge biashara? Hapa Mchawi ni Nani?

Sehemu zingine kama mabaa na grocery, TRA wanajificha wakihesabu umeuza nini, hata beer na chakula wnahesabu umeuza ngapi kisha wanakuvamia wanataka kodi. Hii inafanyika wapi? Mfuga kuku anavamiwa nyumbani kwake alipe kodi. Kwa nini wasifunge, wakati wanahangaika na kuku wanaokufa?

Kodi nchini Tanzania inatumika kama adhabu na kukomoana. TRA inaajiri vijana wasiojitambua, wanatishia walipa kodi. wanatisha kuifunga biashara yako na kupiga mnada ulivyo navyo kama hukubali kulipa kodi waitakayo. hasa wakinyimwa rushwa wanayoitaka wao. Duniani kote, hakuna serikali inayokusanya kodi kwa mtu ambaye hajauza hata chupi. Makadirio ya kodi, hiyo kodi inatoka wap wakati biashara hata bado? Anafanya tathmini, hata ya mwaka, wakati mwingine hata mwaka haufiki?

Uchumi wa Nchi hauendeshwi na kodi.Uchumi unaendeshwa na uzalishaji
 
Haha ha haaa... Naunga mkono hoja! Hawa jamaa wamekua nuksi kwa maendeleo ya nchi yetu halafu hawajulikani!
 
Wameamua kumhujumu Rais Magufuli na Serikali ya Viwanda. TRA ndio wachawi
Mbona malengo ya kiasi gani kikusanywe anapanga mwenyewe magu?meneja Wa Tra usipofikia kiwango kilichowekwa unatumbuliwa
 
Kitu kinachekesha Sana ujaanza biashara wanakwambia kalipe makadilio ya kodi. Hawa watu kama wafu jama wanakadiria kuzimu wakati kabuli ni dogo muno. Mtu ajaanza biashara ana elimu nabiashara pesa kapewa na Mjomba baada ya kukaa nyumbani na huyu ni yatima serikali inamvamia na kuomba tushwa au makadirio makubwa
 
Mfumo mzima Wa kodi tz ni mbovu jiulize tu kwanini bidhaa Uganda ni cheap Mara tatu ya Uganda wakati mganda anatolea mzigo hapa dar?

Kwanini wanatoza kodi kwa siri? Yaani ukitaka kuagiza mfano vitege hujui kodi unakuja kupigwa ngapi?na unaweza kupitisha bidhaa aina moja kila MTU akapigwa kodi yake
 
Lipa Kodi Kwa Maendeleo ya Taifa, Acha Kuhujumu Uchumi Mimi Mwenyewe nalipa Kodi Kila Mwezi ambapo Sasa Imefika Sh. 345,400 kwa Mwaka nalipa Sh.4,114,400 na Silalamiki Najivunia Kulipa Kodi.
 
Wameamua kumhujumu Rais Magufuli na Serikali ya Viwanda. TRA ndio wachawi
Watabaki peke yao kufanya biashara, ngoja tuhamie Zambia, tuchangie uchumi wa Zambia pia ni Jirani zetu,nyie endeleeni kufirisika huko sie tunazidi kuongeza maduka huku.
 
Mfumo mzima Wa kodi tz ni mbovu jiulize tu kwanini bidhaa Uganda ni cheap Mara tatu ya Uganda wakati mganda anatolea mzigo hapa dar?

Kwanini wanatoza kodi kwa siri? Yaani ukitaka kuagiza mfano vitege hujui kodi unakuja kupigwa ngapi?na unaweza kupitisha bidhaa aina moja kila MTU akapigwa kodi yake
True hata dizeal huku Zambia Lita ni 1200 na inapitia Bandari ya dar,Magari huku bei poa.
 
Lipa Kodi Kwa Maendeleo ya Taifa, Acha Kuhujumu Uchumi Mimi Mwenyewe nalipa Kodi Kila Mwezi ambapo Sasa Imefika Sh. 345,400 kwa Mwaka nalipa Sh.4,114,400 na Silalamiki Najivunia Kulipa Kodi.
Mkuu hizo ni namba tu ambazo mtu yeyote anaweza kuandika. Weka ushahidi kama ni kwelli unalipa hicho kiasi. Kama ni mfanyakazi weka salary slip, kama ni mfanyabiashara weka Bank-pay-in slip. Vinginevyo hizo ni porojo tu, ID yenyewe fake!!
 
niliwahi kuwauliza watumishi wa TRA Samora hivi nikifunga biashara na bado wengine wakafunga wanafikiri na wao watakuwa salama na ajira zao maana wao wanajisikia furaha ukifunga biashara wanasahau hata kile kidogo ulichokuwa ukilipa hawatakipata hayo ndio matokeo yake.
Umepata tenda wanakunyima tax clearance tena wanachekelea kabisa
 
Tanzania tunatakiwa kutubu.
Raisi mwenyewe wa Inchi haeleweki anampango gani.
Wanainchi wenyewe ugumu wa maisha na stress nao hawaelewi nini wafanye.
Wafanya biashara ni manyanyaso na vitisho toka TRA.
Polisi wamekuwa Mungu watu.
Wakulima hawana pakukimbilia.
Watumishi wa serekali wamekuwa wanyonge nakufanya kazi kishingo upande.

MFANYA BIASHARA UKIPATA FURSA NJE YA INCHI USIPOTEZE MUDA.
 
Jamaa zangu kibao wapo Lusaka,Ndola na Solwezi Zambia, Mimi mwenyewe muda sio mrefu nitakua huko.

Zambia wametega mikono na miguu kuwapokea wafanyabishara wageni.

Hapa tu Nakonde ukihamia kwao wanakuona kama malaika ..

Zamani wenye mitaji midogo ndio wanakimbilia Zambia kujikuza....Siku hizi wafanyabishara wakubwa ndio wanakimbilia huko.

Tanzania tutakuja kusalimia familia na kujenga nyumba basi ...... mpaka sera zitapobadilika.
 
Lipa Kodi Kwa Maendeleo ya Taifa, Acha Kuhujumu Uchumi Mimi Mwenyewe nalipa Kodi Kila Mwezi ambapo Sasa Imefika Sh. 345,400 kwa Mwaka nalipa Sh.4,114,400 na Silalamiki Najivunia Kulipa Kodi.
hebu weka risiti hapa ili tuamini! Vinginevyo ni uongo wa kiwango cha lami!
 
niliwahi kuwauliza watumishi wa TRA Samora hivi nikifunga biashara na bado wengine wakafunga wanafikiri na wao watakuwa salama na ajira zao maana wao wanajisikia furaha ukifunga biashara wanasahau hata kile kidogo ulichokuwa ukilipa hawatakipata hayo ndio matokeo yake.
Umepata tenda wanakunyima tax clearance tena wanachekelea kabisa
Ni wakati wafanyakazi wote wa TRA wachunguzwe mali zao, mienendo yao kila kona maana wapo wengi ni wala Rishwa na wapiga madili wakubwa.
 
  • Thanks
Reactions: KKC
TRA ni genge la wahuni likiongozwa na yule mnyaruanda anayetaka kuombewa kila kukicha
 
Back
Top Bottom