tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Kumekuwa na malalamiko kila kukicha kwa TRA pale Bandarini kutoka kwa wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi kuhusu kupandishiwa bei ya kununuliwa biadhaa huko nje kwa kisingizio kuwa wao TRA wanautaratibu wao wa kukadiria bei za bidhaa yaani assesment price kulingana na sheria inavyowataka yaani bei ya soko.
TRA wamekuwa wakiwakadiria bei za juu sana wafanyabiashara wanaotoa mizigo kupitia bandari zetu kiasi cha wengine kuhama bandari ni kuhamia Mombasa ili kupata unafuu wa baadhi ya kodi.
Nakumbuka hata niliponunua gari toka Japan ile invoice iliyotumwa toka Japan TRA walikataa wakatoa bei yao ambayo ilikuwa juu ili tu nilipe kodi ya juu na hilo ni tatizo kubwa kiasi kwamba kuna watu wengine wanatelekeza magari yao hapo bandarini.
Na mfano wa jana yule mama wa kutoka Dodoma anayezalisha mvinyo wa Dodoma kwa zabibu alilalamika mbele ya Rais kuhusu kontena la chupa kukwama bandarini kisa kapandishiwa bei ya kununua hizo chupa za kujazia mvinyo yaani Dododma wine na Rais aliamuru huyo mama alipe kodi kutokana na invoice yake inavyosema na leo kontena liwe limetoka bandarini.
Maafisa wa TRA mmekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya watanzania kwa kuwapa kodi za juu na ndiyo maana jana malalamiko mengi yalikuwa kuhusu kodi.
Nakumbuka kulikuwa kuna kontena la dawa na vifaa vya hospitali ya Kahama kutoka Canada mwaka jana kwa wafadhili tu wa msaada wa huduma za kijamii lakini hilo kontena lilikaa bandarini zaidi ya miezi 3 na kiasi cha wale wafadhali kuacha kuleta misaada tena ya huduma za afya Kahama kutokana na kulipia gharama kubwa sana kutokana na sababu zisizo na tija kwa taifa kwa baadhi ya maofisa wa TRA.
TRA fuateni maagizo ya Rais na pia muwaamini wafanyabiashara kwa invoice zao siyo mnaongeza bei wakati sio TRA mlionunua hizo bidhaa.