TRA kwanini hawaziamini invoice zinazowasilishwa na wafanyabiashara bandarini kutoka nje ya nchi

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,788
4,490
Kumekuwa na malalamiko kila kukicha kwa TRA pale Bandarini kutoka kwa wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi kuhusu kupandishiwa bei ya kununuliwa biadhaa huko nje kwa kisingizio kuwa wao TRA wanautaratibu wao wa kukadiria bei za bidhaa yaani assesment price kulingana na sheria inavyowataka yaani bei ya soko.

TRA wamekuwa wakiwakadiria bei za juu sana wafanyabiashara wanaotoa mizigo kupitia bandari zetu kiasi cha wengine kuhama bandari ni kuhamia Mombasa ili kupata unafuu wa baadhi ya kodi.

Nakumbuka hata niliponunua gari toka Japan ile invoice iliyotumwa toka Japan TRA walikataa wakatoa bei yao ambayo ilikuwa juu ili tu nilipe kodi ya juu na hilo ni tatizo kubwa kiasi kwamba kuna watu wengine wanatelekeza magari yao hapo bandarini.

Na mfano wa jana yule mama wa kutoka Dodoma anayezalisha mvinyo wa Dodoma kwa zabibu alilalamika mbele ya Rais kuhusu kontena la chupa kukwama bandarini kisa kapandishiwa bei ya kununua hizo chupa za kujazia mvinyo yaani Dododma wine na Rais aliamuru huyo mama alipe kodi kutokana na invoice yake inavyosema na leo kontena liwe limetoka bandarini.

Maafisa wa TRA mmekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya watanzania kwa kuwapa kodi za juu na ndiyo maana jana malalamiko mengi yalikuwa kuhusu kodi.

Nakumbuka kulikuwa kuna kontena la dawa na vifaa vya hospitali ya Kahama kutoka Canada mwaka jana kwa wafadhili tu wa msaada wa huduma za kijamii lakini hilo kontena lilikaa bandarini zaidi ya miezi 3 na kiasi cha wale wafadhali kuacha kuleta misaada tena ya huduma za afya Kahama kutokana na kulipia gharama kubwa sana kutokana na sababu zisizo na tija kwa taifa kwa baadhi ya maofisa wa TRA.

TRA fuateni maagizo ya Rais na pia muwaamini wafanyabiashara kwa invoice zao siyo mnaongeza bei wakati sio TRA mlionunua hizo bidhaa.
 
TRA ni tatizo kubwa la biashara katika nchi hii! Mentality yao ni kwamba wanawachukulia wafanyabiashara wote kua ni wezi na wakwepa kodi! Kwa mindset hiyo wameua biashara ya nguo na wameua biashara ya vipuri vya magari kama ambavyo watakuja kuua biashara ya vifaa vya ujenzi. Unapowaletea Invoice ya bidhaa ulizoingiza nchini ni mara chache sana wakaipitisha kama ilivyo labda waone mabei makubwa sana
Unaweza kuingiza nchini container la vipuri vya magari ambalo mara ya mwisho ulilipia 15-18Mil next time the same consignment with the same quantity and value ukatakiwa ulipie 35-40mil! NA ukiwapa reference wanakwambia kila shipment ina historia yake, yaani hakuna consistence,

na ukishindwa mzigo wako unapigwa mnada. Hii taasisi ni changamoto kwa biashara kwakweli
 
Karibuni Dunia nzima siku hizi wanatumia Electronic Single Window System.Hii baada ya kuagiza gari au bidhaa zingine muuzaji utuma invoice copy tokea ofcn kwake kwenda kwa wahusika wote kuanzia custom,watu wa vibari na meli.Pia Automatically copy utumwa Kwenye idara ya forodha ya nchi inapoenda mzigo,Mfano ikifika TRA Tanzania ,system itatuma pia hiyo invoice TBS,TDFA, n.k ...hapa mteja awezi ongopa bei kwani copy anatuma alieuza mzigo.Sasa hapa Tanzania ukweli wateja wanafoji Invoices na ana kuwa na copy ya kupeleka TRA ,copy ya TBS,Copy ya TAEC ili aweze lipa fees na kodi chini ya kiwango.
Dawa ya kuondokana na hili Tatizo hapa Tanzania ni Electronic Single Window System. Akuna mbadala na aliepukiki.,Rwanda,Kenya,Uganda,Zambi kote wanatumia EWS
 
Wafanyakazi wengi wa TRA wanacheza sana na akili za walipa kodi. Huwa sielewi kabisa estimation zao wanazifanya kwa taratibu gani.

Pengine tuachane na mambo ya estimation. Kuwekwe utaratibu huru ambao unaeleweka wa namna ya kulipa kodi. Kukadiria kodi kunatumika vibaya kuwakandamiza wafanya biashara
 
Wajitathimini upya TRA wao ndio kikwazo katika kuelekea Tanzania ya viwanda.
Ni kweli TRA wajiangalie upya kwasababu haiwezekani upandishiwe invoice price wakati umeletewa origin invoice toka Japan then wewe TRA hutaki unategemea mteja afanye nini kama si kumkatisha tamaa na kumrudi nyuma kimaendeleo
 
Wafanyakazi wengi wa TRA wanacheza sana na akili za walipa kodi. Huwa sielewi kabisa estimation zao wanazifanya kwa taratibu gani.

Pengine tuachane na mambo ya estimation. Kuwekwe utaratibu huru ambao unaeleweka wa namna ya kulipa kodi. Kukadiria kodi kunatumika vibaya kuwakandamiza wafanya biashara
Hiyo point ya msingi sana
 
tatizo wa tz wamezoea kupika documents
Kama hawaziamini documents zetu TRA wawe madalali basi wawe wanaleta mizigo tununue kwao,maana wao ndo wanazijua bei,maana tukija na invoice zetu hawaziamini,wanataka za kwao sasa kuna haja gani ya kuagiza mzigo wakati wao ndo ujua bei. Nchi zote zinazotuzunguka hawana shida na invoice toka Kwa mnunuzi ndo kusema sisi ni smart sana,kama tunapika data,una kifaa kipi kujua hii data halisi hii siyo,mifumo yao ndo inawafundisha watu kukwepa kodi,mizigo haipiti bandarini kodi kubwa lkn utakuta imejaa mitaani,inapita wapi njia za panya,kodi kubwa makusanyo haba,si wangefanya kama nchi za majirani zetu kodi nafuu makusanyo makubwa,pia wameisingle,na uoni ulazima wa kuikwepa sababu inalipika.Labda kama ni tools ya kuwafanya wengi waishi kama mashetani hapo sawa.
 
Karibuni Dunia nzima siku hizi wanatumia Electronic Single Window System.Hii baada ya kuagiza gari au bidhaa zingine muuzaji utuma invoice copy tokea ofcn kwake kwenda kwa wahusika wote kuanzia custom,watu wa vibari na meli.Pia Automatically copy utumwa Kwenye idara ya forodha ya nchi inapoenda mzigo,Mfano ikifika TRA Tanzania ,system itatuma pia hiyo invoice TBS,TDFA, n.k ...hapa mteja awezi ongopa bei kwani copy anatuma alieuza mzigo.Sasa hapa Tanzania ukweli wateja wanafoji Invoices na ana kuwa na copy ya kupeleka TRA ,copy ya TBS,Copy ya TAEC ili aweze lipa fees na kodi chini ya kiwango.
Dawa ya kuondokana na hili Tatizo hapa Tanzania ni Electronic Single Window System. Akuna mbadala na aliepukiki.,Rwanda,Kenya,Uganda,Zambi kote wanatumia EWS
Ndo maana huko vitu bei chini,wabongo Kwa ubunifu uwawezi upiga transit kisha ikifika kule uingizwa kimagendo nchini pia.
 
Kama hawaziamini documents zetu TRA wawe madalali basi wawe wanaleta mizigo tununue kwao,maana wao ndo wanazijua bei,maana tukija na invoice zetu hawaziamini,wanataka za kwao sasa kuna haja gani ya kuagiza mzigo wakati wao ndo ujua bei. Nchi zote zinazotuzunguka hawana shida na invoice toka Kwa mnunuzi ndo kusema sisi ni smart sana,kama tunapika data,una kifaa kipi kujua hii data halisi hii siyo,mifumo yao ndo inawafundisha watu kukwepa kodi,mizigo haipiti bandarini kodi kubwa lkn utakuta imejaa mitaani,inapita wapi njia za panya,kodi kubwa makusanyo haba,si wangefanya kama nchi za majirani zetu kodi nafuu makusanyo makubwa,pia wameisingle,na uoni ulazima wa kuikwepa sababu inalipika.Labda kama ni tools ya kuwafanya wengi waishi kama mashetani hapo sawa.
umeongea cha maana sana
 
Karibuni Dunia nzima siku hizi wanatumia Electronic Single Window System.Hii baada ya kuagiza gari au bidhaa zingine muuzaji utuma invoice copy tokea ofcn kwake kwenda kwa wahusika wote kuanzia custom,watu wa vibari na meli.Pia Automatically copy utumwa Kwenye idara ya forodha ya nchi inapoenda mzigo,Mfano ikifika TRA Tanzania ,system itatuma pia hiyo invoice TBS,TDFA, n.k ...hapa mteja awezi ongopa bei kwani copy anatuma alieuza mzigo.Sasa hapa Tanzania ukweli wateja wanafoji Invoices na ana kuwa na copy ya kupeleka TRA ,copy ya TBS,Copy ya TAEC ili aweze lipa fees na kodi chini ya kiwango.
Dawa ya kuondokana na hili Tatizo hapa Tanzania ni Electronic Single Window System. Akuna mbadala na aliepukiki.,Rwanda,Kenya,Uganda,Zambi kote wanatumia EWS
Hakuna anayefoji invoice tz hilo nimeliona mwenyewe wakati nanunua gari invoice yangu ni origin toka japan lakini TRA wamekuja na ya kwao.ambayo iko juu sikuwa na jinsi zaidi ya kulipa tu na kutoa gari.

Hiyo system unayosema ingekuwa busara zaidi kwa TRA kupata huo ukweli ili wale wote ambayo ni waaminifu waweze kunufaika na huo utaratibu wa EWS.
 
Kumekuwa na malalamiko kila kukicha kwa TRA pale Bandarini kutoka kwa wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi kuhusu kupandishiwa bei ya kununuliwa biadhaa huko nje kwa kisingizio kuwa wao TRA wanautaratibu wao wa kukadiria bei za bidhaa yaani assesment price kulingana na sheria inavyowataka yaani bei ya soko.

TRA wamekuwa wakiwakadiria bei za juu sana wafanyabiashara wanaotoa mizigo kupitia bandari zetu kiasi cha wengine kuhama bandari ni kuhamia Mombasa ili kupata unafuu wa baadhi ya kodi.

Nakumbuka hata niliponunua gari toka Japan ile invoice iliyotumwa toka Japan TRA walikataa wakatoa bei yao ambayo ilikuwa juu ili tu nilipe kodi ya juu na hilo ni tatizo kubwa kiasi kwamba kuna watu wengine wanatelekeza magari yao hapo bandarini.

Na mfano wa jana yule mama wa kutoka Dodoma anayezalisha mvinyo wa Dodoma kwa zabibu alilalamika mbele ya Rais kuhusu kontena la chupa kukwama bandarini kisa kapandishiwa bei ya kununua hizo chupa za kujazia mvinyo yaani Dododma wine na Rais aliamuru huyo mama alipe kodi kutokana na invoice yake inavyosema na leo kontena liwe limetoka bandarini.

Maafisa wa TRA mmekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya watanzania kwa kuwapa kodi za juu na ndiyo maana jana malalamiko mengi yalikuwa kuhusu kodi.

Nakumbuka kulikuwa kuna kontena la dawa na vifaa vya hospitali ya Kahama kutoka Canada mwaka jana kwa wafadhili tu wa msaada wa huduma za kijamii lakini hilo kontena lilikaa bandarini zaidi ya miezi 3 na kiasi cha wale wafadhali kuacha kuleta misaada tena ya huduma za afya Kahama kutokana na kulipia gharama kubwa sana kutokana na sababu zisizo na tija kwa taifa kwa baadhi ya maofisa wa TRA.

TRA fuateni maagizo ya Rais na pia muwaamini wafanyabiashara kwa invoice zao siyo mnaongeza bei wakati sio TRA mlionunua hizo bidhaa.
Hawa wanatak serikal ichukiwe na wananchi wake!!! Sasa cha kufany fukuza yoote waajiriwe wengne ili waache kujiona wao ndo wao
 
Hakuna anayefoji invoice tz hilo nimeliona mwenyewe wakati nanunua gari invoice yangu ni origin toka japan lakini TRA wamekuja na ya kwao.ambayo iko juu sikuwa na jinsi zaidi ya kulipa tu na kutoa gari.

Hiyo system unayosema ingekuwa busara zaidi kwa TRA kupata huo ukweli ili wale wote ambayo ni waaminifu waweze kunufaika na huo utaratibu wa EWS.
Nasema TRA wao ndo uchangia watu kukwepa kodi, Kwa sababu ya makadirio yasioakisi invoice ya kununulia mizigo,matokeo yake kodi hawapati na mizigo still inaingizwa kwa njia za panya,watu wanashushia nchi za Jirani au transit mfano Rwanda mzigo utatoka Kwa haraka then inarudishwa nchini Kwa njia ya panya,inasaidia nn sasa,kodi wamekosa na still mzigo umejaa nchini.
 
TRA ni tatizo kubwa la biashara katika nchi hii! Mentality yao ni kwamba wanawachukulia wafanyabiashara wote kua ni wezi na wakwepa kodi! Kwa mindset hiyo wameua biashara ya nguo na wameua biashara ya vipuri vya magari kama ambavyo watakuja kuua biashara ya vifaa vya ujenzi. Unapowaletea Invoice ya bidhaa ulizoingiza nchini ni mara chache sana wakaipitisha kama ilivyo labda waone mabei makubwa sana
Unaweza kuingiza nchini container la vipuri vya magari ambalo mara ya mwisho ulilipia 15-18Mil next time the same consignment with the same quantity and value ukatakiwa ulipie 35-40mil! NA ukiwapa reference wanakwambia kila shipment ina historia yake, yaani hakuna consistence,

na ukishindwa mzigo wako unapigwa mnada. Hii taasisi ni changamoto kwa biashara kwakweli
Ila wewe bei ikiwa ndogo wanakupa reference yao hutawasikia wakikubali kila shipment ina historia yake.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom