Candela
JF-Expert Member
- Aug 12, 2021
- 647
- 1,717
Wadau kuna kitu hakipo sawa.
Suala la TRA kukadilia kodi kwa kuangalia mtaji wako pamoja na unalipa pango kiasi gani kwenye biashara yako sio sawa.
Chukulia una mtaji wa milioni 10, na kodi unalipa milion 3.6 kwa mwaka. Kimsingi hii hela ya kodi inatakiwa itoke kwenye faida ya biashara lakini cha ajabu ukienda TRA wanakukadilia kodi kwa mtaji wa milioni 13.6 na sio milioni 10. Sasa pango halizalishi chochote yaani sipati faida kwa kulipa kodi ya pango, faida inapatikana kwenye biashara yangu lakini natakiwa nitoe % ya pango kama kodi. Kwa nini hii wasimdai mwenye frame na sio mfanya biashara?
Hebu wajuzi mje na ujuzi tufunguane pengine mie ndio nimeingizwa cha kike.