TRA kukadiria hadi pango sielewi

Candela

JF-Expert Member
Aug 12, 2021
628
1,644
Wadau kuna kitu hakipo sawa.

Suala la TRA kukadilia kodi kwa kuangalia mtaji wako pamoja na unalipa pango kiasi gani kwenye biashara yako sio sawa.

Chukulia una mtaji wa milioni 10, na kodi unalipa milion 3.6 kwa mwaka. Kimsingi hii hela ya kodi inatakiwa itoke kwenye faida ya biashara lakini cha ajabu ukienda TRA wanakukadilia kodi kwa mtaji wa milioni 13.6 na sio milioni 10. Sasa pango halizalishi chochote yaani sipati faida kwa kulipa kodi ya pango, faida inapatikana kwenye biashara yangu lakini natakiwa nitoe % ya pango kama kodi. Kwa nini hii wasimdai mwenye frame na sio mfanya biashara?

Hebu wajuzi mje na ujuzi tufunguane pengine mie ndio nimeingizwa cha kike.
 
Withholding rental tax

Imeendelea kuumiza walipakodi kwa miaka nenda rudi. TRA wanatambua kua ni kodi ya landlord, sera yao ni kua wewe unayemlipa hela ya kodi uzuie (withholding) kiasi hicho cha kodi upeleke TRA.

Ama ulipe TRA mwanzoni halafu wakati unamlipa landlord umkate.
Landlord anasema, nataka hela yangu kamili, kama unataka kukata hiyo ondoka aingie anayelipa full.

TRA wanajua hili, na wameshindwa kukusanya hii kodi kutoka kwa landlord, wameamua kumtwisha mzigo taxpayer.
Who cares.
 
Unamaanisha walikuuliza mtaji wako ni kiasi gani ukasema milioni 10? Wakakuuliza Kodi ya pango unalipia kiasi gani ukasema unalipia laki 3 kwa mwezi?. Unakuwa honest na TRA unadhani wale Ni wajomba zako? Unaogopa kupata dhambi ya kuwadanganya? Kwa staili hiyo lazima wakulime Kodi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom