TRA Kodi za Wananchi ni Maisha ya Viongozi?

TRA Kodi za Wananchi ni Maisha ya Viongozi?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Tanzania Revenue Authority (TRA), taasisi iliyoundwa rasmi mwaka 1995 kwa madhumuni ya kukusanya mapato ya serikali, leo hii inakabiliwa na lawama nzito kutoka kwa wananchi wanaohoji uhalisia wa mchango wake katika kuboresha maisha ya Watanzania wa kawaida. Wapo wanaosema kuwa mfumo huu wa ukusanyaji kodi umegeuka kuwa chombo cha kulisha matumbo ya wachache walioko madarakani badala ya kuendeleza taifa zima.
images (41).jpeg

Hali hii inatupa picha tata, hasa tukikumbuka enzi za ukoloni ambapo, licha ya unyonyaji uliokuwepo, mfumo wa kodi ulilenga pia kutoa huduma fulani kwa wananchi. Wakati huo, sehemu ya mapato ilielekezwa kwenye miundombinu, huduma za afya, elimu, na usalama wa jamii, ili kudumisha maslahi ya wakoloni lakini pia kuimarisha mazingira ya kazi na maisha kwa Waafrika waliokuwa wakihitajika kwenye mfumo wao wa uzalishaji.
images (42).jpeg

Hali halisi inaonesha kuwa hakuna uwiano kati ya mapato makubwa yanayokusanywa na hali halisi ya maisha ya wananchi kwani ni mdogo mno. Kila mwaka, ripoti zinaonyesha kuwa mabilioni ya shilingi hukusanywa, lakini barabara za vijijini zinabaki kuwa mashimo, zahanati hazina dawa, na walimu wa shule za msingi na sekondari wanakosa vifaa muhimu vya kufundishia. Je hizo pesa ndio zinaenda kulipa goli la mama kwenye mechi za Simba na Yanga? Ama kupiga kampeni za CCM?
images (43).jpeg

Chanzo mbalimbali vimeonesha wazi kuwa baadhi ya mapato hukwama katika mifumo ya matumizi kwa sababu ya “masharti ya juu” kutoka kwa viongozi wakuu wa serikali. Kwa maneno mepesi, miradi inayopewa kipaumbele si ile inayohitajika zaidi na wananchi, bali ile inayoweka alama za kisiasa au maslahi ya kifedha kwa watu fulani.
images (41).jpeg

TRA mara nyingi huelekeza nguvu kwa wafanyabiashara wadogo, mama lishe, na wajasiriamali wa mitaani huku mianya ya ukwepaji kodi inayotumiwa na kampuni kubwa ikibaki wazi. Hii imesababisha hisia kuwa taasisi hii ni “simba kwa wanyonge na paka kwa wakubwa.”
images (44).jpeg

Wakati wa ukoloni, mfumo wa kodi, licha ya kuwa na lengo la kunufaisha wakoloni, ulijumuisha miradi inayotoa faida za moja kwa moja kwa wananchi kama *shule, hospitali, na barabara. Leo, mfumo wetu wa ndani umeshindwa hata kufikia kiwango hicho cha matokeo, jambo linalowashangaza wachambuzi wa historia na uchumi. Kujenga matundu ya vyoo ni kazi ambayo inasubiria mbio za mwenge? SHAME ON YOU!
images (45).jpeg

Sasa hivi mnataka mpaka Mawionga walipe kodi? Serious? Walipe kodi kwenye kuuza bidhaa ambazo zimekwisha kulipiwa kodi? Yaani ni sawa na kununua vocha ya 1000 kisha ulipe kodi ya pili kabla ya kuweka salio.
images (42).jpeg

TRA mko kwenye nafasi ya kuwa injini ya maendeleo ya Tanzania, lakini bila mageuzi ya kweli katika uwazi, usawa, na uwajibikaji, itaendelea kukumbwa na lawama na kupoteza uhalali wake wa kimaadili.
 
Hapo unailaumu bure tu. Yeye ashamaliza kazi yake ya kukusanya Kodi kikamilifu. Jinsi ya kutumia hayo makusanyo waulizwe viongozi wako.
Wamenunua Timu ya mpira ili kuongeza elimu ya ulipaji kodi
 
Back
Top Bottom