TRA, kansa inayoimaliza bandari ya Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA, kansa inayoimaliza bandari ya Dar es Salaam

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kwayu, Jan 10, 2012.

 1. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ufanisi ktk bandari ya dar es salaam unategemea sana efficient ya TRA. Mamlaka hii imekuwa ni kikwazo kikubwa kwani imegubikwa na rushwa ktk kila idara.Mfano kwa documents za transit unapozi lod kwenye system yao ya asy scan huchukua mpaka wiki kwa wao tra kuifanyia kazi hasa hasa kwenye department kama documentary na error management. ili documents zako zifanyiwe kazi inakupasa kutoa rushwa ya sh. 20,000 kwa kila documents. ninawaomba taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa walimulike hili swala kwa umakini. pia serikali itambue kwamba kuna trend kubwa sana ya wateja waliokuwa wakitumia banadari yetu hii wanaamia bandari za waivers bay (namibia) darbun (sa), mombasa na mozambique. gharama za kulipia mizigo zimekuwa ni kubwa sana haswa pale mteja anapochelewa kutoa mzigo wake ndani ya siku 14( kwa mizigo ya transit) mfano baada ya cku 14 wanaanza ku charge cutomer warehouse rent ambayao cku za nyuma kama miezi 2 hivi nyuma walikuwa wakicharge baada ya cku 21, hii ni tofauti kabisa na gharama za storage na removal charges. Ukiritimba, ubinafsi na rushwa vinavyofanywa na tra, pta pamoja na watoa huduma za meli ndizo sababu za kuzorota kwa bandari yetu.
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Sasa unamuambia nani?? hebu ondoka zako hapa kwani TZ ina uongozi? Unategemea ufanisi chini ya Kikwette? Tushirikiane katika maombi ipo siku Tanzania itapata viongozi wenye nia ya kutuondoa Watanzania hapa tulipo. Wee kiongozi anaomba kwenda Ikulu kwa gia ya maisha bora kwa kila Mtanzania na unashoboka kumpigia kura, hivi kuna nchi imefanikiwa kufanya maisha bora kwa kila mwananchi wake? Uongo wa namna hii mimi niliushtukia na sijawahi kumpigia kura aombe Mungu kuna Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyo chini yake na katiba inayokataza kuhoji namna alivyoshinda.
   
 3. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Suala la rushwa sio tatizo la TRA peke yake, ni la nchi nzima.

  Tatizo ni kwamba rushwa inapofanyika mahala nyeti kama bandarini watu wanakuja juu. Rushwa ipo mahospitalini, mashuleni, wizarani, bandarini, mahakamani polisi n.k. Wapi hakuna rushwa bongo? Siku hizi hata kwenye nyumba za ibada wenye pesa ndio watu wa maana.

  Kwa bahati mbaya Tanzania ndio imeshapoteza dira. Kiongozi wetu 'handsome' ndo hivyo tena nayeye anapelekwa shopping ananunuliwa suti anagawa rasilimali za nchi. Hivi kweli unategemea rushwa itaisha? TAKUKURU unadhani hawapokei rushwa?

  Ukombozi wa Tanzania upo mikononi mwa watanzania wenyewe. Lakini kama tusipoweka ubinafsi pembeni na kujenga nguvu katika umoja, viongozi wote watakaoingia madarakani watakuwa ni viongozi wa vijisent.
   
 4. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  TRA- nadhani unamaanisha, Tanzania Revenue Authority. Malalamiko nadhani yamekithiri, hasa ukizingatia kwambo sasa biashara inahamia kwingine na watu wakosa kazi kwa ajili yao. Ingawa nchi inakaribisha investors (wawekezaji) na kuinua private sector (wajasirimali), Hali hii inafanya ugum kufikia hilo lengo la serikali.

  Hawa TRA ndio wanaujuzi wa kudhibiti rushwa. na wajua kufanya Audit. kwa kiwastani ni Accountants wa serikali. Kwa hiyo, wanajua vizuri namna kudhibiti huu ufisadi na dhuluma. Kazi ya bandarini ya customs, nadhani walipewa ili kuzidisha ufanisi wa bandari na kuondoa ufisadi. Wanajua vema namna ya kusimamisha kwa sababu hii ni fani yao na wanajua hiyo siku inakuja. Aidha italetwa na wananchi au TRA inaweza kupata kiongozi muadilifu, basi mara moja atasafisha. Malaamiko yawe Contractive. Yani kuwepo na ushahidi wa makaratasi wa kusapoti madai kama haya ya ACTIVIST. Viongozi wa juu hutaka ushahidi ili wawajibike. Na wasipo wajibika mbele ya ushahidi, nikwenda juu zaidi.

  Wanainchi wakitaka kuondoa Dhuluma na ufisadi Bandarini, watafanikiwa. Hii ni nchi ya kidemokrasia, wakuu. Tusisahau.
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Unapoona miji inavyokia kwa ajili ya kuwa na bandari tu unashangaa kwanini bandari ya dar haikuzi uchumi na muonekano wa mji huo. Dar iko pale kwa ajili ya bandari. Dar itajengwa na bandari. Kama mie ningekuwa meya wa dar ningekuwa na ofisi pale kwenye bandari, kwani ndio kinatakiwa kiwe kitegauchumi kikubwa kabisa cha kuujenga mji, ningekuwa focused, ningewakaba wote wanaoivuruga na ningehakikisha process yote inakuwa inaboreshwa mara kwa mara kukidhi matakwa ya wateja hasa wa transit., mgao wa mkoa kutoka serikali kuuu ningehakikisha unaleta matunda mjini kama migodi huko shinyanga.
  Wangenniua?
  Investments nyingine zingeendelea tu as long as bandari iko juu.
  Dar ni mji wa bandari, kama kahama ulivyo mji wa migodi, moshi mji wa ml kilimanjaro, arusha tanzanite, mwanza samaki.
   
 6. n

  namimih Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekubali sana ulichoeleza, ila kama huyo mkuu wa mkoa atakuwa kweli ana nia ya kuepuka hicho kitu kidogo, vinginevyo inaweza kuwa yeye akawa na watu wake wa kuchukua mlungula na hali ikarudi pale pale tu. Nadhani nchi yetu inahitaji somo la uzalendo wa nchi kwa wananchi na viongozi wote kwa ujumla, kwani inawezekana tatizo letu watanzania hatuna hisia ya nchi yetu. NI maoni tu.
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ulichosema ni sahihi. Tatizo liko kwetu wananchi wote. Tukiona kijana kaanza kazi na baada ya mwaka moja tu kajenga bonge la nyumba na kununua gari la fahari tunamsifia! Hapo si wote tunahamasiha rushwa?
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sio sisi tu tunaomsifia, hata mkuu wa nchi ameshawahi kusema kuwa ongezeko la magari barabarani ni moja ya ishara za utajiri wa tanzania
   
 9. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kumbe TRA kima rushwa kiasi hicho! Sasa nimeona ni kwa nini wananchi wa kabila moja wamejazana hapo kuanzia Mkurugenzi Mkuu hadi dereva
   
 10. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wamasai eeh? Duh wamasai noma, wanajua kutega penye hela
   
 11. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Rafiki yangu mimi ni mzalendo kama wewe na nimewahi kukereka na hili suala la hali ya rushwa ilivyo nchi hii mpaka basi. Tena ukijaribu kuonyesha kuwa uanachukizwa na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma ukiwa ndani ya utumishi wa umma wa tanzania system nzima inakuchukia angalia walichomfanyia DCG wa TRA hakika ameondolewa kwa sababu ya kuchukia kwake rushwa na kuwashughulikia ipasavyo wala rushwa ndani ya TRA . tufunge na kusali SOKOINE au NYERERE warudi vinginevyo hali hii ni ya kudumu na tuishi nayo kwa matumaini kama mgonjwa wa ukimwi anavyoishi na virusi vyake... PERIOD
   
 12. K

  Kwameh JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 482
  Trophy Points: 80
  Hivi ukiingiza mzigo kama vile gari kupitia bandari ya Kenya, kama Mombasa na ukalipa fees and kodis zote zinazotakiwa je ukifika mpakani Horohoro (nadhani) inakuwaje, unaanza upya na makodi na malipo? Kwa hiyo unaishia kulipa tariff za Kenya na Bongo au Kenya itakuwa bure??? Na kutoka Kenya mpaka Bongo utaliendesha kwa plate numbers gani, Kenya wanatoa temporary registration plates? Au itabidi ulibebe kwenye flat bed mpaka Bongo?
   
 13. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Bado ukiingia bongo TRA watakubana ulipie kodi za TZ...
   
 14. H

  Haika JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa mimi Rais, ningetoa amri kuwa wafanya biashara wote wa transit wawe treated kama watalii, yani kwa heshima na ukarimu mpaka wawe wanaona raha kupfanya kazi na bandari yetu.
   
 15. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  TRA ni ovyo kabisa
   
 16. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, Kwa mfano bidhaa kama magari sasa hivi zinatozwa kodi kubwa sana, bora kama hiyo kodi ingekuwa inajenga nchi, lakini hizo hela zinaishia kwenye matumbo ya watu.
   
 17. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  kazi kwenu
   
 18. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  nyie mnayoongea ni kweli au ndio kawaida yenu watanzania kila siku kulalamika
   
 19. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  wewe mtoa thread unahoja yako nyingine si bure!
   
 20. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  sasa ndugu ilo kabila moja si ndo wamesoma peke yao hapa tz,inaelekea we jamaa ni mgogo au mzaramo kama mimi!
   
Loading...