TOZO|CORONA: Idadi ya watali nchini imepungua kwa 77%, Mapato yatokanayo na utali yameshuka kwa 87%, Je mnaopinga tozo hadi leo mnalijua hili?

Hakukuwa na akiba yoyote ya maana, kwani dhalimu alikuwa ameshachota yote na kupeleka kwenye miradi ya kusaka sifa za kisiasa.
i Gaknchi gani inayo jiendesha bila akiba?

Akiba inakazi gani kama kwenye nyakati za emergency kama hizi hhaitumikigakuki
 
HII NCHI NGUMU SANA|WATU WANAPINGA TOZO ZA HIARI WANATAMANI ENZI ZA TRA NA MITUTU YA BUNDUKI,



_________________________________

Kazi iendelee|Tozo ziendelee

Sikilizeni, Mfano, kutoka Wizara ya Maliasili & Utalii FY2021/22 tulitegemea kukusanya jumla ya Tshs 2.7trl kama mapato yatokanayo na Utali kwa matarajio ya kupokea jumla ya watali 1,867,000 but kutokana na COVID-19 tunatarajia kupokea watalii 437,000 sawa na anguko la 77%,na matarajio mapya ya makusanyo ni Tshs 598BL kwa mwaka toka matarajio ya Tshs 2.7trl hii ni sawa na nakisi|pungufu wa Tsh 2.102trl kwa mwaka huu. Wananzengo, hii pesa ya kufidia tunaipataje?

Tukumbushane, Kabla ya Corona kwa mfano, FY 2017/18 mapato yatokanayo na Utali tu yalifikia kiasi cha US$ 2.4BL sawa na Tshs 5.3trl leo Mapato hayohayo ni chini ya Tshs 598BL sawa na anguko la 87% ambayo ni Tsh 4.702trl. Kwa lugha rahisi zaidi ya Tshs 4.7trl tulizopata miaka ya 2010's zitokanazo na Utali zimeyeyushwa na Corona na hazipo tena Serikalini wala kwenye mzunguko,Kumbuka hii Corona si ya CCM, CHADEMA, NCCR, CUF wala TLP ni Ya Mungu na Mungu hakosei, Hii pesa tunaipataje?

Dk Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha na Mipango amesema Serikali ya JMT imekusanya Tshs 48.4BL kwa mwezi moja tu ( wiki nne ) toka kwenye tozo,Kama tozo hizi tulio wengi tutazikubali basi kwa mwaka mmoja wa fedha tutakusanya jumla ya Tshs 581BL ambazo ni zaidi ya hata makusanyo yote ya Wizara ya madini ambayoni ni Tshs 528.24BL kwa mwaka, kwamiaka hii mitano ya Kwanza ya Mama Samia kwa tozo za miamala tu, tutakusanya zaidi ya 3trl kama wapinga maendeleo wa hii nchi hawatashinda hii Vita ya Ujenzi wa nchi bila kumdhulumu yeyote awaye.

Pamoja na Corona, Vituo vya afya 560, Ukarabati wa Hospitali za wilaya 99, Wodi za wagonjwa 201, Vyumba vya madarasa 10,000, Zahanati 1,198, Kilometa 73,242 za Changarawe yote haya lazima yajengwe na njia ni mbili tu, niama TRA wachukue Mitutu ya bunduki wakawatengenezee wafanyabiashara wetu "Presumtive Tax accessment" ili kuwadai kodi hadi za wakati wa JK au Watanzania wote zaidi ya 60M kwa umoja wetu tu-share baraka hizi kwa kuchangia miamia zetu kwenye miamala na tozo nyinginezo zilizopitishwa na bunge ili kuifanya Tanzania kuwa nchi salama kwa yeyote kuishi iwe ni kijijini au mjini,


...tuendelee kumwombea Mama kazi anaipiga ...





" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
 
Baba Askofu Benson Lwakalinda Bagonza anauliza

NAOMBA MSAADA

Nahitaji msaada wenu wasomaji wangu:

1. Hivi mwizi akikuibia hela yako halafu akaitumia kukununulia nguo au chakula, kosa la wizi linakuwa limeisha?

2. Mwizi akikuibia shilingi 100 ukapiga kelele akakurudishia 30 na kubaki na 70, unapaswa kumshukuru kuwa ni mwema?

3. Na kiongozi wako akikukuta unafanya biashara ili upate fedha ya kulipia karo na matibabu, akafunga biashara yako na hela akakunyanganya na kukujengea zahanati na shule, anakuwa amekutendea haki?

TOZO TOZO
LUKU LUKU

VYOTE NI KANDAMIZI. HATULIPI KWA HIARI BALI MNACHUKUA KWA NGUVU. MIILI YETU MNAYO, MIOYO TUMEBAKI NAYO.
 
Baba Askofu Benson Lwakalinda Bagonza anauliza

NAOMBA MSAADA

Nahitaji msaada wenu wasomaji wangu:

1. Hivi mwizi akikuibia hela yako halafu akaitumia kukununulia nguo au chakula, kosa la wizi linakuwa limeisha?

2. Mwizi akikuibia shilingi 100 ukapiga kelele akakurudishia 30 na kubaki na 70, unapaswa kumshukuru kuwa ni mwema?

3. Na kiongozi wako akikukuta unafanya biashara ili upate fedha ya kulipia karo na matibabu, akafunga biashara yako na hela akakunyanganya na kukujengea zahanati na shule, anakuwa amekutendea haki?

TOZO TOZO
LUKU LUKU

VYOTE NI KANDAMIZI. HATULIPI KWA HIARI BALI MNACHUKUA KWA NGUVU. MIILI YETU MNAYO, MIOYO TUMEBAKI NAYO.
Jibu ni moja tu huo wote ni wizi tu
 
Pamoja na upungufu mkubwa hivyo wa mapato uliosababishwa na ugonjwa wa Corona mbona serikali haipunguzi matumizi yasiyo ya lazima. Hizo V8 zinatumia mafuta kiasi gani kwa siku nchi nzima? Misafara mikubwa ya viongozi wa kisiasa kwa pesa za serikali je? Rais inatakiwa aongoze kwa mfano kwa kukubali nae alipe kodi kwenye mapato yake ya mshahara nk.
Hawa jamaa ilibidi wapewe hela fixed ya mafuta ndani ya mwezi maybe 2M basi ikiisha hio kila mtu apambane na hali yake.
 
Back
Top Bottom