TOZO|CORONA: Idadi ya watali nchini imepungua kwa 77%, Mapato yatokanayo na utali yameshuka kwa 87%, Je mnaopinga tozo hadi leo mnalijua hili?

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,450
799
HII NCHI NGUMU SANA|WATU WANAPINGA TOZO ZA HIARI WANATAMANI ENZI ZA TRA NA MITUTU YA BUNDUKI,



_________________________________

Kazi iendelee|Tozo ziendelee

Sikilizeni, Mfano, kutoka Wizara ya Maliasili & Utalii FY2021/22 tulitegemea kukusanya jumla ya Tshs 2.7trl kama mapato yatokanayo na Utali kwa matarajio ya kupokea jumla ya watali 1,867,000 but kutokana na COVID-19 tunatarajia kupokea watalii 437,000 sawa na anguko la 77%,na matarajio mapya ya makusanyo ni Tshs 598BL kwa mwaka toka matarajio ya Tshs 2.7trl hii ni sawa na nakisi|pungufu wa Tsh 2.102trl kwa mwaka huu. Wananzengo, hii pesa ya kufidia tunaipataje?

Tukumbushane, Kabla ya Corona kwa mfano, FY 2017/18 mapato yatokanayo na Utali tu yalifikia kiasi cha US$ 2.4BL sawa na Tshs 5.3trl leo Mapato hayohayo ni chini ya Tshs 598BL sawa na anguko la 87% ambayo ni Tsh 4.702trl. Kwa lugha rahisi zaidi ya Tshs 4.7trl tulizopata miaka ya 2010's zitokanazo na Utali zimeyeyushwa na Corona na hazipo tena Serikalini wala kwenye mzunguko,Kumbuka hii Corona si ya CCM, CHADEMA, NCCR, CUF wala TLP ni Ya Mungu na Mungu hakosei, Hii pesa tunaipataje?

Dk Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha na Mipango amesema Serikali ya JMT imekusanya Tshs 48.4BL kwa mwezi moja tu ( wiki nne ) toka kwenye tozo,Kama tozo hizi tulio wengi tutazikubali basi kwa mwaka mmoja wa fedha tutakusanya jumla ya Tshs 581BL ambazo ni zaidi ya hata makusanyo yote ya Wizara ya madini ambayoni ni Tshs 528.24BL kwa mwaka, kwamiaka hii mitano ya Kwanza ya Mama Samia kwa tozo za miamala tu, tutakusanya zaidi ya 3trl kama wapinga maendeleo wa hii nchi hawatashinda hii Vita ya Ujenzi wa nchi bila kumdhulumu yeyote awaye.

Pamoja na Corona, Vituo vya afya 560, Ukarabati wa Hospitali za wilaya 99, Wodi za wagonjwa 201, Vyumba vya madarasa 10,000, Zahanati 1,198, Kilometa 73,242 za Changarawe yote haya lazima yajengwe na njia ni mbili tu, niama TRA wachukue Mitutu ya bunduki wakawatengenezee wafanyabiashara wetu "Presumtive Tax accessment" ili kuwadai kodi hadi za wakati wa JK au Watanzania wote zaidi ya 60M kwa umoja wetu tu-share baraka hizi kwa kuchangia miamia zetu kwenye miamala na tozo nyinginezo zilizopitishwa na bunge ili kuifanya Tanzania kuwa nchi salama kwa yeyote kuishi iwe ni kijijini au mjini,


...tuendelee kumwombea Mama kazi anaipiga ...
 
HII NCHI NGUMU SANA|WATU WANAPINGA TOZO ZA HIARI WANATAMANI ENZI ZA TRA NA MITUTU YA BUNDUKI,



_________________________________

Kazi iendelee|Tozo ziendelee

Sikilizeni,Mfano,kutoka Wizara ya Maliasili & Utalii FY2021/22 tulitegemea kukusanya jumla ya Tshs 2.7trl kama mapato yatokanayo na Utali kwa matarajio ya kupokea jumla ya watali 1,867,000 but kutokana na COVID-19 tunatarajia kupokea watalii 437,000 sawa na anguko la 77%,na matarajio mapya ya makusanyo ni Tshs 598BL kwa mwaka toka matarajio ya Tshs 2.7trl hii ni sawa na nakisi|pungufu wa Tsh 2.102trl kwa mwaka huu,Wananzengo,hii pesa ya kufidia tunaipataje?

Tukumbushane,Kabla ya Corona kwa mfano,FY 2017/18 mapato yatokanayo na Utali tu yalifikia kiasi cha US$ 2.4BL sawa na Tshs 5.3trl leo Mapato hayohayo ni chini ya Tshs 598BL sawa na anguko la 87% ambayo ni Tsh 4.702trl,Kwa lugha rahisi zaidi ya Tshs 4.7trl tulizopata miaka ya 2010's zitokanazo na Utali zimeyeyushwa na Corona na hazipo tena Serikalini wala kwenye mzunguko,Kumbuka hii Corona si ya CCM,CHADEMA,NCCR,CUF wala TLP ni Ya Mungu na Mungu hakosei,Hii pesa tunaipataje?

Dk Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha na Mipango amesema Serikali ya JMT imekusanya Tshs 48.4BL kwa mwezi moja tu ( wiki nne ) toka kwenye tozo,Kama tozo hizi tulio wengi tutazikubali basi kwa mwaka mmoja wa fedha tutakusanya jumla ya Tshs 581BL ambazo ni zaidi ya hata makusanyo yote ya Wizara ya madini ambayoni ni Tshs 528.24BL kwa mwaka,kwamiaka hii mitano ya Kwanza ya Mama Samia kwa tozo za miamala tu, tutakusanya zaidi ya 3trl kama wapinga maendeleo wa hii nchi hawatashinda hii Vita ya Ujenzi wa nchi bila kumdhulumu yeyote awaye.

Pamoja na Corona,Vituo vya afya 560,Ukarabati wa Hospitali za wilaya 99,Wodi za wagonjwa 201,Vyumba vya madarasa 10,000,Zahanati 1,198,Kilometa73,242 za Changarawe yote haya lazima yajengwe na njia ni mbili tu,niama TRA wachukue Mitutu ya bunduki wakawatengenezee wafanyabiashara wetu "Presumtive Tax accessment" ili kuwadai kodi hadi za wakati wa JK au Watanzania wote zaidi ya 60M kwa umoja wetu tu-share baraka hizi kwa kuchangia miamia zetu kwenye miamala na tozo nyinginezo zilizopitishwa na bunge ili kuifanya Tanzania kuwa nchi salama kwa yeyote kuishi iwe ni kijijini au mjini,


...tuendelee kumwombea Mama kazi anaipiga ...
😏
 
Daaah,


Shida kubwa serikali ya awamu ya Sita ni Taarifa,

Mimi nilikuwa nimemchukia Samia kwenye tozo bure kumbe Mama anahangaika kuinusuru nchi kimaendeleo,

Mbona msemaji wa Serikali hatokei kufafanua kama huyu member,

Mbona waziri hatokei kufafanua hili anakimbilia kutuambia tuvumilie au tuhame,

Kunaubaya gani kuwaambia wananchi hizi taarifa kuwa wafunge mikanda wakati huu wa CORONA?

Wanaogopa kwani CORONA imeletwa na CCM?

Hata kama wangekuwa Chadema wao wangepata wapi hiyo pungufu ya 4T kwa mwaka?

Mama kama utapitia huu uzienajua unasoma jaribu kuwatoa watu wako waje waisemee serikali watu hawana Taarifa zakutosha,

SASA NIMETAMBUA KWANINI TOZO,

NAUNGA MKONO HOJA TOZO IENDELEE KIROHO SAFI KABISA,
 
Kama hilo wanaliona, kwa nini wananchi pekee ndio wanaofunga mkanda kwa kutoa kodi ili serikali iendeshe mambo yake vema, halafu wao kila leo ni safari tuu!! mara semina na posho za ajabuajabu!!

Serikali ikisema tufunge mkanda, basi ianzie kwao, misafara ipungizwe, semina zikatizwe, safari ziachwe, hapo tutasogea
 
Hivi kipindi kile tunapiga nyungu "kama hatuna akili nzuri"/ sana idadi ya watalii ilipungua ama iliongezeka!?
 
Kwani nchi gani inayo jiendesha bila akiba?

Akiba inakazi gani kama kwenye nyakati za emergency kama hizi haitumiki
 
Sasa tule nyasi ama???
Mpaka umeweza kuweka umeme maana yake wewe upo njema, imagine unabundle la kusurf kila uzi una comment na hii ni JamiiForums pekee sijui huko Twitter na IG….
Masikini wa kiukweli kweli hizi tozo na yeye ni kama ardhi na mbingu, hawakutani. Tumezaliwa maisha ya shida na majani ndio lishe yetu kuu, nyie wala kuku zamu yenu sasa kuisoma namba.
karibu chama la u-green
 
Back
Top Bottom