Toyota Land Cruiser VX ni aina mojawapo ya magari yanayojulikana kama SUV (sports utility vehicles). Kimsingi, magari ya aina hii (mengine ni kama Nissan Patrol, Toyota Surf, Toyota Prado, Mitsubishi Pajero, Land Rover Discovery, nk) hayatakiwi kuendeshwa mwendo wa kasi hata kama ni kwenye barabara nzuri kwa kuwa ni rahisi kupinduka kutokana na muundo wake wa kuwa marefu kwenda juu ikilinganishwa na upana wake (high centre of gravity). Hii inayafanya yawe "unstable" katika mwendo wa kasi. Wanaoendesha magari ya aina hii wanatakiwa kuwa makini sana katika kona na wanapokwepwa vitu barabarani wawapo katika mwendo wa kilomita 80 kwa saa au zaidi.