Samahani mkuu. Naomba unichanganulie kidogo kati ya corrolla E 111 na corrolla 110 mnayoizungumzia na ukizilinganisha na carina it ni ipi bora kwa vigezo vya ulaji mafuta,comfortability na durability.Comfort ability yake iko vizuri sana, spare zipo nyingi na bei nafuu na inaweza kuhimili mikiki ndio maana nyingi huwa wanazifanya taxi na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana na unaweza ukasafiria safari ndefu kama unaenda Arusha full tank la lita arobaini unaweza ukaenda kuongezea Same tena kidogo tu, mimi mwenyewe nina Chevrolet SUV lilinishinda kutokana na kubwia mafuta ukabidi ninunue hivi vigari vidogo nilianza na vitz baadae nikanunua corolla 110 baada ya kuona vitz haiko comfortable sana na huwa naenjoy sana kwa safari za Tanga kwani full tank naenda na kurudi
Habari za leo wanajukwaa letu pendwa!! kama heading inavyoonesha hapo juu kuhusu hayo magari tajwa. katika pita pita zangu za kusaka japo kausafiri ka kunitoa huku Chanika kwetu hadi Mikocheni, zimekuja offer mbili hadi sasa zenye bei sawa kwa hizo gari tajwa hapo juu.
zote zinaenda kwa 5.5M.
Sasa kilichonileta hapa jukwaani ni kuwa nimeshindwa kufanya maamuzi kuwa nichukue ipi kati ya hizo gari mbili, yaani hapo kigezo kikubwa ni fuel economy reasonability of the price for each na durability kati ya haya magari mawili with reference to the distance I cover daily from Chanika, Mikocheni Chanika.
Naombeni michango ya dhati jamani juu ya haya magari mawili. Natanguliza shukurani za dhati kabisa.