MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 704
Waheshimiwa!
Nilikuwa ninaperuzi (hili ni neno pia?) kwenye lile/ile tovuti ya Serikali (www.tanzania.go.tz), ambayo ninaamini inakuwa hosted na iliyokuwa Kamisheni ya Mipango (Planning Commission), kwa sasa ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango, Uchumi na Uwezeshaji... nenda kabofye www.plancom.go.tz uone kitakachotokea.
Najua kule Mipango kuna wataalam wa ICT, ambao ndio wana-update hiyo tovuti ya Serikali. Nitawasamehe, kwa kuwa wao sio walioiandaa. Inasadikika kwamba Dola za Kimarekani 50,000/= zilitumika kuiandaa tovuti hiyo, kwa mfumo uliokuwa unatumika zamani, yaani, Selective Tendering, kabla ya hii sheria ya Public Procurement kuja kuweka mambo sawia... labda?
Anyway, sikumbuki jina la kampuni iliyopewa zabuni hiyo, lakini, hata tukifanya comparison na jirani zetu wa Kenya (www.kenya.go.tz) ambao nao bado wanajikongoja, utaona mwenyewe tofauti kubwa kati ya tovuti ya Serikali ya Kenya na ile ya Serikali ya Tanzania.
Kwanza kabisa, habari mpya kutoka Ikulu (ambazo zinatakiwa kutolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi ya Rais, ikiwa ama kwenye Tovuti ya Ikulu au ya Kurugenzi yenyewe... changamoto kwa Kaka Salva...) zinapatikana SASA kwenye tovuti hii ya Serikali! Mwe! Mi si Mkaguru wala Mpogoro, lakini, Mwe!
Hiki ni kichekesho cha mwaka. Nakumbuka enzi zile za Kaka Ben, tovuti ya Ikulu ilikuwa inafanya kazi vizuri sana, na tulikuwa tunaweza hata kupata picha za Kaka Ben alipokuwa akizuru huku na kule, ndani na nje ya nchi. Leo hii nenda katafute za Kaka Jakaya, kama utazipata... kama kuna mtu anajua aniambie...
Tovuti ya Serikali ni aibu na fedheha kwa nchi yetu hii. Wakinipa kazi ya kuikarabati nitaifanya kwa robo tu ya gharama zilizotumika hapo awali! Sitanii kwa hili!
Tovuti inatakiwa kuwa na very simple HTML, wala haihitaji sijui Cascading Style Sheets, wala sijui PHP, Java, ActionScript na madudu mengine. Simple clean HTML, pamoja na cool graphics...
Mgeni akifika pale, auone UTANZANIA wetu, kwani hakuna hata picha ya Twiga pale! Hakuna! Mlima Kilimanjaro ndio usiseme! Hakuna!
Ni simple kuweka vitu sawa, lakini kwa kuwa kuna "mtoto wa shemeji yangu" au "mtoto wa mjomba wangu" ambaye anajua vizuri kazi hii ya Web design, basi ngoja nimpe yeye, aje kutusaidia...
... ndivyo walivyokuwa wakifanya?
Tathmini yangu? Hii tovuti ya Serikali ni sawa na High School Graduation Project, ya mwanafunzi yeyote katika high school yeyote, Marekani! Na huo sio mfano mzuri...
Jamani, basi kungekuwa na direction uniformity, kutoka kurasa hadi kurasa... mimi nilipotea baada ya dakika tano hivi, lakini kwa kuwa nilikuwa ninafanya uchunguzi, nikasema nibakie nichambue... ingawa kweli nilipotea.
Wataalam tupo, tuiteni, tutaifanyia kazi! Aibu gani hii?