Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Ni muongozo mzuri. Ila pia badala ya chuma anaweza kujenga ya miti, gharama yake ni nafuu sana.
Hivi hizo plastik sheet huwa zinapatikana wapi?
 
Ktk shamba darasa la dar kwa sasa ukiacha kilimo cha kisasa cha GH lkn pia imejengwa GH ya gharama nafuu hivyo utaeeza kupata idea jinsi wewe mwenyewe unaweza kuj
 
Ktk shamba darasa la dar kwa sasa ukiacha kilimo cha kisasa cha GH lkn pia imejengwa GH ya gharama nafuu hivyo utaeeza kupata idea jinsi wewe mwenyewe unaweza kuj
Naomba kufahamu gharama za kutengeneza GH ya saizi ndogo,na wapi naweza kupata vifaa.
 
Habari yako bwana Biashara2000. Nimramua Ku share mrejesho wa kilimo changu. Kwanza kabla sijasema zaidi, niseme tu nilikuwa naogopa sana kutuma pesa kwa MTU ambaye nimempata jf. Lakini kwa kuwa umaskini wangu umenikaba na wewe ukasema kuwa ungenitumia mafunzo kisha nilipie ikanipa ihakika. Sikupata nafasi ya kuja shamba darasa lkn niliweza kuanza kwa msaada wako. Niliamua kulima Miche michache sana km 112 HV tu ya majaribio kwa mbegu ya shanty na niliyumia mtaji wa 105,000 na mavuno yalikuwa kilo 3 kwa Mche kwa mwezi ambayo ni sawa na kilo 330 kwa mwezi nikuza buku kwa kilo ni 330 000 kwa mwezi na hii ni mbegu ya miezi 4 hivyo nategemea msimu ukiisha nipate mil 1,2 ambayo sio mbaya. Sasa hapo msimu wa pili nataka nitumie mbegu boea zaidi zemye mavuno mengi za hybrid kwani bado nataka nijikwamue kwa umaskini.

Nakushukuru lakini najipongeza mwenyewe kwa kuamua kuanza kilimo kuliko kusubiti subiri. Sasa HV sisubiri MTU aniletee maendeleo ntajiletea mwenyewe. Kila biashara INA ugumu si kilimo tu.
 
Hongera
 
Maswali yangu juu ya ulimaji wa nje ya hiyo Ghouse..
Hata kama kuna mvua nyingi hayo mazao yako hayataathirika?

Nimeona hapo unafanya umwagiliaji wa matone.vip gharama zake kwa hekari moja?

Changamoto ni zipi?kama hali ya hewa,magonjwa ya mimea?

Na soko lake la uhakika bila kusuasua?
 
Mkuu umesema unavuna matunda ya nyanya kwa muda wa miezi 8! Je, tangu kupanda mpaka kuanza kuvuna ni muda gani? Je, hiyo ni nyanya ya aina gani? Je, nyanya hiyo ni mwaka mzima au?
 
Mkuu umesema mbegu hizi huwa hazikuli kilimo cha nje ya gh yani kilimo cha wazi. Kwani kuna tofauti gani kubwa hasa kati ya kilimo cha gh na kilimo cha wazi ambazo zinasababisha hizi mbegu kukubali maisha ndani ya gh na sio nje?
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikisaidia watu ushauri wa namna ya kulima kilimo cha kisasa kwa greenhouse na bila gh. Nilichogundua mpaka sasa ni kuwa watu wengi hawana uwezo wa kifedha wa kujenga gh. Wengi wana uwezo na matamanio ya kulima kisasa nje ya gh yaani open field farming lakini kwa kutumia teknolojia ya gh km nilivyoelezea katika video yangu hapo juu.

Pia kuhusu kilimo ni kuwa watu wengi wanapenda sisi tuwafanyie utaratibu wote wa kilimo sio kuwapa mafunzo tu bali pia kuwatembelea na kuwawekea miundombinu ya kilimo cha kisasa katika mashamba yao hivyo kuwarahisishia kazi katika shughuli yao ya kilimo.

Hivyo tumeanzisha package mpya ya kuwapa wateja wanaohitaji kulima kisasa bila gh yaani open farming. Package hii gharama yake ni sh. 500,000 ambayo itakuwa na vitu vifuatavyo:

1. Mbegu za kisasa za hybrid za aidha Nyanya, Matango au Matikitiki maji,
2. Mbolea ya kuanzia
3. Madawa ya wadudu
4. Kutembelewa shambani na kusaidiwa kuwekewa miundombinu ya kusimamishia miche. Hapa tutakuelekeza namna ya kuandaa fimbo
5. elimu ya namna ya kulima step by step shambani kwako
6. Ushauri endelevu

Package hii inawafaa watu wale tu ambao wameamua kulima kisasa ili kujiongezea kipato na si kwa wale wanaopenda idea ya kuwa mkulima lakini hawafanyi hatua ya aina yoyote ile

Package hii inahusisha kulima katika eneo la kuanzia square meter 0 - 120

ambaye yuko interested kulima kisasa anaweza nipigia simu
 
Hii ndio Tanzania tuliokuwa tunaisubiri. Watu wanadhani Viwanda ni magodawn na mimashine kama ya Smelter kumbe hata kwako unaweza kutengeneza kiwanda cha nyanya kwa kuwa na garden ya nyanya/mboga mboga
 
Kwa dar shade net zinapatikana wapi mkuu.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A to Z Textile Mills Ltd... Ila siwafahamu, niliona kwenye uzi flani humu jukwaani. Jaribu ku-google. Ukiweza kupata ule uzi kuna namba zao za cm
 
kwa wale wanaoulizia net shedding na uv plastics wanaweza pata siku hizi ziko nyingi unaweza pata balton, A to Z, au ukienda pale arusha wako baadhi ya watu wanakwenda Nairobi kuleta kwa gharama nafuu kidogo. Lakini km unataka kujenga gh andaa kuanzia Mil.6-10

Ukishindwa jaribu kulima miche kadhaa nyumbani kwako. Km huwezi hata kulima ki bustani cha miche mia kadhaa utaweza gh? Hili ni swali nawaulizaga watu hawana jibu. Mtu ana ana mpango wa kuweka gh tokea 2005 lkn hadi leo bado. Je, km angeanza kulima shamba la wazi la kisasa tokea kipindi hicho leo angekuwa wapi? Chukua dakika kadhaa kufikiria UNGEKUWA WAPI KI KIPATO

Kilimo cha nyanya mfano kina faida kadhaa:

- Kuuza nyanya km nyanya
-kutengeneza tomato paste yaani nyanya iliyoagwa
-Tomato source
-Kutengeneza health drinks
-Kutengeneza smoothes

Na uzuri ni kuwa vyote hiviunaweza vifanya katika eneo hilo hilo lenye shamba inakuwa ni shamba na kiwanda. Kinachotakiwa ni KUTHUBUTU na kuondoa hofu na kutokusikiliza watu wenye negative thinking
 
Honestly kusema ukweli kabisa watanzania tunaongea sana lakini vitendo ni zero kabisa,
Umaskini tunajitakia wenyewe, Hofu, mashaka na kutokujiamini vimerudisha wengi kufikiria Ajira kama first option badala ya kufikiria Kuajiri watu..
We should act rather than counting!

 

Ok, vipi kwa mtu mwenye ekari moja ya shamba, vipi gharama zake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…