Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

kwa wakazi wa mikoa ya pwani, moro na dar ambaye ana shamba, huwa tunafanya site visit ktk shamba lako kisha kukupa elimu nzima shambani mwako. Piga simu kuweka appointment.
 
Kwanza kabisa nadhani aliyekwambia gh hiyo inakaa miche mia nne amekudanganya. Huwa inakaa miche 300 ikiwa imejaa. Inategemea mbegu gani unatumia, km unatumia km hii yangu unapata ndo moja na nusu kwa mwezi ktk mche mmoja. 1.5 x 300 ni kilo 450 kwa mwezi x miezi nane ni kilo 3600
Hiyo mbegu yako mbona huitaji jina lake umekomaa tu "hii yangu"
 
Mkuu nimesikia kuna mbegu inaitwa al jazeera eti ni nzuri, je una uzoefu nayo? uzao wake ukoje? Na gharama za kumtembelea mkulima ni sh ngapi kwa sasa?
 
Nimepata hamasa ya kufanya hichi kilimo cha nyanya. Ningependa kujua kama nyanya ili kustawi zinahitaji udongo wa aina gani? Eneo kama Kibaha is it favourable?

Eneo la kibaha na Dar yanafaa kabisa. Hiyo video ya shamba langu niliirekodia katika shamba langu la kibaha. Actually nyanya inastawi katika aina za udongo zote katika nchi hii, cha msingi lazima upime udongo wako kwanza kujua Ph yake na kujua ni kiwango kiasi gani cha mbolea inahitajika kuweka. Huweki tu mbolea kwa kuwa kuna ardhi inabidi iwe na kiwango chake kulingana na udongo wa eneo husika
 
Mkuu nimesikia kuna mbegu inaitwa al jazeera eti ni nzuri, je una uzoefu nayo? uzao wake ukoje? Na gharama za kumtembelea mkulima ni sh ngapi kwa sasa?

Kusema ukweli nimewahi kuisikia lakini sijawahi itumia hivyo sijui uzao wake.
 
Eneo la kibaha na Dar yanafaa kabisa. Hiyo video ya shamba langu niliirekodia katika shamba langu la kibaha. Actually nyanya inastawi katika aina za udongo zote katika nchi hii, cha msingi lazima upime udongo wako kwanza kujua Ph yake na kujua ni kiwango kiasi gani cha mbolea inahitajika kuweka. Huweki tu mbolea kwa kuwa kuna ardhi inabidi iwe na kiwango chake kulingana na udongo wa eneo husika
Udongo unapimwa wapi kwa kibaha mana nina eneo la wastani kila nipata mazao mavuno yanaku duni mno ama hayatoki kuna ndugu akaniambia kuna uwezekano wa chumvi ama magadi hivyo nikapime ila ndio hajui gharama wala ni wapi:!
 
Biashara 2000, kwa sasa huku kwetu mvua zinakaribia kuanza je naweza kupanda hiyo mbegu au nisubiri hadi mvua zikate?
 
Mwaka ndio unaelekea mwishoni kuingia mwaka mpya. Km ulikuwa na mpango wa kuanzisha shamba je, mpango umefikia wapi? na kwa mwaka huu umefanya nn? Je, utaendelea kusubiri hadi lini? Anza sasa ili ikifika mwakani km sasa uwe umefika mbali
 
Mi nipo Kagera, ila nikija Dar itabidi nikutafute nipate elimu. Ila bei ya nyanya huku Kagera ni sh. 600 hadi 800 kwa kilo. Nitatoboa kweli? Je kinacholimwa kwenye green house ni nyanya tu?.
 
Mwaka huu ndio unakwenda kuisha na kuingia mwaka mpya. Ni wakati wa kujithathmini kwa mwaka huu umeweza fanya nini cha kimaendeleo cha kukuingizia kipato. Je umejifunza nini ulikosea ili ujipange upya na ufanye vitu kivingine?

Kwa ushauri tu ningemshauri yeyote anayesoma hapa kuwa tafuta elimu popote pale hata km sio kutoka kwangu jifunze lakini cha msingi zaidi ufanyie kazi hata kama ni japo kiduchu. Mwaka 2017 january labda ulisema mwaka huu ungefanya kitu fulani cha kujipatia kipato lakini imefika december sasa hujafanya chochote. K, umepanga mwaka ujao ufanye kitu basi fanya kweli ili isije tena ikafika next year december hujafanya chochote. Ni bora uanze leo ili angalau uwe na cha kuonyesha. Angalia tu usije ukawa ni mwaka wa stress

Heri ya mwaka mpya
 
Endelea kukaza buti. Usisikilize maneno ya watu negative km baadhi ya niliowasoma humu. KM rose mhando alivyoimba usisikilize walioshindwa kwani ndio wenye maneno mengi
 
Tunashukuru kwa kutusadia elimu hii. Nilikwenda katika shamba darasa lenu. Aisee nie ni noma. Mungu awabariki sana. Nyie hamuogopi kuthubutu. Siku zote wanaoogopa kuthubutu ndio wanabaki nyuma. Siku zote waoga ndio hubaki myuma
 
Biashara 2000, kwa sasa huku kwetu mvua zinakaribia kuanza je naweza kupanda hiyo mbegu au nisubiri hadi mvua zikate?

Mbegu hii haijalishi ni kipindi cha mvua au la. Cha msingi tu fuata utaratbu wa kuandaa miche na jinsi ya kuweka matuta
 
Back
Top Bottom