Shuli
JF-Expert Member
- Nov 11, 2014
- 264
- 617
Huyu jamaa Biashara2000 yuko vizuri, ukiwa na nia ya kulima, mtumie pls. Mie nililipia PDF za Kilimo kwake lakini sikulima. Nikaja kuanza kulima mwaka huu mwezi wa saba, sikuvuna chochote maana Shamba langu lilikuwa na waangalizi wengine wakati Mimi nahangaika na kibarua kingine. Mwezi wa tisa mwishoni nilimpigia Biashara2000 anipe mwongozo wa kulima pilipili hoho, na nililima kwa kufuata mwongozo wake. Nilisimamia Shamba kwa wiki Mbili tu na hoho zikawa fresh kabisa, na nikawaacha vijana wangu waendelee na utunzaji wa shamba. Kwa sasa niko mbali na eneo la Shamba yapata wiki 3, lakini mambo yanaendelea vzr. Jumapili naanza kuuza hoho . kwa hiyo huyu Biashara2000 habahatishi mambo, kilimo anakifahamu vyema saana