Top ten ya Mikoa inayoongoza kuchangia pato la Taifa

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,624
2,000
Wewe una shida na Mkoa wa Dar.
Viwanda vyote vikubwa viko Dar na Watu wengi wako Dar, inapitwaje?
Shida unayo wewe mkuu ambae umeganda kama barafu,tukifanya sensa ya viwanda kwa sasa mkoa wa pwani unaongoza sasa sijui wewe unazungumzia Dar ya wapi.Nimekwambia mda utaongea kwani miaka 10 iliyopita gap ilikuaje hapo
 
mjombakim

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
1,179
2,000
Labda Dar kama jiji ila sio Dar kama mkoa.Jimbo la Carlifonia ni tajiri kuliko yote marekani ila jiji kuu ni New York jimbo jingine pengine ndivyo itakuwa but ushawishi wake unapungua kwa kasi sana.
ukingalia jiografia ya Dar na uwekezaji wake ulio kwisha kufanyika na unao endelea kufanyika ni dhahiri hakuna mikoa itakayo weza kuja kupita mapato ya Dar!
 
Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
1,542
2,000
Ndio tunataka taarifa za kichambuzi kama hizi JF. Sio mtu anaamka tu na kutoa yake kichwani bila source yoyote anakuja na kichwa "tafiti niliyofanya kuhusu.........." Ukimuuliza source ya data zako anakwambia fanya na wewe tafiti utaona.

Turudi kwenye mada, nchi imepanuka mkuu siku hizi watu hawajali saana kukimbilia mijini kama ilivyokua zamani zaidi zaidi wengi wanarudisha mpira kwa kipa(wanarudi mikoa waliyokulia kama miji waliyoenda kusaka ugali imewatupa mkono ama lah wanazidi jichimbia mikoa mingine sio dar dar dar tu.)
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
Niwasalimu kwa jina la JMT

Moja kwa moja kwenye mada,Kila mkoa na wananchi wake wanachangia sana kukuza uchumi wa Nchi na pato lao,lakini Ifuatayo ni Mikoa 10 ya wachapa kazi inayoongoza kuchangia pato la Taifa "GDP" zaidi kuliko Mikoa mingine.Ni muhimu kuibainisha na kuitambua ili kuipa credit stahiki.(Regions with the Largest Shares of GDP 2019),Figures in Million TZS.
Hivi kwanini Serikali ya Samia inamsaliti Mwendazake?!

Kwa miaka 3 mfululizo Serikali ya Mwendazake imetuaminisha Watanzania kwamba Dodoma ndiyo inachangia pato kubwa zaidi... yaani imeipiku hata Dar es salaam!

Yaani leo hii mnatuambia Dodoma haipo hata kwenye 10 Bora?! Au tayari wezi na mafisadi wameshaanza kupora mapato ya Dodoma na kuja kuyaficha kwenye mabenki ya Mabeberu Jijini Dar es salaam?!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
2016 tulitangaziwa kuwa Geita, Mwanza, Kagera ndiyo mikoa masikininsana Tanzania
Takwimu zile na hizi ni tofauti Chifu! Zile ni umaskini wa watu! Si unaona hapo Kilimanjaro haipo kwenye Top 5?! Lakini takwimu za "utajiri" wa watu lazima iwepo kwenye Top 3.

Yaani tofauti hapo ni kama unavyoona India yenye li-GDP likuuubwa lakini watu wake maskini wakati Norway yenye GDP ya kawaida compared to India, wao ndo wenye maisha mazuri zaidi!!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
Pili nitoe pongezi kwa Mikoa ya Mwanza,Mbeya na Geita kwa kuendelea kufanya vizuri,japo inashangaza kuona mkoa kama Morogoro, Lindi, Ruvuma, Kagera, Njombe, Mtwara na Kigoma kushindwa kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa maana mikoa hiyo ina kila kitu kinachoweza kuufanya kuongoza Kitafa. kama ardhi nzuri, mvua za kutosha, mifugo, madini, misitu bahari, maziwa nk
Hiyo mikoa ni ngumu kuchomoza kwa sababu haina investments! Huoni hapo kuna mikoa ya Kanda ya Ziwa? Mikoa yenye uwekezaji kama vile madini ndiyo inakuwa rahisi sana kuchomoza kwenye hiyo orodha!

Subiri Lindi na Mtwara zianze kuchimba gesi na mapato yake yarekodiwe huko! Nakuhakikishia hata Dar es salaam itapigwa gap ingawaje watu wa Kusini wataendelea kuwa maskini kwa sababu kiasi kikubwa cha GDP kinatona na pesa za wawekezaji!!
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,624
2,000
Hiyo mikoa ni ngumu kuchomoza kwa sababu haina investments! Huoni hapo kuna mikoa ya Kanda ya Ziwa? Mikoa yenye uwekezaji kama vile madini ndiyo inakuwa rahisi sana kuchomoza kwenye hiyo orodha!

Subiri Lindi na Mtwara zianze kuchimba gesi na mapato yake yarekodiwe huko! Nakuhakikishia hata Dar es salaam itapigwa gap ingawaje watu wa Kusini wataendelea kuwa maskini kwa sababu kiasi kikubwa cha GDP kinatona na pesa za wawekezaji!!
Mbeya,Iringa na Njombe hakuna migodi lakini inafanya vizuri kwa uwiano wa per capita japo kwenye mchango wa GDP iko Mbeya tuu hapo Iringa kabla ya kugawanywa ilikuwa inatokea top ten

Ni kweli migodi inachangia zaidi lakini sio endelevu na haireflects sana kwenye maisha ya mtu mmja mmja.So mimi naona bado fursa iko kwenye kilimo biashara na cha kimkakati
 
KVM

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
1,842
2,000
Ni kweli mkuu yaani mkoa kama Kigoma,Mara,Kagera nk iko njema sana lakini cha ajabu hakuna inachozalisha cha maana ,kiufupi inategemea mikoa mingine hii sio sawa
Na mimi nataka ishuke zaidi Ili tuheahimiane

Miaka 20 ijayo bila shaka inaweza.kujikuta at par na mikoa mingine, yaani nataka tufike mahala kama Jimbo la california kuongoza kiuchumi marekani lakini stii Jiji la Newyork ndio Jiji kuu la uchumi
Unafananisha vitu visivyofanana. Lini California iliizidi New York?
 
Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,380
2,000
Wewe una shida na Mkoa wa Dar.
Viwanda vyote vikubwa viko Dar na Watu wengi wako Dar, inapitwaje?

hujanielewa,
nilichomaanisha Dar haina "natural advantage" kwa maana viwanda au population ni vitu vinafuata mazingira flani haswa yaliyotengenezwa kama point yangu ilivyojikita

mfano Tanzania inasifika kuwa na rasilimali nyingi sana ila jiulize ni zipi zinapatikana Dar ?...

ukizipata hata tatu kubwa na special bhasi nipo wrong ila usipozipata, jua tu influence ya dar imetengenezwa na hivyo itazidi kupungua zaidi pale mikoa mingine inavyoendelea kukua
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,624
2,000
Hivi kwanini Serikali ya Samia inamsaliti Mwendazake?!

Kwa miaka 3 mfululizo Serikali ya Mwendazake imetuaminisha Watanzania kwamba Dodoma ndiyo inachangia pato kubwa zaidi... yaani imeipiku hata Dar es salaam!

Yaani leo hii mnatuambia Dodoma haipo hata kwenye 10 Bora?! Au tayari wezi na mafisadi wameshaanza kupora mapato ya Dodoma na kuja kuyaficha kwenye mabenki ya Mabeberu Jijini Dar es salaam?!
Kuna vigezo tofauti tofauti,vigezo vya makusanyo ya halmashauri nitofauti na vigezo kwa ngazi ya mkoa
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,624
2,000
Ndio tunataka taarifa za kichambuzi kama hizi JF. Sio mtu anaamka tu na kutoa yake kichwani bila source yoyote anakuja na kichwa "tafiti niliyofanya kuhusu.........." Ukimuuliza source ya data zako anakwambia fanya na wewe tafiti utaona.

Turudi kwenye mada, nchi imepanuka mkuu siku hizi watu hawajali saana kukimbilia mijini kama ilivyokua zamani zaidi zaidi wengi wanarudisha mpira kwa kipa(wanarudi mikoa waliyokulia kama miji waliyoenda kusaka ugali imewatupa mkono ama lah wanazidi jichimbia mikoa mingine sio dar dar dar tu.)
🙏🙏 Upatikanaji wa umeme na huduma zingine za msingi kijijini kunafanya kasi ya kuhamia mijini kupungua.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom