TOP 10 za Rais Kikwete

Ameweza: kuwa kimya kwa kashfa zinazowahusu rafiki zake kama vile Lo na Ro
 
Ameweza:
1.Kujaza marafiki zake kwenye Baraza la Mawaziri bila kujali uwezo wao wa kiutendaji.
2. Kuwashawishi Watanzania kwamba yeye ni Rais bora ila wanaomwangusha ni watendaji wake aliowateua yeye mwenyewe!


Ameshindwa:
1.Kutoa hotuba za kila mwezi kama alivyofanya Mkapa.
2. Kukamilisha miradi mingi hasa ya miundombinu iliyoachwa na serikali ya awamu ya tatu.
3. Kufanya chochote cha maana cha kuonyesha Watanzania kwa kipindi chote cha miaka mitano!
 
Ameweza sijui ameweza nini?
Ameshindwa ...Anatembea sana nadhani kuliko rais yoyote hapa duniani
 
AMEWEZA: Kuvunja Record yake mwenyewe ya kukaa zaidi ya siku 18 nje ya nchi kwa kukaa siku 22. Ameweza kumpeleka Mtoto wake Chodo Jandoni,Ameweza kuwa Rais wa kwanza kuwajulia watu afya Muhimbili mara nyingi zaidi kuliko yoyote,ameweza kushiriki Mazishi ya karibu wabunge wote na viongozi wengine kuliko Rais yeyote aliyetangulia...
AMESHINDWA: Kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania...
 
JK ameweza kuruhusu nnchi yake kuliwa na mafisadi, amewweza kulipa fadhila kwa wanamtandao hata wale vilaza kabisa kama Sofia Simba, Makongoro Mahanga,Adam Malima.
Ameweza kuunda baraza la mawaziri akitumia mzania wa kikanda zaidi kuliko uwezo wa mtu.
JK amekua mtawala wa kwanza wa Tanzania Kupimwa akili akiwa madarakani maana kuna mambo ambayo hata yeye mwenyewe anayafanya yanamtia mashaka kama yuko sawasawa , rejea mazungumzo yake mapema alipotoka Jamaika kwenye mabembea.
 
Amefanikiwa:
1. Kurudisha pesa za EPA japo si zote
2. Kujenga shule za sekondari, vituo vya afya na zahanati kwa wingi
3. Kujenga mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani
4. Kujenga chuo kikuu cha dodoma
5. Kusimamia mapato ya nchi vizuri
6. Kuweka wanawake wengi kwenye nyadhifa mbalimbali
7. Kuendelea kuimarisha mtandao wa barabara za rami nchini
8. Kutuletea kivuko kimpya pale kigamboni na sehemu zingine
9. Kupeleka mafisadi mahakamani japo si wote
10. Kuhimili msukosuko wa kiuchumi
11. Kuleta muafaka wa kisiasa zenji
N.K .........

Ameshindwa:
1. Kupeleka mafisadi PAPA mahakamani
2. Kudhibiti matumizi mabaya ya pesa za umma.
3. Kuleta mabadiliko ya kilimo
4. Kujenga viwanda kwa ajili ya malighafi za ndani (processing industry)
5. Kuimarisha shirika la umeme TANESCO ili tuondokane na mgao
6. Kuwawezesha vijana kupata ajira kama alivyoahidi kwenye kampeni
7. Kuwashughulikia akina KAGODA, MEREMETA, n.k
8. Kuimalisha uchumi wa nchi
9. Kufanya upanuzi wa miundo mbinu na facilities kwenye vyuo vikuu vilivyopo kama UDSM, SUA, MUHAS n.k
10. Kuboresha elimu kuanzia ngazi ya chini hadi juu (shule hazina walimu, vyuo havina walimu na vitendea kazi)
11. Vituo vya afya na zahanati havina wataalam wa kutosha
12. Kuwa na sera nzuri ya wastaafu (wazee wetu)

n.K .........
 
Ameweza: Nothing
1. Kupata kura asilimia 80% kwa kauli mbiu uliyovutia wapiga kura wengi
2. Kutishia uhuru wa Bunge, bila Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani nae
3. Ameweza kulinda rafiki zake walioshirikiana katika harakati za kisiasa
4. Kuvumilia kauli za kejeli kutoka kwa wananchi wake
5. Kuachia kila kiongozi kutoa kauli anazotaka mahali popote
6. Kubadilisha siasa za nchi kutoka Ujamaa na Kujitegemea hadi Ubepari bila kubadilisha Katiba
7. Ameweza kuwa na Baraza kubwa la mawaziri bila kujali ufanisi wao

Ameshindwa: Everything
1. Kutimiza ahadi karibu zote alizotoa wakati wa kampeni
2. Kulinda Katiba ya nchi kwa kuingilia uhuru wa Bunge
3. Kuhakikisha sheria za nchi zinafanya kazi ipasavyo hasa kwa watuhumiwa wa Ufisadi na viongozi wengine wabadhirifu
4. Kutoa majibu ya changamoto linazoikabili nchi (hasa kipindi cha financial crisis, na majanga mengine)
5. Kuhakikisha nidhamu kwa watendaji wote wa serikali anayoongoza, hivyo kuifanya serikali ionekane haina nidhamu
6. Kulinda Katiba ya nchi kwa kusimamia siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, au kuibadilisha kwa taratibu zilizopo
7. Kuimarisha umoja wa kitaifa, ushirikiano wa kweli na majirani (badala ya mataifa makubwa pekee)
8. Kufahamu kuwa shule ni wanafunzi na waalimu, hospitali ni madaktari, vifaa na dawa
9. Kudumisha na kurekebisha mipango ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wanachi wake
10. Ajira milioni 1
 
Ameweza: Kuziba masikio na kuendelea na safari za nje kwa manufaa anayoyaelewa yeye na walio karibu yake...

Ameshindwa: Kutekeleza kauli mbiu yake ya uchaguzi ya maisha bora kwa kila mtanzania...


Annina

Ameweza: kuwadanganya watanzania kuwa hakuna mwanafunzi wa chuo kikuu atakayefukuzwa chuo kwa kukosa ada, ajabu baada ya muda mfupi wanachuo wengi walifukuzwa kwa kukosa ada.

Ameshindwa: kutatua tatizo la ajira hapa nchini
 
Amefanikiwa:
1. Kurudisha pesa za EPA japo si zote
2. Kujenga shule za sekondari, vituo vya afya na zahanati kwa wingi
3. Kujenga mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani
4. Kujenga chuo kikuu cha dodoma
5. Kusimamia mapato ya nchi vizuri
6. Kuweka wanawake wengi kwenye nyadhifa mbalimbali
7. Kuendelea kuimarisha mtandao wa barabara za rami nchini
8. Kutuletea kivuko kimpya pale kigamboni na sehemu zingine
9. Kupeleka mafisadi mahakamani japo si wote
10. Kuhimili msukosuko wa kiuchumi
11. Kuleta muafaka wa kisiasa zenji

N.K .........

really?

Ameweza
kutufanya tumchague
kugundua matatizo yetu

ameshindwa
kutufanya tumuamini
kutatua mataizo yetu
 
Ameweza kuligawa Taifa la Tanzania katika makundi ambayo yameuangamiza Utaifa na uzalendo uliojengwa na waliomtangulia!

Ameshindwa kuwathibiti wateule wake waliovurunda kazi alizowapa ingawa kuna ushahidi wa kutosha; mfano akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Idris Rashid.
 
AMEWEZA kuwafanya wanajimu nchini kuwa viongozi waandamizi na wasemaji wa ikulu.
AMESHINDWA kuzuia unit ya umeme isipande bei baada ya kuwahakikishia wananchi wake kwamba haitapanda.
 
Ameweza kwenda kinyume na utaratibu wa CCM bila kufukuzwa chama wala ku-'Nnauyewa'...(utaratibu wa chama ni pamoja na kutosema ukweli hasa vigogo fulani wanapoamua kupora mali za nchi). Ameshindwa kuunda chama chake mwenyewe na kujitoa CCM kama alivyofanya Bingu wa Mutarika Rais wa Malawi, kuonyesha kuwa kweli hakubaliani na ufisadi ulioko CCM au vyama vingine vya kisiasa vyenye lengo la kushika madaraka tu. Ameshindwa angalau kujiunga na vyama vyenye uzalendo kuliko CCM. Kwa hiyo ameweza kuendelea kuthibitisha kuwa HATAGOMBEA 2010.....Kwa maana hiyo AMEWEZA KUWA RAIS WA MKONO MMOJA.
 
Ameweza: kwenda kupokea shahada yake ya uzamivu huko Turkey

Ameshindwa: kutuma salaam za rambi rambi kwa wafiwa walio poteza ndg zao 17 katika mauaji ya kutisha Musoma!
 
mimi naona amejitahidi kuliko maraisi wawili walio pita mambo mengi anayo lalamikiwa yanatokana na uongozi mbaya uliopita.
 
Back
Top Bottom