[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Yaani mi nachekaga kimoyo moyo.
Kuna siku nilikuwa na rafiki yangu, yeye mweupeee, alafu mimi cheusi mangala, sasa ile tunapita wakaanza "aaah fanta na coca hao, kitu cheupe na cheusi rangi za mvuto" mie nikacheka alafu nikawapa tu hi alafu wakaendelea kujiongelesha, cheupe hakujibu chochote wala kuwasalimia, weeeeh acha waanze kumkashifu "we cheupe weupe wenyewe wa mkorogo nawe unajifanya mzuri.....cheki mwenzio rangi ilivyotulia,mtoto rangi adimu....." Jamani tulicheka yaani kutoka kusifiwa hadi kukashifiwa. Sasa hapo tusingeitikia wote kila mmoja angepewa kichambo sawasawa na rangi yake.