Tony Blair Deeply Regrets 'ALL' Lives Lost in Iraq War | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tony Blair Deeply Regrets 'ALL' Lives Lost in Iraq War

Discussion in 'International Forum' started by Uwezo Tunao, Jan 21, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waziri Mkuu wa Zamani nhini Uingereza (1997 -2007), Tony Blair, leo hii alasiri amekiri majuto mazito moyoni kwa maafa nchini Iraq wakati wa vita.

  Kiongozi huyu mstaafu alielezea jinsi anavyoendelea kukumbwa na MISONONEKO MIZITO SANA MOYONI kufuatia maafa yaliotokea katika vita hivyo.

  Alifafanua kwamba anasikitikia sana maisha ya ama wanajeshi wake, Wamarekani, Wairaki, Watumishi wa Mashirika ya kimataifa na raia wa kawaida pale Iraq.

  Ndugu Blair alikiri hayo leo hii saa 10:53 alielezea hisia zake hizo wakati akiwa kikaangoni mbele ya Tume ya Uchunguzi juu ya ushiriki wa Uingereza katika vita nchini Iraq (the British Commission of Inquiry into Iraq War - BCIIC) ikiongozwa na Mwenyekiti wake John Chilot.

  Pamoja na yote, Waziri Mkuu mstaafu huyo alisisita kwa uzito wake kwamba vita dhidi ya Iraq ilikua haikwepeki kwa vyovyote vile kutokana na vikundi haramia na hatari vikifadhiliwa na mikono mibaya huku vikiwa vimepandikizwa chuki za kidini na kuhatarisha maisha kwa ulimwengu mzima.

  Kikao cha tume kitaendelea siku ya jumanne wiki ijayo kwa kuleta viongozi wengine wazito zaidi kikaangoni.

  Kwa habari zaidi, fuatilia katika mikondo hii: Iraq Inquiry na C-SPAN | Capitol Hill, The White House and National Politics

  HOJA YANGU:

  Tunajifunza nini kama nchi na vile vita vya Iraq na misingi ya kuchochewa au kufadhiliwa migawanyiko kwa misingi ya kidini ndani ya taifa letu?

  Na kitendo cha kiongozi wa ngazi ya juu duniani kama Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza anapowekwa kikaangoni vikali kiasi hiki panapoonekana kuna MASWALI MAZITO YANAYOHITA MAJIBU KITAIFA, sisi hapa kwetu somo ni nini hadi hapo kwa viongozi wetu ama walioko madarakani au wanaopumzika nyumbani?

  SOURCE: C-Span2 TV.
   
 2. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Peleka jukwaa la kimataifa, International Forum
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Katika taifa letu kuna uwezekano kiasi gani na sisi kuwaweka kikaangoni viongozi wetu ama walioko madarakani au wastaafu, mbele ya vyombo vya kisheria, kutolea majibu maswali mazito kitaifa yakotanayo na utendaji wa serikali wanazoziongoza?
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,289
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Mnafiki mkubwa huyu. Nashangaa kwa nini ile mahakama ya the Hague inakosa meno kwa wahalifu kama Blair na Bush.Hawa wakwetu nao wajue kuwa siku moja tutawaundia tume.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lakini katika historia ya taifa letu hili limewahi kutokea hata mara moja au hata katika bara la Afrika kwa ujumla?

  Kama jibu ni hapana, huenda ikawa ndio maana viongozi wetu barani kwetu hufanya mambo ya kuwasikitisha sana wananchi wao bila woga wowote wa kuja kuhojiwa na mtu au kuwajibishwa kabisa?
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  Katiba ni SHERIA MAMA ambapo sheria zote za nchi hupatikana na kufanyiwa kazi.

  Wakati sheria za kawaida hutungwa na wawakilishi wa wananchi kwa maana ya Wabunge kule bungeni Dodoma, Katiba ni sheria mama yenye UPEKEE KATIKA JAMII HUSIKA ambapo utungaji wake ni JUKUMU LA RAIA WOTE katika nchi.

  Sasa Ugomvi mkubwa kati ya vyama vya upinzani na Wanaharakati, kwa upande mmoja, dhidi ya CCM ni katika kusema kwamba NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA katika kutekeleza wajibu wao kutunga Katiba Mpya.

  Lakini wao CCM wakiongozwa na Mafisadi wao wanasema Rais ANATOSHA KUTUTUNGIA TU KATIBA KWA KUSHIRIKIANA NA LOWASA, CHENGE na akina ROSTAM AZIZI kututungia tu katiba hiyo kupitia KIKUNDI CHA MADALALI WAO KWA JINA LA WATAALAM WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

  Sasa swali hapa ni kwamba; tangu lini Watanzania tukasikia KIKUNDI CHA Mi-FISI wakatunga sheria murua ya kulinda maslahi ya SWALA jangwani???

  UWEZO TUNAO, haki hapewi mtu bali ni kwamba haki hufuatwa na kuchukuliwa. Kazi inaendelea kila kona ya nchi kwa watu tunaojali maslahi ya taifa letu. Hakuna kulala!!!
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mnafiki mkubwa you regret now baada ya kuwa ameishatoka madarakani miaka kadhaa, totally unacceptable you regret wakati your are the responsible for the lives of the people which have been lost.
   
 8. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  that war was unavoidable
   
Loading...