Tonda DSM Iringa yapata ajari

Milindi

JF-Expert Member
Mar 3, 2009
1,462
745
Nakaribia kufika Iringa. Na upendo bus.tonda imepata ajari a kugonga semi iliyokuwa imeharibika pembeni.inasemekana driver Kafa.
majeruhi na abiria wengine wa tonda tumewabeba ndani ya upendo zaidi nikifika Iringa
 
Aisee,pole zao waliojeruhiwa na waliopoteza ndugu but ilikuwa mitaa gani vile?
 
Nakaribia kufika Iringa. Na upendo bus.tonda imepata ajari a kugonga semi iliyokuwa imeharibika pembeni.inasemekana driver Kafa.
majeruhi na abiria wengine wa tonda tumewabeba ndani ya upendo zaidi nikifika Iringa

Pole sana jamani. Madereva walaaniwe wote, carelessness
 
Nadhan Ni Muda Muafaka wa polisi Kufanya Kazi Yao Kwa Kuzingatia sheria za Usalama Barabarani Na kugundua Hapa Bila shaka itakuwa Ni Lori ambalo limeharibikia Kati kati ya Barabara na Kufanya Uzembe wa kutoweka alama yoyote ya Tahadhari kama reflactors
 
Hawa madereva waruwaru watatutaliza jamani. Mungu awasaidie majeruhi wapone waendelee na majukumu yao
 
MUNGU wangu! Tutafika kweli! Poleni majeruhi wote na Rest In Peace kwa yeyote yule alipatwa na mauti ktk ajali hiyo.
 
Waliokuwa siti za mbele wanasema dereva alikuwa speed na mbele kidogo ya mikumi alikuwa akishuka kwa kasi mbele semi ilikuwa ime park. Ile ku over take akakutana na semi nyingine inapandisha akabidi arudi na kuingia semi. Iliyo park.kwa chiyo dereva alibanwa na usukani na kukatika mguu. Na neno alilosema ni maamaaaa hakuweza kuonyesha tena na ilichukua muda mrefu sana kumchomoa alvyokua amebanwa.alifariki wakati anakimbizwa mikumi.MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMIN.
 
nilipanda bus hili mwezi wa 11 linaondoka iringa saa 5 asubihi, hadi tunafika kitonga tayari nilikuwa na mashaka na dereva kuto kuwa mzoefu wa kuendesha mabasi, nikamuuliza dada mmoja ambaye ndio kondakta wa bus hilo , alicho jibu ni kuwa dereva wao hana uzoofu na njia ya iringa alikuwa anaendesha njia ya mwanza, hakuna aliyeridhishwa na majibu hayo hadi tunafika moro kuna makosa zaidi ya 5 ya udereva alikuwa ameyafanya mm nilishuka moro na kubadili gari kwani niliona hatari inayokuja mbele yetu
RIP dereva ee mwenyezi mungu wape nafuu majeruhi wa ajali hiyo
 
Back
Top Bottom