Toleo Jipya: Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania

Leo hii nimeguswa sana na kura za maoni zilizofanyika Zanzibar pasipo kuelewa haswa malengo yake kitaifa zaidi ya kuchanganyikiwa. Ni rahisi sana kwa mtu yeyote kuchukulia uhalali wa kura hizi kama hataweza kuzingatia mfumo mzima wa kiutawala wa nchi yetu.

Majuzi nimemsikia rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh.Kikwete akihutubia kwa mara ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu ujao, na katika hotuba yake amezungumzia pia matumaini yake na wananchi kuhusiana na zoezi zima la kura za maoni yanayofanyika Visiwani na hata kudiriki kutoa mifano ya nchi kama Kenya, Zimbabwe S.A na Kongo, ili kuonyesha jinsi gani zoezi hili linaweza kuondoa uhasama uliopo baina ya vyama na wafuasi wa vyama viwili vya CUF na CCM hali nchi hizo zimetumia mfumo huo Kitaifa (federalism) na sio sehemu moja ya nchi zao.

Kwa hiyo pasipo kufikiria haya ni matumaini mazuri sana kuyasikia lakini sidhani kama yana ladha nzuri ukiyaweka kinywani kwa sababu nyingi na za msingi hasa ukizingatia mfumo wa kiutawala wa nchi yetu. Na kutokana na hilo yamekuja maswali mengi kichwani mwangu ambayo nimeshindwa kuyapatia jibu.

Kwanza tutazame muundo wa kiutawala kwa nchi yetu. Ni hivi karibuni tu bunge letu lilishikwa na mgogoro mkubwa unaohusu nafasi ya Zanzibar katika Muungano wetu. Mgogoro ambao unanikumbusha sana mgogoro wa kiutawala uliopo baina ya Canada na jimbo la Quebec ambao umedumu kwa miaka mingi sana pasipo ufumbuzi wa regulations zinazohusiana na maswala ya Kiuchimi, kodi za mapato na rasilimali..

Na nakumbuka vizuri Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akinukuu katiba yetu ya Muungano kwa maelezo kwamba Zanzibar sio Taifa (a nation) isipokuwa tuna Taifa moja tu nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Likaja swala la Zanzibar kama nchi nalo likapingwa pamoja na kwamba Zanzibar ni nchi inayoongozwa na rais wake, bunge lake na mahakama ktk muundo mzima wa serikali unaoiwezesha kuitwa nchi. Na hakika hadi leo hii nashindwa kuelewa nafasi ya Zanzibar ktk Muungano wetu hata baada ya kufikia muafaka baina ya chama cha CUF na CCM ulofanikisha upigani wa hizi kura za maoni.


Sielewi kama zoezi hili la kura za maoni zimelenga kuondoa tatizo la Muungano ama kuondoa chuki baina ya viongozi wa vyama na serikali ya Zanzibar ktk kuimarisha udugu baina yao. Na sielewi pia mafanikio yoyote ya hizi kura za maoni utawezesha vipi kujenga sheria zinazohusiana na kero za Muungano wa nchi zetu kisheria ikiwa nguvu kubwa imewekwa ktk kuridhisha matakwa ya vyama vya kisiasa.

Swali kubwa linalojitokeza ni mamlaka haya yataweza vipi kujenga na kuimarisha mfumo mzima wa uchaguzi nchini ikiwa vyama viwili vinaweza kukubaliana kuunda serikali ya mseto (share power) kabla ya uchaguzi mkuu kuvipa mamlaka ya kuunda serikali hiyo chini ya kifungu gani cha katiba ikiwa nchi yetu ni moja itawaliwe na mifumo miwili tofauti ya kiutawala.

Najiuliza ni vigezo gani vimetumika haswa kufikia maamuzi ya kuundwa kwa serikali ya mseto mbele ya matokeo ya uchaguzi mkuu pasipo kushirikisha bunge la Muungano, vyama vyote vya kisiasa, mwanasheria mkuu na taasisi zote za kiutawala zinazoweza kufikia maamuzi ya busara kuhusiana na kero za Kitaifa na sio kero za upinzani baina ya vyama viwili pasipo kutumia ushahidi wowote wa Uchaguzi mkuu.

Kisha sijawahi kusikia TAIFA MOJA (a nation) yenye kuunda serikali ya mseto ktk nchi moja kisha ikatawaliwa na chama kimoja Kitaifa.
Kama nilivyosema hapo juu rais wetu Mh.Kikwete ametoa mifano ya Kenya, sidhani kama hao Kenya wamefikia muafaka wa kuunda serikali ya mseto kwa jimbo moja la kanda ya ziwa au hata hao Zimbabwe au nchi za Marekani na Uingereza.

Kama Zanzibar sio Taifa wala nchi isipokuwa tuna nchi moja ya Jamhuri ya Tanzania. Au itumike lugha yoyote ile kutenganisha Visiwani na bara ktk muundo wa serikali hizi bado kikatiba sioni sheria inayoviwezesha vyama viwili kuunda serikali ya mseto ktk sehemu moja ya taifa kabla hata ya uchaguzi mkuu.

Je, kilichofanyika ni kuungana kwa vyama hivi (coalition) ili kuunda nguvu moja ya ushiriki ktk kutafuta ushindi wa uchaguzi mwezi October na sio kuunda serikali ya mseto (share power) kama tunavyotangaziwa.. Na kama kilichoundwa ni serikali ya mseto, Je sheria ya uchaguzi inaruhusu kuundwa kwa serikali ya mseto hata kabla ya matokeo ya uchaguzi mkuu na pia sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Labda watu watakiwe kwa nguvu kusoma kijitabu hiki ndio wataelewa kwanini uhuni umefanyika Zanzibar.
 
Pamoja na kwamba sijapiga hodi rasmi, hii nimeipenda. KITABU HIKI NI USHAHIDI WA UWEPO WA VIONGOZI WALIOTAYARI KULITUMIKIA TAIFA HADI UPEO.:confused2:
 
asante sana mkuu, nchi itajengwa na wenye moyo kama wewe, na hakika malipo yako yapo peponi..
 
Tusome kitabu hiki. Kisha tuache uoga, TUPAMBANAE na mafisadi kama Nyerere. Kwani uoga, vitisho kuwa CCM ikiondoka madarakani kutakuwa na fujo nchini ndiyo mbinu ya mwisho ya CCM ya mafisadi kubaki madarakani. Huo ni uongo, period.
 
Natumaini kitasaidia katika kuchangia mwamko wa kuwawajibisha viongozi wetu bila kuwachekea chekea..

Mze Nakubali kazi yako maana kilikua ni kazi kweli kukipata.

Tatizo lingine wengi hawapendi kusoma Hoja za Mdingi wetu maana yote aliyokua akiyapiga vita ndo yamepata kushika kasi ya ajabu sasaivi
 
Mze Nakubali kazi yako maana kilikua ni kazi kweli kukipata.

Tatizo lingine wengi hawapendi kusoma Hoja za Mdingi wetu maana yote aliyokua akiyapiga vita ndo yamepata kushika kasi ya ajabu sasaivi


Kukisoma kitabu hiki kutawasaida watu kwanini kuelewa kwanini mimi kama Nyerere siamini katika serikali ya Tanganyika.
 
mwanakijiji kwanza mimi mwana kitongoji nakupongeza kwa kazi hiyo na mola akulipe nahisi sasa ni wakati wa kusoma na kuwafanya hata watawala wetu wafanye hivyo all vision na mission ziko wazi na kwa sababu hiyo utakua unafuatilia hata nakala zake wameficha hazipatikani kamwe na huenda ikawa chanzo cha matatizo katika jamii
 
well.. labda MMM hakuwepo wakati huo!! lakini siyo jambo jipya kuandika na kuhariri maandishi ya wale waliotutangulia.. ndio maana utaona hata biblia na qurani zimepangwa na watu vizuri baadaye na hata maandishi ya kina Plato na wenzake yamehaririwa baadaye.

Kitabu cha Nyerere kilikuwa na makosa mabaya sana ya matumizi ya herufi. Itakuwa ni uzembe kuendelea kusoma lugha ya kiswahili ikiwa imemomonyolewa... Hii inaitwa "journalistic liberties".. Unaweza ukakipitia na kulinganisha mpangiliko wangu wa kihariri na kijitabu cha awali.. kama kuna makosa tunaweza kujadiliana na kuona kwanini nimechukua maamuzi fulani. And no.... sometimes we have to deal with the ghosts of our history past..
Nimependa ulivyomjibu kwa upole na kiwango cha ufahamu wake. Eti kauliza waatanzania tuna akili Daaah!! ikiwa kitu fulani hukijui hamaanishi hakipo duniani
 
Sioni sababu ya kukipiga marufuku kitabu hiki, kwa serikli ya wamu ya pili, mamabo yaliyo andikwa humu ni ya kawaida sana. na ya ukweli, sasa mambulula wa ccm hawajui kusoma au ni wavivu walisoma kurasa 2 wakamshauri Rais Akipige marufuku, SHIT wakubwa hao, sijui wako wapi siku hizi.
 
Back
Top Bottom