Kimsingi wanawake wana tabia ambazo hata wao wenyewe hawazijui,pamoja na hilo kuna mambo ambayo wewe umeyafanya ambayo kwao yanaleta tafsiri tofauti na wewe unavyoyaona
Kwanza kabisa kimsingi unapokuwa unamtaka mwanamke na ukamuonesha uhitaji mkubwa sana jua huyo huwezi kumpata kwakuwa kawaida mwanamke akijua unamuhitaji mara nyingi huanza kuhisi tofauti na hali hiyo hupelekea kuanza kukuona kama wewe humuhitaji
Hili linasababishwa na ile hali ya mwanamke kujisikia salama,wanawake huwa wanazama sana mapenzini hasa pale ambapo anapokuwa hana uhakika na penzi lake kwa anaempenda,jaribu kuangalia wanawake wanawapenda kupindukia waume au wapenzi wao ni wale ambao wako kwenye mahusiano na watu ambao hawaeleweki kabisa,ni uongo mwanamke akisema akipata mwanaume ambae atamhakikishia penzi lake atampenda
Wanawake wakijua kuwa wanaweza kuachwa muda wowote ule basi huwapenda sana wanaume hao
Kwenye ishu yako wewe ni kwamba kwanza wakati wa ubachela ulikuwa ni mtulivu kiasi au sana,hili liliwafanya wanawake wasiwe na wasiwasi na wewe kwani "watakukuta tu",yaani wewe walikuwa wanakutazama kama mtu fulani wa uhakika hivi kwasababu ya utulivu wako jambo hilo liliwafanya wakuone kama "hufai kwa sasa"
Kingine ni kuwa walikuwa "wanahisi huwezi" na hili lilitokana na wewe kutokuwa na mahusiano mengi au kutokuwa nayo kabisa,jiulize ni kwanini wale vicheche ndio hao hao wanagombaniwa na wanawake huku mitaani? Jibu rahisi ni kwasababu wanawake wanakuwa wanavutiwa nao sana kwasababu hiyo hapo juu
Ulipokuja kuoa hapo ndipo wale ambao walikuwa wanakuona "huwezi" wamekuja kugundua "unaweza",wale ambao walikuwa wanadhani "watakukta tu" wamejua sasa hawatakukuta,hali zote hizi zinawafanya wasijisikie amani kuhusiana na wewe kwenye suala la mapenzi kitu ambacho kinawafanya uwavutie na kutaka mahusiano na wewe
Hiyo iko hivyo na wala usidhani kuna chochote kipya hapo, wanawake wapo hivyo
CC:
Himidini ....!!