Toka mtandoani : umri wa Michael Jackson

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,095
Reaction score
828,901
Nimeinakili kutoka group la Whatsapp. Simjui mwandishi but its worthy sharing. Japo ningefurahi kumjua mwandishi ili nimpe credits zake. Hili kwangu ni andiko bora kwa mwezi huu.
_________
Michael Jackson alikuwa ni binadamu mwenye ndoto nyingi lakini Ndoto zake 2 kuu maishani zilikuwa ni:

1. Kwanza ni kuwa mwanamziki mkubwa zaidi duniani wa Pop.

2. Kuishi miaka 150.

Baada ya kuifanikisha ndoto yake ya kwanza kwa ufanisi mkubwa akiwa na miaka 25 tu aliamua kuanza kuwekeza kwenye ndoto yake ya pili ambayo kwa wakati huo ilikuwa ndiyo takwa lake kubwa.

Ili aweze kuishi miaka 150 (Karne moja na nusu) aliamua kufanya mambo yafuatayo:

1. Aliajiri madaktari binafsi 12 wa kumchunguza mwili wake wote hadi nywele na kucha kila siku.

2. Ilikuwa ni lazima chakula chake kipitie maabara kupimwa kabla hajala.

3. Aliwaajiri wataalamu 15 kufuatilia mazoezi, kazi na kila jambo alilofanya kila siku.

4. Alitengeneza kitanda maalumu kilichokuwa na uwezo wa kufanya 'regulation' ya hewa.

5. Watu 50 waliwekwa tayari kujitolea viungo vyao kama angepata dharura yoyote. Aliwalisha watu hao, aliwatunza na kuwalipa mshahara kila mwezi kwa kazi hiyo.

Baada ya kufanya hayo alikuwa na uhakika wa kuishi karne moja na nusu bila mashaka yoyote. Lakini June 25, mwaka 2009 akiwa na miaka 50 tu moyo wake ulizima ghafla na ndoto yake ikawa imefika mwisho.

Timu ya madaktari wake bingwa 12 haikuweza kuzuia pumzi yake isiondoke. Wale watu 50 waliowekwa 'standby' kumpa viungo hawakuweza kumsaidia. Akazima ghafla kama taa ya umeme iliyoishiwa luku.

Pamoja na juhudi za madaktari wengine kutoka Calfornia na Los Angeles hawakuweza pia kuokoa maisha yake. Mtu ambaye kwa miaka 25 alikuwa hawezi kunyanyua unyayo wake bila ushauri na ruhusa ya madaktari akawa kafika mwisho bila kutimiza ndoto yake ya kuishi miaka 150.

Safari ya mwisho ya Michael Jackson ilishuhudiwa moja kwa moja na zaidi ya watu milioni 3, rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa. Ndiye mtu aliyepata kuagwa na watu wengi zaidi katika historia ya dunia tangu enzi za Pontio Pilato.

Siku aliyofariki mitandao mikubwa ya Wikipedia, Twitter, Yahoo, AOL's instant messenger ilielemewa na mzigo wa watumiaji waliokuwa wakisaka taarifa za kifo hiki hadi ikaacha kufanya kazi. Google pia ilivunja historia ya matumizi yake kwa siku ile.

Michael Jackson alitaka kupambana na kifo lakini hakuweza hata kufikia nusu ya umri aliopenda kuuishi. Mtu aliyekua na uwezo wa kufanya lolote ili aweze kuishi umri autakao lakini alizima kama mshumaa. Biblia inasema ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Hakuna. (Mathayo 6:27).

Ikiwa hatuwezi kuongeza hata kimo chetu basi hatuwezi kufanya lolote kuhusu hatma ya maisha yetu. Michael Jackson alifanya yote yaliyowezekana ili aishi miaka 150 lakini hakufika hata nusu ya umri huo. Lakini kuna mzee asiye na uhakika wa milo mitatu kule Tandahimba, Rombo, Ngara au Tukuyu ameishi umri mkubwa hata mara mbili ya Michael Jackson. Ni kwa neema tu.

Uhai na uzima tulionao ni zawadi kutoka kwa Mungu. Sio kwamba tunastahili kuliko wengine, hapana. Sio kwamba tumejitunza kuliko wengine. Hapana. Ni kwa neema tu. Hata hatma ya maisha yetu vipo mikononi mwa MUNGU mwenyewe.

Ishi kwa upendo na kila mtu. Ukipata madaraka usiyatumie kunyanyasa wengine. Damu zao zitakulilia daima na siku ya mwisho utaulizwa.

Hapa duniani hatuna mji udumuo bali sote twautafuta ule ujao. Ishi kwa amani na watu wote. Maandiko yanasema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi (Ayubu 14:1). Tumuombe Mungu atuepushe na kiburi, atufundishe kuzihesabu siku zetu na kutujalia mwisho mwema.!

#TunaSimamaKwaNeema#
 
Mkuu Mshana hivi hofu juu ya kifo inaletwa na nini!?.. Vp kama tungejua huko mtu anakoenda baada ya kufa ni pazuri zaidi kuna mtu angeendelea kubaki duniani!?
 
hakuna ukweli hata mmoja hapo kumuhusu MJ, hayo yote yalikuwa ni mawazo na fikra tu za watu pengine labda sababu ya umaarufu wake na pesa zake...ukifatilia documentary nyingi utaona jinsi gani MJ hakufurahia maisha ya umaarufu hasa kipindi cha utoto sababu baba yake alikua hampi muda wa kuutumia utoto wake.

kwenye hilo la kutaka kuishi miaka 150 nalo sidhani kama lina ukweli, hapa duniani hakuna asiyejua kila mwanadamu ana ukomo wake wa kuishi hata awe na pesa kiasi gani....tena kwa karne hizi za sasa mtu kufika miaka 100 sio rahisi hivyo,

nadhani yeye mwenyewe alifika point alichoka hata kuishì kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya aliyokuwa nayo ambayo kulingana na maelezo yake alisema amerithi kutoka upande wa baba yake (matatizo ya ngozi)

kuna mahojiano alifanya na Oprah aliulizwa kuhusu kile kitanda ambacho watu walikuwa wanasema anakitumia ili kuMaintain ujana na mambo kama hayo mliyosema humu.....alikanusha mwenyewe,

ni kweli MJ alikuwa na mapungufu yake kama binadamu wengine ila haya mambo ya kumtolea mifano isiyokuwa na ukweli sio vizuri,

tumuacheni MJ apumzike aisee....tulimsema akiwa hai inatosha.
 
Kwahiyo tufuate lipi la kwako au la mtoa mada
 
Mkuu Mshana hivi hofu juu ya kifo inaletwa na nini!?.. Vp kama tungejua huko mtu anakoenda baada ya kufa ni pazuri zaidi kuna mtu angeendelea kubaki duniani!?
Hapajulikani ndio maana... Halafu ule uchungu na makali ya roho kutoka ndio vinaogopwa zaidi
 
hakuna ukweli hata mmoja hapo kumuhusu MJ, hayo yote yalikuwa ni mawazo na fikra tu za watu pengine labda sababu ya umaarufu wake na pesa zake...ukifatilia documentary nyingi utaona jinsi gani MJ hakufurahia maisha ya umaarufu hasa kipindi cha utoto sababu baba yake alikua hampi muda wa kuutumia utoto wake.

kwenye hilo la kutaka kuishi miaka 150 nalo sidhani kama lina ukweli, hapa duniani hakuna asiyejua kila mwanadamu ana ukomo wake wa kuishi hata awe na pesa kiasi gani....tena kwa karne hizi za sasa mtu kufika miaka 100 sio rahisi hivyo,

nadhani yeye mwenyewe alifika point alichoka hata kuishì kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya aliyokuwa nayo ambayo kulingana na maelezo yake alisema amerithi kutoka upande wa baba yake (matatizo ya ngozi)

kuna mahojiano alifanya na Oprah aliulizwa kuhusu kile kitanda ambacho watu walikuwa wanasema anakitumia ili kuMaintain ujana na mambo kama hayo mliyosema humu.....alikanusha mwenyewe,

ni kweli MJ alikuwa na mapungufu yake kama binadamu wengine ila haya mambo ya kumtolea mifano isiyokuwa na ukweli sio vizuri,

tumuacheni MJ apumzike aisee....tulimsema akiwa hai inatosha.
Kwamba hata ishu ya madaktari na waangalizi lukuki ilikuwa uongo?

hakuna ukweli hata mmoja hapo kumuhusu MJ, hayo yote yalikuwa ni mawazo na fikra tu za watu pengine labda sababu ya umaarufu wake na pesa zake...ukifatilia documentary nyingi utaona jinsi
Hapa nitapingana nawe
 
Hivi Nini kilimuua !??
Na hayo Mambo watu waliyajuaje km kweli alitaka iwe hivyo?
Niliwahi sikia historia yake kuwa ;
MJ amekuwa kwenye taasisi ya kifrimason tokea akiwa mdogo sana.
Hao ndiyo waliomkuza na kumuweka kwenye ramani ya muziki akawa na umaarufu sana na akawa tajiri mkubwa.

Baada ya kuwa star mkubwa na utajiri wa pesa, majumba ya kifahari, magari, n. K.
Akaanza kuwa na kiburi na dharau kwa wakubwa zake wa taasisi hiyo.

Pia , MJ alichoka kumtumikia shetani. Akawa anaanza kutaka kujitoa huko. Aliona sasa ni muda wa kumrudia Muumba wake.

Ndipo jamaa wakamshusha.
Ila yote haya ni fununu tu. So za kuambiwa uchanganye na zako pia.
 
Back
Top Bottom